Video ya wimbo wa BABA NA MAMA wa dogo rama msanii wa tegemezi wa twanga pepeta sasa umekwisha kamilika hii ikiwa ni nyimbo ya 3 kufanyiwa kutoka katika album ya DOGO RAMA iliyopewa jina la KILIOMETA 10000 nyingine zikiwa ni CHUKI ZA NINI,IMANI YA MAPENZI,KILOMETA ELFU 10000 na sasa imekamilia ya BABA NA MAMA ambapo nyimbo hiyo amemshirikisha mwanana dada nguli wa miondoko ya dansi KHADIJA MNOGA KIMOBITEL,hii ikiwa ni katika kukamilisha mpango wake wa kutolea video nyimbo zake zote zilizo kwenye lbum yake hiyo mpya ambayo yupo mbioni kuizindua akiwa na wana kilometa ingawa bado hajabainisha ramsi ni lini ataizindua album hiyo na kuingia mtaani ila kiukweli mimi kama mdau ninayo ina rhumba za ukweli ambazo huwezi kuchoka kuzisikiliza hata kidogo.
DOGO RAMA JEMBE a.k.a VUALAAAAA nyimbo nyingine zilizo katika album hiyo ni UZURI WANGU ambao amemshirika nguli mwingine kutoka twanga pepeta AMIGOLASI BABA NA SOPHII na nyingine ni SIRI YA MAPENZI ambayo amewashirikisha wakali wawili kutoka bnd tofauti ikiwa NI ROGERT HEGGA CARTAPILER WA EXTRA BONGO NA MWINGINE NI ERIC CANTONA MGOGO WA MAZIZINI KUTOKA DIAMOND MUSICA VIJANA CLASSIC
MARTIN KIBOSHO Kiumri ni kijana mdogo sana lakini ana jina kubwa na ana mambo makubwa sana katika muziki wa dansi tanzania baada yakusimama na band nyingi sana ncchini tanzania. Alizaliwa mnamo mwaka 1985 huko mkoani kilimanjaro akiwa ni mchanganyiko wa mchanga na mbena wa iringa Rasmi kwenye muziki aliingia mnamo mwaka 2001 akiwa kama mcheza sarakasi na mpiga ngoma katika kikundi cha MUUNGANO CULTURE TROUP ambapo hapo alikuwa na wakli wa sarakasi kipindi hicho wakina TUPATUPA,KILIAN,MOSHI MKALI,MUSA ambaye sasa anafanya shughuli zake za sanaa ndani ya jiji la LONDON-UINGEREZA na hapo muun gano ndipo alipopatamwalimu wa kupigangoma am drums kwa lugha iliyozoeleka kwa wana band wengi. katika kijipima kama amefuzu upigaji wa drums kuotka kwa mwalimu wake huyo martin alijiunga na band ya TANGO STARS akiwa na mkongwe mlemavu mwenye uwezo wa hali ya juu ANANIA NGOLIGA hiyo ikiwa ni mwaka 2004.
MKALI MARTINI KIBOSHO AKITAFAKARI JAMBO KITAA Mwaka 2005 aliweza kujiunga na band ilyokua chini ya aset chini ya mkugurugenzi iron lady ASHA BARAKA katikaband iliyokua inajulikana kama AFRICAN REVOLUTION WANA TAM TAM hapo ikiwa katika jina jipya baada ya lile la african revolution wanachumvi chumvi so marin kibosho alikua na kina BADI BAKULE,WAZIRI SONYO, ambapo aliweza kupiga katika nyimbo mbili tu kutokana na uchanga aliokua nao kipindi hicho!
MARTIN KIBOSHO MZIGONI AKING'UTA DRUMS KIHATARI HATARI
Mwaka 2006 aliweza kujiunga na band iliyotikisa sna kipindi hicho iliyokua chini ya kiongozi wake Kamarade ALLY CHOKI, kipindi hicho ikiitwa EXTRA BONGO 3*3 lakin baadae band hiyo ikafa lakini wakaunganisha band moja kwa mbili na martin aliendelea kuwa mpiga drums wao ni EXTRA BONGO NA DOUBLE M SOUND wakajiunga na baada ya hapo ikaitwa DOUBLE EXTRA viongozi ama wakurugenzi wa band hiyo wakiwa ni ALLY CHOKI NA MUUMIN MWINJUMA ambapo hapo waliweza kutoa album moja ambayo hata hivyo haikufanya vizuri sana sokoni
KAZI NA DAWA SI UNAJUA DRUMS KAZI YAKE HAPA ANATUPIA KITU CHA MSOSI Mwaka 2007 alijiunga na band ya MCHINGA GENERATION iliyokua chini ya mh MUDHIHIR MUDHIHIR hapo alipiga MWAKA WA TABU na NGUZO TANO na mwishoni mwa mwaka huo huo aliweza kwenda kujiunga na bandya twanga chipolopolo iliyokuna na le GENERAL BANZA STONE NA KINA MSAFIRI DIOF ambapo hapa aliweza kuandaa nyimbo moja iliyoitwa hujafa hujaumbika.
MARTIN KIBOSHO AKIZIKAANGA CHIPS LAZIMA UCHEZE Mwaka 2008 aliweza kupata deal ya kwenda kupiga nchini SAUDI ARABIA pale DUBAI ambapo hapo aliunda band yake aliyoiita THE ROUTE BAND akiwa na kina GOD KANUTI,HOSEA,SUPER K,SUZY CRAZY na wengineo na baada ya kuisha kwa mkata wake huko ndipo aliporudi tena bongo na kungana tena na wana EXTRA BONGO NEXT LEVEL WAZEE WA KIZIGO ambapo aliikuta album ya MJINI MIPANGO ikiwa jikoni ambapo alipata nafasi ya kupiga nyimbo ya FIRST LADY ambayo ilikua ni utunzi wake ALLY CHOKI kibabu cha loliondo Lakini MARTIN KIBOSHO amesharekodi nyimbo nne kati ya sita zitakazo patikana katika album mpya ya extra bongo ambayo bado haijapewa jina huku ikiwa inatamba na nyimbo mbili radioni MTENDA AKITENDEWA NA WATU NA FALSAFA ZA MAISHA MARTIN aaanasema mvuto wake wa kupiga drums ulikuwa kutoka kwa mwalimu wake wa kipindi hicho JIMMY KIBELO,NA PETIT MAKAMBO
MARTIN KIBOSHO a.k.a MUUZA SURA AKIFANYA VITU NA WAZEE WA KIZIGO FOR MORE ADVICE KWA MARTIN KIBOSHO NI kiboshodrama@yahoo.com
RAMA PENTAGONE alizaliwa mnamo mwaka 1979 ambapo alizaliwa na kusomea elimu yake hadi kidato cha nne katika jiji la mwanza Rasmi alianza kujiingiza katika tasnia ya muziki mnamo miaka ya 2000 akianzia katika band ya magereza MAGEREZA BAND kipindi hicho wanapiga bwaloni magereza mwaka 2004RAMA PENTAGONE alijiunga na band ya DOUBLE M a.k.a WANAMSHIKEMSHIKE kipindi hicho ikiongozwa na kocha wa dunia ambapo hapo aliweza kushirika katika album mbili zilizotolewa na band hiyo kipindi hicho ikiwa ni ile ya CALL BOX ambapo nadni ya album hiyo aliweza kushiriki nyimbo mbili tu lakini album iliyofata ya TITANIC aliweza kushiriki nyimbo zote za album hiyo
RAMA PENTAGONE MI NAPENDA KUMWITA SHAROBARO Mwaka 2005 DOUBLE M iliweza kujiunga na bad nyingine ya SERENGETI BAND ambapo hapo ikaitwa SERENGETI MSHIKEMSHIKE wakati huo akiwa nawatu kama AMOROSO ambaye kwa sasa ni producer,RASHID SUMUNI,AMINA NGALUMA,KASSIM RASHID,KAWANINGA,JUMA KATUNDU na wengineo! mwaka 2007 aliweza kurudi home city Mwanza na akajiunga na ban ya CARNIVAL ya jijini mwanza ikijulikana kama TAIFA STARS wakati huo akiwa na kina ALLY YAHYA,PETIT MAKAMBO,ROGAROGA,SEBA huku ikiongozwa na mkongwe BENO VILLA ANTONY
RAMA PENTAGONE AKIONYESHA MAVOCAL Mwaka 2008 aliweza kujiunga na band ya MILE LEVENT MUSICA ambapo hapo aliweza kushiriki kutoa album ya MAMA KABIBI hukuakindika nyimbo kama MCHAKATO,LIFE JACKET na wakati huo akiwa nakina RICH MAARIFA,BOB KISSA,ATANAS NA SUZUKI Mwaka 2009 alijiunga rasmi na EXTRA BONGO NEXT LEVEL WAZEE WA KIZIGO ambapo aliwezac kusimama vyema kwenye album ya kwanza ya MJINI MIPANGO aidha rama pentagone anatarajia kutoa album nyingine akiwa na wa extra bongo huku akitarajikuweka nyimbo yake ya jeolus
RAMA PENTAGONE AKIWA NA WANA EXTRA BONGO RAMA PENTAGONE kuandaa album yake binafsi ikiwa na nyimbo kama NJIA PANDA,CHINI YA MTI,AZIZA,MKE WA MWENZIO USIMNONG'ONEZE SIKIO, aidha rama amesema mashabiki na wapenzi wa EXTRA BONGO wategemee makubwa kutoka kwake kwa kuwa anaamini ni mmoja kati ya wanamuziki wenye vipaji vya hali ya juu hapa Tanzania na mm nasaport hilo! kwa ushauri wowte juu ya dogo rama mtafute kupitia 0713-541508
SUPER NYAMWELA Alizaliwa mnamo mwaka 1977 katika mkoa wa Ruvuma wilaya ya Tunduru alisona na kumalizia elimu yake ya msingi akiwa huko Rasmi alijiingiza katika fani ya muziki mwanzoni mwa miaka ya 1990 akiwa kama mcheza show katika kumbi mbali mblai za burudani huko na hatimaye baadae kuhamia katika jiji la Dar-es-salaam huku akiendeleza kipaji alichokua nacho acha kucheza miziki tofauti tifauti kipindi hicho ikijulikana kama bingwa wa kucheza disco lakini ikiukweli ilikua ni breakdance Mwaka 1995 aliweza kuchukua ubingwa wa breakdance kwa mkoa wa Dar-es-salaam kipindi hicho akishindana na kina MAREHEM BLACK MOSES,KING JOBISO,na wengine wengi akini super nyamwela hakuishia hapo
SUPER NYAMWELA MWENYE NYEKUNDU AKIWA MZIGONI Mwaka 1996 aliibuka tena bingwa wa mikoa miwili ya dar na moro katika shindano lililopewa jina la nani zaidi ambapo hapao aliwaangusha wakali toka morogoro na dar vile na yeye kuiuka kidedea Mtaalam Super nyamwela haukishia hapo kuibuka kidedea mwaka 1997 aliibuka bingwa wa taifa wa mashindano ya breakdance hapo nikimaanisha bingwa wa Tanzania nzima katika mashindano ya kucheza kipindi hicho akiwabwaga wakali wa kipindi hicho kina marehemu BLACK MOSES,ATHMAN DIGADIGA,KING JOBISO,marehem MAX PRINCE lakin mwishoni mwa mwaka 1997 aliweza kuibuka kudedea na kuwa bingwa wa AFRICA MASHARIKI akiwabwaga wakali toka nchi za KENYA,UGANDA, Mwaka 1998 aliweza kupata shavu la kuzunguka na mwanamuziki nguli AWAILO LONGOMBA katika baadhi ya mikoa Tanzania na alifanikiwa kurekodi video na AWILO katika nyimbo ya GET LA COUN Mwaka huo huo wa 1998 aliweza kupata shavu lingine la kuzungukana aliekua nguli wa muziki wa rhumba kutoka kundi la TP OK JAZZ iliyokua ikiongozwa na gwiji la muzki FRANCO LUAMBO MIKIADI nae si mwingine ni MADILU SYSTEM ambaye aliweza kupiga nae tour katika nchi za KENYA,UGANDA NA TANZANIA na baada ya kumaliza tour hiyo alirejea tena bongo na kuunda kundi lililotikisa la break dance lililotikisa mwishoni mwa miaka ya tisini la BILL BAMS lililokua lilikua na mskani yake pale CLUB BILCANAS
SUPER NYAMWELA Mwaka 2000 aliweza kujiunga rasmi ma kundi la AFRICA STARS kipindi hicho na kwa sasa wanajulikakana kama TWANGA PEPETA SUGU KISIMA CHA BURUDANI mwaka huo akijiunga na madancer kina super danger,danger boy,dogodogo rashidi,bokilo,edy boy,aisha madinda,lilian internet,khadija.pendo bonzo,mwantumu hapo super nyamwela aliweza kusimamia show za albu zote kumi za twanga kuanzia KISA CHA MPEMBA,JIRANI,CHUKI BINAFSI,UKUBWA JIWE,MTU PESA,SAFARI 2005 Na nyingine zilizofatia
SUPER NYWAMWELA WA PILI TOKA KULIA AKIWA NA WANA WA TWANGA PEPETA
SUPER NYAMWELA WA MBELE AKIWA NA WANA EXTRA BONGO Lakini mwaka 2006 alijiingiza katika tasnia yakuimba huku akiendelea kucheza lakini na uimbaji wake ukaangukia katika nyimbo za kiafrica zaidi na ndipo alipofanikiwa kutoka album yake ya kwanza ya MASTER ON THE TEMPLE ambapo aliwashirikisha watu kama BADI BAKULE,LUZA MBUTU,MSAFIR DIOF,PAPII KOCHA,NA RASHID MWENZINGO baada ya miaka minne tena yaani mwaka 2010 alifanikiwa kutoa album yake nyingine aliyoiita AFRICA KILOMONDO na ndio nyimbo inayotikisa kwa sasa katika muziki wa kiafirica ikiwa na nyimbo za WATOTO YATIMA.UTAMADUNI WETU,BABA NA MAMA,MSUMARI WA MOTO,AFRICA KILOMONDO,MAMA MWENYE NYUMBA,LISA,AMANI AFRICA huku ndani akiwa amwewashirikisha wanamuziki tofauti akiwemo Ally Choki,Richard Maarifa,juma nature,bob rudala,modester nyoni,
SUPER NYAMWELA AKIWA MZIGONI KWA KUGHANI AKIWA EXTRA BONGO
SUPER NYAMWELA MIUKA IMEMPANDA KAZINI. HUYO NI MKONGWE ANAETIKISA KWENYE KATIKA ANGA LA MUZIKI WA KIAFRICA.........................................................................................................................
HUKU NDIKO ALIKOTEKA ROGERT HEGGA (CATAPILA) ROGERT HEGGA alizaliwa katika miaka ya 1973 jijini Dar-es-salaam na kusoma shule ya msingi na kumaliza na hatimaye alijunga na chuo cha ufundi Dar-salaam DAR TECH Rasmi rogert alijiinga katika muziki mnamo mwaka 1987 kwa kuimba kwaya kanisani, baada ya hapo mwaka huo huo wa 1987 alijunga na band iliyoitwa SAFARI BAND mwenyewe akiita band ya mtaani wakati huo katika band alikuwa na mchekeshaji maarufu katika tasnia ya uigizaji KINGWENDU NGWENDULILE ambapo alidumu na band hiyo ya safari mpaka mwaka 1989 ambapo alijunga na band nyingine iliyokua inajulikana kama CITY SOUND ambapo alikutana na mkonge wa muziki wa kiafrica toka south Africa TABOO nadhani wafatiliaji wa muziki wa dansi watakua wanamkumbuka taboo Baaday ahapo mwaka 1992 alijiunga na band ya kipindi hicho iliyoanzishwa mwishoni mwa miaka ya tisini na kina kamarade ALLY CHOKI band ya BANTU GROUP lakini wakati ROGGERT anajiunga na band hiyo tayari inaesemekana ni muasisi wa band ya bantu group KOMANDOO HAMZA KALALA ndio alikua amejiunga na band hiyo ambayo roggert alidumu nayo mpka mwaka 1995 lakini maka wa 1995 ROGGERT alifanikiwa kutoa album yake mwenye kama kazi binafisi(SOLO ARTIST) huku akiwa na kundi lake dogo la AFRI GENERATION wakati huo akiwa ametokea nchini ZIMBABWE ambako alikwenda kufanya kazi hiyo hiyo ya muziki wa dansi album hiyo ambayo aliipa jina la MAMA RADHIA ambacho ni moja ya kibao ambacho kilimtambilisha vilivyo rogert hegga nyimbo nyingine zilizopatikana katika album hiyo ni ASMA,SINTO KATA TAMAA,THEO MAZIMBABWE, Mwaka 1997 roggert alijiunga na band ya MASAI BAND ambayo ilikua na maskani yake pale kijitonyama jijini DAR-ES-SALAAM kipindi hicho akiwa na kina YAHAYA MKANGO,JOHN MPONI, ambapo hapo alidumu kwa muda wa mwaka mmoja tu na hatimaye Mwaka 1998 alijiunga na band ya TWIGA BAND ilyokua na maskani yake mwananyamala ambapo hapo alikutana na mtu mmoja maarufu sana CHE MUDUNGWAO, pamoja na JOHN MPONI ambapo hakudumu sana.
CARTAPILLER ROGGERT HEGGA
Mwaka 1999 alijiunga na band ya AFRICAN STAR kabla haijapewa jina la TWANGA PEPETA ambapo hapoa likutana wanamuziki mbali mbali akiwemo LE GENERAL BANZA STONE,LUIZA MBUTU kipindi hicho akiitwa LIUZA NYONI,AMIGOLASI,YAHYA MKANGO,JOSEPH KANUTI,DEO MWANAMBILIMBI,MICHAEL LILOKO,BOB GAD WILLIUM,JESCA CHALS,MAREHEM ABUU SEMHANDO kipindi hicho ilikua ni HOTEL BAND ambayo ilikua ikipiga pale BAHARI BEACH lakini walifanikiwa kutoa album moja ya KISA CHA MPEMBA ambapo ndani yake kulikuan nyimbo moja ambayo ni utunzi wake roggert FADHILA KWA WAZAZI NO. 01 hata hivyo hakumaliza mwaka na african star mwisho mwa Mwaka 1999 alitimkia nchini KENYA katika jiji la NAIROBI katika band moja iliyojulikana kama BENGA INTERNATIONAL ambapo hapo alikutana na wanamuziki nguli kwa sasa kama MUUMINI MWINJUMA,RASHID SUMUNI,hakudumu sana katika band hiyo na baadae kutimkia katika mji wa KISUMU ambapo hapoa pia likutana na mtu kama kamarade ALLY CHOKI ambae alikua kiongozi kwenye Band iliyoitwa EXTRA KIMWA ambapo hapo vile vile kulikupwepo na mpiga gita maarufu tanzania kwa sasa EPHRAIM JOSHUA NA MTOTO WA KING MAJUTO ATHMAN MAJUTO, ambapo hapo alikaa kwa muda kidog na baandae kurejea tena tanzania, mwanzoni mwa mwaka 2000 alitua tena AFRICA STAR ambapo aliikuta album ya pili ya twanga pepeta JIRANI ikiwa jikoni na yeye kuweza kupata kushiriki katika kuimba katika nyimbo zilizokuwemo katika album hiyo ambayo ilatakiwa kuitwa AUNGURUMAPO SIMBA lakini kabla haijamalizika kiongozi wa wakati huo banza stone aliondoka na ndipo ali choki alipewa jukumu la kuandika nyimbo itakayobeba jina la album Safari ya roggert haikuishia hapo mwaka huo huo wa 20000 mwishoni alijitoa yeye na wenzake na kwenda kuanzisha band ya MCHINGA SOUND ambapo alikutana na wenzake kina ADOLPH MBINGA,MWIJUMA MUUMIN,JOSEPH WATUGURU,MOSHI MSELELA,GODFREY KANUTI,MICHAEL LILOKO,SELEMAN BONGO napo hakudumu sana katikati ya mwaka 2001 akajiunga tena african stars ambapo alidumu sasa kwa muda na kuweza kutoa nao album za 2001-fainali uzeeni 2002-chuki binafsi-ambapo alitunga nyimbo ya LA MGAMBO 2003-ukubwa jiwe-2004 mtu pesa ambapo ndani ya album hiyo alitunga nyimbo ya FAMILY COMFLICT
ROGERT HEGGA CARTAPILER a.k.a KILIMANJARO AKIWA NA TWANGA
Baada ya hapo mwaka 2004 roggert akatoka tena african stars na kujiunga tena na mchinga lakini safari hii ikiitwa MCHINGA GENERATION AU G8 ikiundwa na kina kamarade ALLY CHOKI,RASHID MWENZINGO,MUSEMBA MINYUNGU,OMARI SESEME,KALALA JOUNIOUR,SAULO FERGASON,ATHMAN MAJUTO,GOD KANUTI,BONZO KWEMBE,AMOUR ZUNGU, Ambapo hapoa aliweza kutoka album mbili akiwa na band hiyo ambazo ni 2005 NAFSI-2006 MWAKA WA TABU na aliweza kukaa mchinga generation mpka mwaka 2008 Alijiunga na T.O.T PLUS wana achimenengule ambayo ilikua chini ya kocha wa dunia MUUMUNI MWINJUMA ambapo hapo aliweza kuandika nyimbo ya CHEUPE SANDRA na baada ya hapo mwaka 2009 band ikabadilishwa jina na kuitwa T.O.T RESPECT hapo ilikua chini ya mzee wa kijiko kamarade ally choki.
LUIZA MBUTU NA ROGGERT WAKICHAPA KAZI
mwaka 2010 alirudi tena TWANGA PEPETA na sasa ivi inaitwa TWANGA PEPETA INTERNATIONAL ambapo hapo ailifanikiwa kutoa albm moja ambayo inaitwa MWANADAR-ES-SALAAM ambapo ndani kuna nyimbo ya RAFIKI ADUI ambayo ni utunzi wake mwenyewe roggert na mwaka 2011 alihamia band yenye wanamuziki nguli wa siku nyingi na inayofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa dansi ambayo ipo chini ya mkurugenzi mtendaji ally choki EXTRA BONGO NEXT LEVEL a.k.a WAZEE WA KIZIGO ambapo hapo ametunga nyibma ya UFISADI WA MAPENZI ambao utakuwepo kwenye album ambayo bado haijapewa jina na yeye yupo kama kiongozi wa band na hapo anaunga na wanamuziki LE GENERAL BANZA STONE,RAMA PENTAGONE,ATANASI,ALLY CHOKI MWENYEWE,SUPER NYAMWELA, AISHA MADINDA na wengine kibaoooooooooooooooo FUNDI ANAYETAMBA KATIKA TASNIA YA MUZIKI WA DANSI SASA
ROGGERT AKIWA NA WANA EXTRA BONGO
ROGGERT,BANZA NA ALLY.
ROGGERTHEGGA a.k.a CARTAPILAa.k.a KILIMANJARO TANZANIA.
LE GENERAL BANZA STONE a.k.a MWALIMU Alizaliwa mnamo mwaka 1972 Rasmia le general BANZA STONE alianza muziki yeye anauitwa wa ukweli mnamo mwanzoni mwa miaka ya 90 ambako alikuwa akisomea muziki katika chuo cha cha sanaa KOREA CULTURAL MUSIC CENTRE na wakati huo pia alikua akishughlika na uchezaji show nikiwa na maana dansi kama walivyokua wakina marehem BLACK MOSES,marehem MAX, na banza nae alikua napitia humo humo lakini mwaka 1992 aliingia rasmi katika fani ya uimbaji pale alipojiunga na ya THE HEART STRESS BAND ambayo ilikua ikijihusisha zaidi kupiga muziki kwenye mahotel toafauti tofauti yaan ni hotel band ambako alikaaa kwa muda wa miaka kadhaa ambapo baada ya hapo 1994 alijiuga na band nyingine ya hotel iliyokuwa ikiitwa AFRISUEZ lakini utofauti wa band hii walikua wakipiga nyimbo mchnanyiko yaani copy na nyingine walizotunga wao hapo ndipo BANZA STONE alipoandika nyimbo yake yakwanza ambayo ilikua kwenye staili ya dansi ambayo alikuja kuirudia baadae katika band ambayo nakutaka uendelee kunifatilia utaijua band gani, nyimbo alioitunga akiwa afrisuez iliitwa KUMEKUCHA lakini hata hivyo hakuwahi kurekodi nyimbo hiyo na kipindi hicho band hiyo ilikua ikipiga mahotelini kama kawaida alikaa afri suez kwa muda wakati huo alikua akiendelea na kazi yake ya ufundi selemara akiwa na mshkaji wake wa karibu lakini Mwaka 1998 le general Banza stone ambaye jina lake la kuzaliwa ni ramadhani masanja asili yake ikiwa ni msukuma wa shinyanga lakini aliekulia jijini DAR-ES-SALAAM alihamia band ambsayo ilikua ikipiga hotel vile vile kwa wakati huo AFRICAN STARS na kama watu walikua hawajui siri ya twanga pepeta basi le general ndio muasisi ya jina la TWANGA PEPETA kwani zamani ilijulikana kama african stars
ENZI HIZO LE GENERAL BANZA STONE MWALIMU WA WALIMU Mwaka 1999 banza aliweza kukirudia kibao chake alichokitunga afrosuez cha kumekucha na kuitoa bana hyo kutoka kwenye kupiga kwenye mahotel na kuanza kupiga katika kumbi mbalimbali akiwa na wanamuziki wenzake kibao wa wakati ndio walikuwa wakiunda african stars LUIZA MBUTU,JESCA CHARLES,AMIGOLASI,ALDOPH MBINGA,MAREHEMU ABUU SEMHANDO,MCD na ndipo walipofyatua album yao ya kwanza ikibeba jina la KISA CHA MPEMBA ukiwa ni utunzi wake LE GENERAL BANZA STONE Mwaka 2002 wakati wanajiandaa kutoa album yao ya pili ambayo tayari ilishapewa jina la AUNGURUMAPO SIMBA kibao ambacho kilitungwa na banza stone alichomoka kutoka african stars ambapo albm hiyo ilipewa jina jingine na banza akajiunga na band ya T.O.T PLUS(wanaachimenengule) ambapo alikutana na kina TOTO TUNDU,ABDUL MISAMBANO hapo aliweza kutoa album ya kwanza iliyotikisa na wimbo wa MTAJI WA MASIKINI na ndio uliobeba jina la album lakini ndani ya album hiyo kulikua na nyimbo kamatushirikiane na mwngine uliitwa jahazi zote zikiwa ni utunzi wake banza stone Mwaka 2004 banza tena akiwa na kina ley chinyama ambae alipiga gita la solo na bado akiwa na t.o.t plus aliibuka na ELIMU YA MJINGA ambayo nayo ilibeba jina album Mwaka 2005 banza tena akiwa bado na wana t.o.t aliweza tena kutoa remix vision ya AUNGURUMAPO SIMBA VOL 2 na ndio ikabeba jina la album tena humo kukiwa na nyimbo iliyotikisa kwa kipindi hicho KWA HERI wakati huo akiwa na WAZIRI SONYO,TOT TUNDU, NA ABDUL MISAMBANO.
LE GENERAL BANZA AKICHAPA KAZI NA MSAFIRI DIOF SOKOINE Na mnamo MWAKA 2004 aliibukia katika bend ya africa stars hapa jina la TWANGA PEPETA likiwa limesha komaa toka alipokua muasisi wakati linaanza na hapo aliibuka na kitu cha MTU PESA ambacho kilitikisa uliwngu wa dansi Tanzania na sio bongo tu hadi kiliweza kuchukua tuzo ya BBC AWARD kama nyimbo bora ya dansi na vile vile yeye mwenye kuibuka BEST MALE VOCALIST kwenye KILI AWARD za mwaka 2005 kutokana na kibao cha mtu pesa kufanya vizuri na album kupewa jina la MTU PESA lakin mwaka huo wa 2005 na tano akahamishiwa band Tanza ya african revolution ili kuongeza nguvu baada ya aliekua akiiongoza band hiyo muumini mwinjuma kujotoa na kuanzisha band yake wakati huo band ya african stars akirudishwa ALLY CHOKI kutoka mchinga sound Mwaka huo 2005 alifanikia kushiriki kwenye album ya safari 2005 ya twanga chipolopolo baada ya hapo akatengeneza band yake mwenyewe aliyoipa jina la BAMBINO SOUNG wakati huo akiwa na kina KALALA JUNOUR,ATNASI,BOB KISA, baada ya hapo mwaka 2006 mwishoni wakaunda band ya mafahari watatu ambao walikua ni yeye mwenyewe LE GENERALY BANZA STONE.ALLY CHOKI,NA MUUMINI MWINJUMA,
kutoka kushoto khadija mnoga kimobilte,ally choki banza stone,muumini mwinjuma enzi za mafahari.
lakini band hiyo haikudumu sana ndipo ally choki akatoka na kuanziah band yake na muumin kuunda band yake lakini na yeye kurudi bambino lakini mwaka 2007 mwishoni hadi 2009 akapata matatizo ya kiafya kwa takribani miaka miwili na hatimaye mwaka 2009 aliweza kurejea kidogo na kupata afueni na kuanza tena shughuliza muziki na kuibuka tena na band yake ya BAMBINO SOUND
LE GENERAL BANZA STONE a.k.a MAKAVELI
lakini hakuweza kukaa sana na band yake hiyo na mwaka 2010 alijuinga na band ya RUFITA CONNECTION ambapo alikuwa nao mpaka 20011 akajiunga na band mbayo inatikisa sasa EXTRA BONGO ambapo ameungana na mwanmuziki mweznie nguli ambaye pia ndie mkurugenzi wa band hiyo ally choki na mtuzni wa siku nyingi Roggert hegga cartapilla!
Le General banza stone wa kwanza kulia akiwa mzigoni na wana extra bongo.