Ujenzi wa Hospital ya Rufaa Mkoani Mara
Tatizo
kubwa la ukosefu wa huduma za afya za rufaa ambalo
limekuwa likichangia vifo vingi kwa wananchi wa mkoa wa
mara nchini Tanzania ,limeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya
serikali kuanza ujenzi wa hospitali kubwa ya rufaa ya
Mwalimu Nyerere Medical Center katika eneo la Kwangwa manispaa
ya Musoma mkoani humo.
Akipokea
madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya
moyo,upasuaji na wanawake na watoto ambao wamepelekwa mkoani
Mara kupitia mpango wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
ili kusogeza huduma za madakari bingwa kwa wananchi wa
mikoa wa pembezoni, Mgaga mkuu wa Hospatal ya Mkoa wa Mara Samson
Winani amesema tayari Serikali imenza utekelezaji wa ujenzi wa
hospitali hiyo.
kwa
upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya Bw Michael Kishiwa,amesema mfuko huo umechukua
uamuzi wa kupeleka madakatari bingwa katika mikoa ya
pembezoni baada ya kubaini idadi kubwa ya wananchi wamekuwa
wakipoteza maisha kwa kukosa uwezo wa kifedha kwa ajili ya
kutafuta huduma za matibabu za rufaa.
--
0 comments:
Post a Comment