Band inayokuja kwa kasi ya ajabu katika muziki wa dansi nchini tanzania MASHUJAA MUSIC BAND imeachia nyimbo NNE mfululizo huku nyingine mbili zikiwa bado zinatamba kwenye vituo kadhaa vya radio ambazo ni HUKUMU YA MNAFIKI na UNGENIELEZA ambayo ni utunzi wa chalz baba baada ya kutua katika kundi hilo na kuiachia kama zawadi kwa mashabiki wake NNE walizoziachia ni pamoja na UMENINYIMA ambayo wamamemshirikisha gwiji la muziki wa bolingo africa JULES SHUNGU WEMBADIO PENE KIKUMBA maarufu kama PAPA WEMBA, nyingine ni KWA WAKWE ambapo ndani wanamuziki waliohamia hivi karibu kutoka band kubwa nchini CHALZ BABA TOKA TWANGA PEPETA NA 33 TOKA FM ACADEMIA wamekamua vilivyo.
33 PAMOJA NA CHALZ BABA WAKALI WA MASHUJAA BAND Nyimbo nyingine ni UNGENIELEZA ambao ni utunzi wa chalz baba a.k.a kingunge a.k.a torres na ya mwisho iliyokua katika mtindo wa kiafrika zaidi unaitwa TIKISIKA ambapo pindipo utakapousikia lazima utacheza mwanzo mwisho lakini pia wimbo wa HUKUMU YA MNAFIKI umeingia katika tuzo za KILI MUSIC AWARDS Wimbo Bora wa Kiswahili (Bendi) :: Dunia Daraja-African Stars G1
Hukumu yamnafiki-Mashujaa Band G2
Falsafa ya Mapenzi- Extra Bongo G3
Usia wa Babu-Mapacha 3 G4
Mtenda-Extra Bongo G5 lakini ukitaka mashujaa hukumu ya mnafiki uweze kuibuka kidedea. HUKUMU YA MNAFIKI kwa SMS tuma KILI G2 kwenda 15747 au online ktk link http://www.kilitime.co.tz/awards/2009/nominees_2007.php
hapa nikiwa na jadoh pamoja na mastage show wa mashujaa
Rapa wa band inayotikisa katika ulimwengu wa muziki wa dansi nchini kutoka band ya AKUDO IMPACT aweka wazi kuzuia kazi aliyokwishaanza kuisambaza na kusema kulikuaa na wajanja wachace waliotakata kumzidi kete kwa kupiga kopi kifupi wanaitwa maharamia. Totoo ze bingwa amekwisha kamiliasha album yake yenye jumla ya nyimbo nane ambazo ameimba peke ake bila ya kumshirikisha msanii yeyete yule huku akiweka bayana kwa kufanya hivyo ni kudhihirisha uwezo na kipaji alichojaliwa na mungu.Nyimbo nane zilizopo kwenye album ya toto ze bingwa ni pamoja na SEBENE DOOZI ambapo humo amesema ameonyesha uwezo wa kuwa yeye ni mkali wa rap za kiswahili katika muziki wa dansi nchini tanzania na kusema kuwa rap nyingi wanazozitumia hata fm academia ni zile zile ambazo alitoka nazo yeye wakati akiwa katika band hiyo nyimbo nyingine ni SINA NENO JINGINE ambayo imepata tuzo ya mziki bora wa kiafrica katika tuzo zinazotolewa na BBC,vile vile kuna nyimbo kama HII MAMBO HAIELWEKI ambayo imebeba jina la album ya totoo ze bingwa yeye anajiita TSUNAMI WIMBO HUO ANASEMA UNAGUSA MAISHA YA WATU WANAOFANYA VITU HUKU WAO WAKIWA HAWANA HIVYO VITU AU KWA KIFUPI MTU KUFANYA KAZI LAKINI ANAEFAIDIKA MWINGINE
TOTOO ZE BINGWA MZEE WA RAPING 7777 KATIKA SIKU 7 Wimbo mwingine unaopatikana katika album ya mambo haielweki ni SIKU HIYO ambapo humo ndani amezungumzia siku ambayo anahisi atakua na furaha pindi atakapoa pata anachokihittaji ikwemo akimuona rafiki yake wa karibu PAPII KOCHA akitoka jela ni wimbo wenye mahadhi tofauti ya kiafria. wimbo mwingine uliomo katika album hiyo ni DISPILINE ambao amepiga katka mahadhi flani ya kiafrica magharabi huku akitoa ujumbe wa kuwa yeye ni mklai zaidi ya vile ya watu wanavyofikiri na kipaji anaamni kapewa na mungu kwa ajili ya kuwapa burudani huku akitoa onyo kwa ma rapa wanaomuiga rap zake huku wakishindwa kumshukuru kwa ubunifu wake. kuna wimbo mwingine uliomo ndani ya album hiyo ambao ukiona kwa maandishi ya kuandikwa ni AMEKUBALIKA lakini kwa mujibu wa yeye na vile animba ndani amegeuza maneno hayo na kuuita AKILABUKEMA ambao amesema amefanya hivyo ili kuup[a mahadhi ya kiafrica zaidi!
TOTOO ZE BINGWA AKIWA NA WAREMBO WA BAND YAO AKUDO Wimbo mwengine ulio kwenye album hiyo ni JAMAN ambao amelalamikia watoaji tozo za kili music award kuwa wamejawa na uzawa lakini hawaangali kipaji wala uzoefu na hivyo kusema tuzo hizo huwa zinamvunja moyo kutokana na kujaa ukiritimba na uototo wa nyumbani mwingi wakati hata yeye alipo anawakilihsa TANZANIA na wimbo wa mwisho kwenye album hiyo ameuita world cup ambao aliiutunga kama kumbukumbu ya kombe la dunia kuchezewa africa lakini totoo ameongeza katika kukabiliana na maharamamia na wanyonyaji ambao ni madistrbuter amesema mpnago wake ni kuiza album kwa mtu mmooja au kampuni ili ashughulike nayo na mpka sasa kuna wazungu kutoka marekani tayari wameshakubali kuinunua album ya TOTOO ZE BINGWA na mpka naongea nae alikua na wazungu hao so TOTOO ZE BINGWA AMESEMA SAPOTI KUBWA SANA ITATOKA KWA WATANZNIA WENYEWE KUPENDWA VYA KWAO.
HUYO NDIO TOTOO ZE BINGWA AMBAE AMESMEA KILICHOMTOA FM ACADEMIA NI UBINAFSI NA KUSEMA HAWEZI KAZI WAKATI RAPIN ZAKE NDIZO WANAZOZITUMIA MPAKA LEO AKIITOLEA MFANO RAPING ALIOITOA RAPA TOTOO KALALA KWENYE WIMBO WA HEINKEIN NA VILE VILE HATA JINA LA TOTOO KALALA KAPEWA ILI WATU JUE KUWA ZE BINGWA BADO YUPO NAO HAYO NI KWA MUJIBU WA TOTOO ZE BINGWA MWENYEWE.