WAY

Friday, February 24, 2012

MASHUJAA MUSICA WAACHIA NNE KWA MPIGO MOJA WAKIWA NA GWIJI LA MUZIKI AFRICA PAPA WEMBA

Band inayokuja kwa kasi ya ajabu katika muziki wa dansi nchini tanzania MASHUJAA MUSIC BAND imeachia nyimbo NNE mfululizo huku nyingine mbili zikiwa bado zinatamba kwenye vituo kadhaa vya radio ambazo ni HUKUMU YA MNAFIKI na UNGENIELEZA ambayo ni utunzi wa chalz baba baada ya kutua katika kundi hilo na kuiachia kama zawadi kwa mashabiki wake
NNE walizoziachia ni pamoja na UMENINYIMA ambayo wamamemshirikisha gwiji la muziki wa bolingo africa JULES SHUNGU WEMBADIO PENE KIKUMBA maarufu kama PAPA WEMBA, nyingine ni KWA WAKWE ambapo ndani wanamuziki waliohamia hivi karibu kutoka band kubwa nchini CHALZ BABA TOKA TWANGA PEPETA NA 33 TOKA FM ACADEMIA wamekamua vilivyo.
                      33 PAMOJA NA CHALZ BABA WAKALI WA MASHUJAA BAND
Nyimbo nyingine ni UNGENIELEZA ambao ni utunzi wa chalz baba a.k.a kingunge a.k.a torres na ya mwisho iliyokua katika mtindo wa kiafrika zaidi unaitwa TIKISIKA ambapo pindipo utakapousikia lazima utacheza mwanzo mwisho lakini pia wimbo wa HUKUMU YA MNAFIKI umeingia katika tuzo za KILI MUSIC AWARDS Wimbo Bora wa Kiswahili (Bendi) ::
Dunia Daraja-African Stars G1
Hukumu yamnafiki-Mashujaa Band G2
Falsafa ya Mapenzi- Extra Bongo G3
Usia wa Babu-Mapacha 3 G4
Mtenda-Extra Bongo G5

 lakini ukitaka mashujaa hukumu ya mnafiki uweze kuibuka kidedea.  HUKUMU YA MNAFIKI kwa SMS tuma KILI G2 kwenda 15747 au online ktk link http://www.kilitime.co.tz/awards/2009/nominees_2007.php
Goza Msale Chuma
 
      hapa nikiwa na jadoh pamoja na mastage show wa mashujaa
      MASHUJAA MZIGONI
 

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...