WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Thursday, November 20, 2014

HABARI ZA MTO ZA LEO ASUBUHI ZISOME HAPA


 SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU MALALAMIKO CHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
Serikali imetoa tamko kuhusiana na malalamiko ya Vyama vya siasa kuhusu kuingilia mamlaka ya vyama ya kuwapangia watu wa kuwadhamini Wananachama wao pamoja na Mihuri ambayo inatakiwa kutumika kutokana na Watendaji wa Vijiji kuwazuia wanachama hao kujiandikisha.

Akitoka Kauli ya Serikali jana Bungeni Mjini Dodoma Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema Ofisi yake itatoa maelekezo kwa watendaji hao ili wananchama hao waweze kudhamini kutoka mashina au vitongoji vyao tofauti na ilivyokua awali.

Mh. Pinda ameongeza kuwa hatua ya Kufanya hivyo ni kutokana na migogoro iliyopo sasa ambayo inaonekana itaweza kuwanyima fursa wanachama wengine kushiriki katika chaguzi hizo na kusema hilo ni tatizo ambalo linarekebisha na wamefanya hivyo kwa maslahi ya Vyama vyote.

...................................
 WILAYA YA ROMBO YAONGOZA KWA UKATILI WA KIJINSIA
Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania inaogoza kwa ukatilia wa kijinsia na watoto huku ikibainika kuwa watoto ndio wamekuwa wahanga wa kubwa katika jamii.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa Kilimanjaro Bi. Grace Limo wakati wa Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.

Bi. Grace amesema watoto wengi katika wilaya hiyo wanathirika kwa kutumikishwa katika shughuli za kibiashara na kwa kuachishwa shule huku wengine wakilelea na wazazi ambao wamejikita kwenye ulevi wa Kupindukia.

...................................
UKOSEFU ELIMU YA UZAZI SABABU YA MIMBA ZA UTOTONI SHINYANGA
Ukosefu wa  elimu ya uzazi na elimu ya uzazi wa mpango bado  ni changamoto  kubwa kwa wananchi wa halmashauri  ya  wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga,hali ambayo imekuwa ikisababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni kwa kiasi kikubwa na hivyo kuhatarisha  maisha ya mama na mtoto.

Mratibu  msaidizi  wa huduma za afya  ya  uzazi na mtoto wa wilaya ya kishapu  Bi. Suzana Kulindwa ameyabainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema idadi  kubwa ya wasichana ambao wanabeba mimba kuanzia miaka 14 hadi 19.

Amesema kuwa kwa mwaka 2013 wanawake 13,373 walihudhuria kliniki na kati  yao 2,562  walikuwa na umri wa chini ya miaka 20 ikiwa ni sawa na asilimia 19.1 na kuwa  katika kipindi  cha  Januari na Juni mwaka huu wanawake 1,370  wenye umri wa chini ya miaka 20 walihudhuria Kliniki sawa na asilimia19.9 wakiwa wajawazito.

Amebainisha kuwa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka 2014, kati ya wanawake 6,871 waliohudhulia 1,370 , wamebainika ni vijana waliokuwa na umri wa chini ya miaka 20, hali aliyodai imekuwa ikisababisha kuwepo kwa ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na uzazi.
.....................................
MTU MMOJA AUWAWA NCHINI KENYA KATIKA MAPIGANO
Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya.

Polisi walipambana na vijana walioingia katika Msikiti wa Swafaa eneo la Kisauni na mpaka sasa zaidi ya vijana 400 wanashikiliwa tangu kuanza kwa msako huo, mapema wiki hii.

Msako huo katika msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni unakuja baada ya msako mwingine wa Jumatatu ambapo polisi pia walipata silaha ndani ya msikiti ambao wanasema hutumika kutoa mafunzo yenye itikadi kali.
................... .................
WANANCHI NCHINI MEXICO WAKUSANYIKA KUFANYA MAANDAMANO
Wananchi wa Mexico wamekuwa wakikusanyika kabla ya maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mexico City na miji mingine ili kupinga utekaji nyara wa wanafunzi arobaini na watatu.

Mikusanyiko mitatu ya maandamano itaungana katika lango la bustani kuu mjini Mexico City.

Shughuli za biashara na maduka katika eneo hilo yamefungwa kama njia ya kuchukua tahadhari huku Rais wa Mexico akisema nchi imeumizwa, lakini amani na haki ni mambo yanayotakiwa kusonga mbele
....................................
IRAQ YASEMA IMEKUBALIANA NA UTURUKI KATIKA VITA NA IS
Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, amesema nchi yake na nchi jirani ya Uturuki, zimekubaliana kushirikiana kwa karibu kwenye masuala ya usalama na intelijensia, katika kukabiliana na kitisho cha kundi lijiitalo Dola la Kiislamu.

Haider ametoa kauli hiyo leo kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad, baada ya mazungumzo na mwenzake wa Uturuki, Ahmet Davutoglu, aliye ziarani huko. 

Uhusiano kati ya pande hizo mbili ulikuwa mbaya kwa siku za hivi karibuni, kwa kile Iraq inachochukulia kuwa ni mauzo haramu ya mafuta yanayofanywa na jimbo la Kurdistan kupitia Uturuki.
................................
 TALGWU YAITAKA SERIKALI KULIPA MADENI YAKE
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) nchini, kimeitaka
serikali kuhakikisha inalipa madai ya wanachama wake yanayofikia kiasi
cha  shilingi bilioni 18 ,yanayotokana na malimbikizo ya mishahara
,uhamisho na masomo.

Akizungumza jana katika mkutano uliowakutanisha  viongozi mbalimbali  wa
TALGWU, Jijini Arusha, Mwenyekiti wa chama hicho,Seleiman Kikingo ametoa
tamko hilo, huku akisisitiza kuwa madai hayo yamedumu kwa zaidi ya
miaka mitano na serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu ikiwa kimya.

Amesema pamoja na serikali kulipa kiasi cha shilingi bilioni 5,ikiwa
ni sehemu ya deni hilo jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha kuwa
madai yao yanakamilika kabla ya uchaguzi mkuu mwakani kufika,hatua
ambayo itawawezesha kujikimu na ukata unaowakabili.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo, amesisitiza kwa kuzitaka
halimashauri za miji na majiji hapa nchini kuunda mabaraza ya
wafanyakazi kwani katika halmashauri  167 za hapa nchini mabaraza
yaliyoundwa yapo 154 na kati ya hayo mabaraza 77 ndiyo yapo hai ,huku
mabaraza 73 hayapo hai.

MIGOGORO MINGI YA ARDHI NI UKOSEFU WA ELIMU YA ARDHI
Imebainika kuwa uwepo wa migogoro hiyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini licha ya kuchangiwa na utendaji mbovu wa viongozi wa serikali bado ukosefu wa elimu kwa wakulima umekuwa ni sababu ya wakulina na wafugaji  kushindwa kujua haki zao na hivyo kujikuta wakiingia katika migogoro ambayo ingeweza kumalizwa kwa misingi ya sheria.

Hayo yamebainika katika warsha ya wakulima na wafugaji wa mkoani Arusha chini ya Umoja wao wa MVIWATA na mtaalamu wa sheria wa  umoja huo Joseph Chiombola  na kuwataka viongozi mbalimbali wa siasa kutumia majukwaa yao katika kuwaelimisha wananchi ili kuepukana na migogoro iliyopo hivi sasa katika baadai ya maeneo.

Akifungua warsha hiyo  Mkuu wa wilaya ya Monduli Joika  Kasunga amesema migogoro ya ardhi ya mara kwa mara baina ya makundi ya wafugaji na wakulima yameifanya sekta hiyo kushindwa kuonyesha matokeo chanya,na hivyo kuwafanya kushindwa kufikia viwango vya kitaalamu katika uzalishaji wa mazao ya kilimo hali ambayo inatajwa kuwa kama itaendelea upo uwezekano wa usalama wa chakula nchini kuwa hatarini..

…............................................
 WANASHERIA AFRIKA MASHARIKI WAAZIMIA KUFANYA KAZI BILA MIPAKA
Wanasheria wa nchi wanachama wa Afrika Mashariki EAC, wamepitisha Azimio la kufanya kazi bila mipaka ndani ya eneo hilo lengo likiwa ni kupanua wigo wa kiutendaji kwa wataalalmu wa sheria walio katika eneo hilo.

Akizungumzia hatua hiyo, Rais wa Chama cha Wanasheria Afrika mashariki EALS, aliemaliza Muda wake, James Mwamu, amesema azimio hilo litapitishwa na wanachama kabla ya kupelekwa mbele.

Kwa mujibu wa Mwamu, pendekezo la kuanzisha jambo hilo lilitoka kwa vyama vya wanasheria wanachama wa EALS kutoka Tanzania, Rwanda, Burundi, Zanzibar, Kenya, na Uganda.
…............................................
MEYA WA ASHKELON APINGA KUAJIRIWA WAARABU KATIKA MJI WAKE
Meya wa mji wa Ashkelon nchini Israel, Itamar Shimoni, amepiga marufuku kuajiriwa kwa Waarabu kwenye mji wake kwa kile anachokiita "sababu za kiusalama".

Akitangaza kupitia mtandao wake wa kijamii jana, meya huyo amesema wafanyakazi wa ujenzi ambao ni Waarabu wanaojenga mahandaki ya kujikinga na mabomu katika skuli za chekechea wanazuiwa mara moja hadi tangazo jengine litakapotolewa.

Wafanyakazi wengi wa ujenzi nchini Israel ni wa jamii ya Kiarabu, ambayo ni asilimia 20 ya raia wote wa nchi hiyo.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu pamoja na maafisa wa ngazi za juu wa serikali yake wameikosoa amri hiyo.

SOMA HABARI HIZO KATIKA BLOG HII

 WANAWAKE WAMELETA MABADILIKO NCHINI- MAKINDA

Spika wa bunge kutoka Tanzania Anne Makinda amesema wabunge wanawake nchini  wamefanya kazi kubwa katika kuleta mabadiliko juu ya mtizamo wa watu kuhusu wanawake kwenye jamii.

Spika Makinda ambaye kwa sasa ni rais wa bunge la nchi za kusini mwa Afrika SADC amefafanua wajibu wa bunge hilo  Kwa kueleza kile kilichojadiliwa na kikao hicho cha maandalizi cha mkutano wa maspika kwa mwaka 2015.

Mh. Makinda amesema moja ya Agenda ambazo zitajaliwa katika vikao vya bunge hilo ni pamoja na kuona ni jinsi gani nchi zimefikia malengo ya milenia lakini pia na kuangazia masula ya Jinsia katika nchini Wanachama.
MWISHO


WAFUGAJI WATAKIWA KUISOMA KATIBA INAYOPENDEKEZWA
...................................
Wakulima  na  wafugaji   nchini  Tanzania  wameshauriwa   kuisoma  na  kuielewa   katiba  iliyopendekezwa   ili  ukifika  wakati   wa  kupiga  kura  wachukue  maamuzi   sahihi   badala  ya  kusubiri  kusomewa  na  wanasiasa majukwaani kwani asilimia  kubwa  wanasukumwa  na  maslahi   yao.

Akizungumza  na  wanachama  wa mtandao   wa  vikundi  vya   wakulima  Tanzania (MVIWATA)  Mkoa  wa  Arusha  Mkuu   wa  Wilaya  ya  Monduli  Bw,  Jowika  Kasunga  amesema  changamoto  nyingi  zinazoyakabili  makundi   hayo  ni  matokeo   ya kukosekana  kwa  uelewa  wa  kutosha  wakati   wa  kufanya  maamuzi   yanayowahusu.

Aidha  Bw.  Kasunga   amewataka   wadau  wanaosaidia  makundi  hayo   ukiwemo  mtandao  wa  (mviwata ) kuongeza  jitihada  za  kuwaunganisha  na  kuwaeleza  ukweli  juu  ya  masuala  yanayowahusu   hatua  itakayosaidia  kuziba  mianya  ya  watu wachache  wanaotaka  kuwatumia  kwa  maslahi  yao 

...................................
WATOTO 130,00 WANA VIRUSI VYA UKIMWI NA VVU NCHINI TANZANIA
Takwimu  zinaonesha kwamba watoto 1,30,000 wana maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) Huku kati ya hao 39317 wamefikiwa na kupatiwa huduma ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo.

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la  VVU na UKIMWI kwa watoto linalofanyika  katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar-es-salaam.

Dkt . Chana alisema asilimia 39 ya watoto walio katika hatari ya kupata maambukii ya  UKIMWI hupimwa vipimo vya kubaini maambukizi ya VVU ndani ya miezi miwili baada ya kuzaliwa hivyo basi kuna  umuhimu kwa watoto hawa kupata huduma za tiba mapema.

Akizungumzia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waziri huyo alisema Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lengo likiwa  ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya kwa watoto wachanga.
.....................................
MIRADI YA MENDELEO NCHINI KENYA NI NJIA YA KUKOMESHA UGAIDI
Naibu Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi  Koki Muli Grignon amesema uanzishwaji wa miradi yenye lengo la kutokomeza umaskini ni mojawapo ya hatua za serikali za kukabiliana na vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali.

Akihutubia Baraza hilo wakati wa mjadala wa ngazi ya juu wa wazi kuhusu ugaidi, wapiganaji mamluki Balozi Muli amesema miradi hiyo inatekelezwa kupitia mamlaka za majimbo nchini Kenya kupitia mfumo wa ugatuaji madaraka.

Amesema ugatuaji wa matumizi ya fedha na uchukuaji wa maamuzi kwenye maeneo  husika ni msingi wa kutokomeza umaskini na tayari hatua hiyo ya  ugatuaji imejumuishwa kwenye katiba ya Kenya.

ZAIDI YA SERIKALI  100 ZIMEAHIDI KUZUIA UTAPIAMLO DUNIANI
…................................
Zaidi  ya  serikali 170 zimeahidi kuchukua  hatua zaidi  kuzuwia utapia  mlo  duniani, zikiidhinisha  kwa  hiyari  yao  misingi  ya kuhimiza  vyakula  vyenye  afya  na  kupunguza  viwango vya  unene kupita  kiasi  wakati wakianza  mkutano  wao  wa  siku  tatu ulioandaliwa  na  Umoja  wa  Mataifa.

Kwa  hivi  sasa , kiasi ya  watu  bilioni  mbili , ikiwa  ni  theluthi  ya watu wote  duniani, wanataabika  kwa  kukosa chakula  bora, ikiwa ni  pamoja  na  vitamini A, madini  ya  joto  na  zinki.

Ukosefu  huo  unasababisha  vifo  vya  asilimia  45  ya  watoto  wote waliofariki  mwaka  2013.

Wakati  huo  huo , kiasi  ya  watoto  milioni 42  chini  ya  miaka  5 wanauzito  wa  juu  na  kiasi  ya  watu wazima  milioni  500  ni  wanene  kupita  kiasi  katika  mwaka  2010 kwa  mujibu  wa  tarakimu  za  Umoja  wa  Mataifa.
....................................
WATU 10 WA FAMILIA MOJA WAMEUAWA NCHINI MISRI
Watu  kumi  wa  familia  moja  wameuwawa  usiku wakati  jeshi  la anga  la  Misri  liliposhambulia  nyumba  moja  katika  rasi  ya  Sinai kwa  makosa.

Watu  hao  kumi, ikiwa  ni  pamoja  na  wanawake watatu  na  watoto  watatu, wamefariki  walipofikishwa  katika hospitali  ya  al-Arish   katika  mji  mkuu  wa  jimbo  hilo. 

Majeshi ya Misri yamekuwa katika mlolongo wa  kampeni  za kupambana na makundi ya wapiganaji wa Jihadi tangu Agosti 2011katika eneo la jangwani linalopakana na Israe na  eneo la Palestina la Ukanda wa Gaza.
.............................
CCM WAITAKA SERIKALI KUWAWAJIBISHA WALIOSHINDWA KUVIENDELEZA VIWANDA
Chama  Cha Mapinduzi kimeitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya waliobinafshiwa viwanda nchini sanjali na kunyang'anywa viwanda hivyo na kurudishwa kuwa mali ya umma.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa, Bw. Abrahmani Kinana,inakuja mara baada ya kutembelea na kujionea,mlundikano wa korosho na msururu wa magari ya kisubili kupakuliwa,huku moja ya kiwanda cha kubangua korosho na ufuta kikigeuzwa ghala la kuifadhia vifaa vya kusambazaia umeme.

Bw. Kinana akihutubia kwenye mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Nachingwea Mkoani Lindi,ameitaka serikali kuwawajibisha viongozi au watumishi wa umma,ambapo amesema serikali haipaswi kuogopa watu wachache hasa wenye fedha na kuwacha mamilioni ya  watanzania waliowaweka madarakani wakitaabika.
TCCIA KIMEWATAKA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI
.............................................
Chama cha wafanyabiashara wa viwandani na kilimo (TCCIA) kimetoa wito kwa wafanyabiashara kote nchini kuitumia vizuri wiki ya mlipa kodi inayoendelea nchini ili waweze kupata elimu ya kutosha kuhusiana na faida za kulipia kodi biashara zao kwa mustakabali wa Taifa.

Wito huo umetolewa leo na mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Dodoma, Fautine Mwakalinga wakati akizungumza na East Afrika Radio kuhusiana na faida za wiki ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara nchini.

Mwakalinga amesema kuwa elimu inayotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuhusiana na umuhimu wa kulipa kodi  ina faida kubwa kwa wafanyabiashara hata kwa wale ambao wanakwepa kulipa kodo kwani wakipata elimu ya kutosha wanaweza kuanza kulipa kodi kwa ajili kukuza uchumi wa Taifa.

Pia ametoa wito kwa jumuiya za wafanyabiashara kuhakikisha kuwa zinatatua matatizo yao na serikali kwa kukaa mezani na kuachana na migomo isiyokuwa na tija kwa taifa.

MUSWADA WA KUSANYAJI DATA ZA SIMU MAREKANI WAKATALIWA
Mswada  ambao  ungezuwia  ukusanyaji  wa  data  za  simu unaofanywa  na  shirika  la  usalama  wa  taifa  nchini  Marekani , NSA, umezuiwa  na  wabunge  mjini  Washington. 

Kura  hiyo  katika baraza  la  Seneti  ilikuwa  kura  58  za  ndio  na 42  za  hapana , ikiwa  ni  kura  mbili chini  ya  kura  60  zinazohitajiwa  kuupitisha mswada  huo.

Mswada  huo uliokataliwa  ungefikisha  mwisho  ukusanyaji  wa  data za  simu  za  mamilioni  ya  Wamarekani.   Wanaoupinga  wanasema ukusanyaji  wa  data  ni  muhimu  kwa  ajili  ya  juhudi  za  kupambana na  ugaidi.

Kiwango  cha  udukuzi  huo ulikuwa  miongoni  mwa  ufichuaji uliofanywa  na  mfanyakazi  wa  zamani  wa  shirika  la  NSA Edward Snowden.

Saturday, November 15, 2014

ZAMU ZAO ZIMEPITA SASA NI ZAMU YA TARSIS MASELA JOTO RAIS YA FASHION-ACHA HIZO NI USIKU WAKE TAR 21.11



              Tarsis Masela akizungumza na Waandishi wa Habari
Mwimbaji Nguli wa Akudo Impact Tarsis Masela Joto Rais wa Fasheni na Rais wa Band ya Akudo Impacht antarajia kuzndua Album yake Binafsi nje ya band yake ambayo amwashirkisha wanamuziki mbalimbali akiwemo Mzee Yusuph uzinduzi unaotarajiwa kuwashika watu kwa aina yake kwaku wa atasindikizwa na band tafauti wakwemo Akudo wenyewe, Mashujaa Musica Band, na Jahazi Morden Taarab chini Y Mfalme Mzee Yusuph ambae nae yumo ndani ya Albam hiyo.

Kwa Mujibu wa Tarsis amesema album yake hiyo imesheheni nyimbo Takribani nane ambazo ikiwemo Tabia mbaya, Penzi lako limezidi Asali Remix, Chaguo Langu, Mwiko, Acha hizo, na nyingine kibao ambapo amesema album hiyo itakuja kufanya mapinduzi halisi katika Tasnia ya Muziki wa Dansi.
                                    Tarsis Masela 'Joto'
Tarsis Masela Anakua Mwanamuziki wa Tatu kutoka ndani ya akudo Impact kutengenea album yake mwenyewe Wengine waliwahi kutamba na Akudo na Kufanya kazi zao binafsi ni pamoja na Totoo ze Bingwa na Cristian Bella sasa ni Zamu yake.

Tarsis ambae alitua nchini Akitokea Congo na baada kufanya kazi na Ndanda Cosovo na Stono Musica na baadae alijiunga na Akudo na mpaka leo anaendelea kufnya vizuri na kuongeza kwa baada ya Album yake hiyo kitafuata ni kuzindua album ya akudo ambayo ipo tayari kabisa.

Tuesday, November 4, 2014

TANZANIA YATUNGA KANUNI MPYA ZA UKAGUZI MAGARI KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI

           
 Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Mohamed Mpinga

Jeshi la Polisi nchini Tanzania Kikosi cha Usalama Barabarani,kimewasilisha kanuni nne mpya za ukaguzi wa Magari nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukabiliana na Ongezeko la ajali za barabani hususani kwa magari yanayosafirisha abiria nchini.

Wakati akifungua majadiliano ya namna kanuini hivyo zitakavyosaidia kukabiliana na ajali hizo,Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania,Kamanda Mohamed Mpinga amesema kanuni hizo zitasaidia kuyabaini magari ambayo yamechakaa kwa kutumia mfumo wa kisasa.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na Majini SUMATRA,Ahmad Kilima amesema kanuni hizo zitaponguza ajali zisizo za lazima zinazosababishwa na uchakavu wa magari.

VIJANA WATAKIWA KUACHA KUTUMIKA KISIASA NA BADALA WAWE CHACHU YA MAENDELEO

          
 Wawakilishi wa vijana kutoka Afrika mashariki pamoja na balozi wa vijana          katika jumuiya ya Madola

Vijana katika nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki wameanza kuonyesha hofu yao,juu ya namna wanavyotumiwa na baadhi ya wanasiasa, wenye maslahi binafsi katika kuleta machafuko, huku wakibainisha kutokuridhishwa na mwenendo wa ushirikishwaji, katika masuala ya maendeleo na uchumi.

Wawakilishi wa vijana kutoka Afrika mashariki pamoja na balozi wa vijana katika jumuiya ya Madola kwa pamoja wamekutaka katika Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa cha MS TCDC-USA RIVER Arusha katika ushirikishwaji mpana zaidi unaolenga kuwafanya vijana waweze kuwa sehemu ya kupanga na kufanya maamuzi katika kuitengeneza Jumuiya.
Akizungumza katika majadiliano hayo,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Nyirembe Munasa ameonya dhana ya kuwachukulia Vijana kama bomu linalosubiri kupasuaka na badala yake wafikiriwe kama rasilimali inayoweza kuijenga Afrika.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Vijana kutoka nchini Kenya Noli Kaaya amesema kuwa vijana wanaweza kuwa wawakilishi wazuri wa taifa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na uongozi katika kukuza uchumi.

KURA YA MAONI KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI APRIL 30, 2015- PRF. JK

                 
                                   Rais wa Tanzania Prof. Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania Prof. Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi Aprili 30 , 2015 kupiga kura ya maoni ya kapiga inayopendekezwa kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa na kwa vizazi vijavyo

Akiongea na wazee wa mkoa wa Dodoma hapo jana Prof Kikwete amesema Wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu upatikanaji wa katiba mpya huku akiwataka wananchi kupata nakala za katiba inayopendekezwa ili waweze kuisoma na kuielewa ili kuwa na maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura ya maoni.

Prof. Kikwete akizungumzia kuhusu uchaguzi wa serikali za mtaa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kuwataka kutumia fursa hiyo kujitokeza katika kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za serikali za mtaa.

Monday, November 3, 2014

WAKAZI WAKIMBIA MAKAZI YAO KISA MICHANGO YA MAABARA YA SHULE ZA KATA

                      Mfano wa Maabara zinazotakiwa kuwepo nchini nzima
Baadhi ya Wananchi Wilayani Karagwe Mkoani Kagera nchini Tanzania wameyakimbia makazi yao kwa ajili ya Kukwepa kuchangishwa Michango kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba vya maabara katika shule za Kata.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyakabanga Bw. John Bigimano na kusema kuwa Wanasiasa wanaohitaji kura ndio kimekua chanzo kikubwa cha wakazi hao kukimbia michango hiyo kwa kuwadanganya kuwa Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi huo.

Bw. Bigemano ameongeza kuwa hali hiyo inafanya mapaka sasa katika Shule 19 ni shule 5 tu katika kata yake ndio zimeanza ujenzi wa maabara hizo ambapo kwa mujibu wa agizo la rais hadi mwishoni mwa mwezi huu shule zote ziwe zimekamilisha ujenzi huo.


BAWACHA WALAANI VIKALI VURUGU KWENYE MJADALA WA JAJI WARIOBA



                          Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake CHADEMA, Halima Mdee
Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, nchini Tanzania limelaani vikali Vurugu alizofanyiwa aliekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba zilizotokea hivi karibuni.

Akizungumza katika Mkutano wa Hadhara katika Ziara ya Baraza hilo kanda ya Ziwa Mwenyekiti wa BAWACHA, Mh. Halima Mdee amesema kitendo alichofanyiwa Jaji Warioba ambae alishika Nyadhifa za Juu serikalini Hakikubaliki.

Mh. Mdee pia Vijana wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam waepuke kujiingiza katika vurugu kama hizo ambazo zinahatarisha amani ya nchini na kusema wao kama Chama watazunguka nchini nzima kuendelea kutoa Elimu kuhusu kupinga katiba inayopendekezwa na Kujiandikisha ili kupiga kura katika Chaguzi za Serikali za Mitaa.


SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA HOSPITAL YA RUFAA MKOANI MARA

          Ujenzi wa Hospital ya Rufaa Mkoani Mara
Tatizo kubwa la ukosefu wa huduma za afya za rufaa ambalo limekuwa likichangia vifo vingi kwa wananchi wa mkoa wa mara nchini Tanzania ,limeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya serikali kuanza ujenzi wa hospitali kubwa ya rufaa ya Mwalimu Nyerere Medical Center katika eneo la Kwangwa manispaa ya Musoma mkoani humo.

Akipokea madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya moyo,upasuaji na wanawake na watoto ambao wamepelekwa mkoani Mara kupitia mpango wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kusogeza huduma za madakari bingwa kwa wananchi wa mikoa wa pembezoni, Mgaga mkuu wa Hospatal ya Mkoa wa Mara Samson Winani amesema tayari Serikali imenza utekelezaji wa ujenzi wa hospitali hiyo.
kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw Michael Kishiwa,amesema mfuko huo umechukua uamuzi wa kupeleka madakatari bingwa katika mikoa ya pembezoni baada ya kubaini idadi kubwa ya wananchi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kukosa uwezo wa kifedha kwa ajili ya kutafuta huduma za matibabu za rufaa.
--

Saturday, November 1, 2014

Serikali imetenga zaidi ya shilingi Bilion moja kwa ajili ya kununua vifaa vya Maabara zote zinazojengwa nchini

                             Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa
Serikali imetenga zaidi ya shilingi Bilion moja kwa ajili ya kununua vifaa vya Maabara zote zinazojengwa nchini kwa lengo la kuboresha kiwango cha elimu na hasa katika shule za sekondari za kata ambazo zilikuwa hazina maabara.

Akiongea na wanachi mjini Bukoba Naibu wa Waziri wa Elimu Tamisemi Kasim majaliwa ambae alikuwa mgeni rasimi katika harambee ya kuchangisha pesa zitakzo tumika katika ujenzi wa maabara amesema zoezi la ujenzi wa maabara katika shule za sekondari si la wananchi pekee .

Mh. majaliwa ameongeza kuwa serikali imetenga bajeti ya zaidi ya sh. bilioni 1 ambazo zitatumika kununua vifaa vya maabara zote zinazojengwa nchini nakwamba zoezi la ujenzi wa maabara limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa fedha ambapo amewataka wadau wa elimu na taasisi mbalimbali zenye uzalendo na taifa wajitokeze ili kuchangia ujenzi huo.

Kwa Upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa amesema Serikali imetangaza kutoa ajira za mkataba kwa walimu wastaafu wa masomo ya hisabati na sayansi ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo hayo nchini huku akiwataka maafisa elimu wa mikoa nchini kuorodhesha walimu hao kwa ajili ya kuanza tarabu za kuwajiriwa

Wakati huo huo Serikali imetangaza rasmi kuanza mchakato wa kuwahamisha wanafunzi wa shule ya sekondari ya Oswald Mang’ombe Wilayani Butiama ili majengo ya shule hiyo yatumike kwa ajili ya chuo kikuu cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati serikali ikikamilisha mchakato wa ujenzi wa chuo hicho cha sayansi na teknolijia katika kumuenzi

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...