WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Wednesday, September 25, 2013

SALEHE KUPAZA ASIMAMISHWA KAZI TWANGA PEPETA HATARINI KUIKOSA BONANZA YA TWANGA NDANI YA MTWARA


MUIMBAJI mwenye sauti ya aina yake Salehe Kupaza , amesimamishwa kazi  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Stars  (ASET)  Asha Baraka ,inayomiliki bendi kongwe ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta International.
Kusimamishwa kazi kwa muimbaji huyo kunatokana na kosa la utovu wa nidhamu aliouonesha mbele ya Mkurugenzi wake.
Akizungumza na Bongoweekend  Asha alisema kwamba ametoa amri asimamishe ili kujifunza adabu mpakaatakavyoambiwa vinginevyo.
liongeza kwa kusema kwamba kumsimamisha kazi Kupaza ni njia mojawapo katika kumwonesha kwamba anawajibu wa kumuheshimu yeye kama Mkurugenzi wake.Kupaza amekumbana na kibano hicho baada ya kumtusi bosi wake ikiwa ni bada ya kuhojiwa juu ya uchelewaji kazini  kutoroka  mazoezini na kwenda katika mazoezi ya bendi ya Victoria  na kuomba kazi .Pia aliwatukana wanamuziki wenzake .Adhabu hiyo ameanza kuitumikia kuanzia Jumatatu Septemba 23  bada ya kizaazaa kilichotokea kwenye ofisi za ASET zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam-

Friday, September 20, 2013

fm academia ndani ya mtwara naimbo zao mpya tizama hapa

Tuesday, September 17, 2013

BAADA YA KUTEKESEKA KWA MUDA MREFU NA MADAWA YA KULEVYA AISHA MADINDA AACHA UTEJA NA ARUDI TWANGA PEPETA IKIWEZEKANA KUWEPO KWENYE TOUR YA BONANZA LA TWANGA NDANI YA MAKONDE BAECH CLUB 29.9.2013


 Kutoka kulia aliyekuwa mnenguaji  nyota wa  bendi ya Twanga Pepeta Aisha Madinda na Mkurugenzi wake Asha Baraka  katika ofisi za ASET, zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Aisha Madinda  akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi  Mtendaji wa ASET , Kampuni inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka 'Iron Lady', Kiongozi wa bendi Luiza Mbutu, Kushoto kwa Aisha ni Haji Ramadhani 'Haji BSS'  na Kalala Junior.

Aisha Madinda hivi sasa anajifua kwa mazoezi ya hali ya juu akijiwinda kurudi tena ulingoni ambako ameahidi kuwa atakuwa moto wa kuotea mbali , hiyo ni baada ya kutopea katika utumiaji wa dawa za kulevya ambazo hivi sasa amefanikiwa kuacha na kuwa akipata huduma katika kliniki ya watumiaji wa dawa hizo iliyopo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza na Bongoweekend  katika nyakati tofauti wasanii wenzake kama Kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu 'Mamaa Brian' alisema kwamba wanashukuru mungu kwa kuona msanii mwenzao ameweza    kupambana na utumiaji wa dawa za kulevya na wanamkaribisha kwa mikono miwili kundini. Wakati huohuo Kalala Junior alisema kwamba "Kama nilivyotunga wimbo wangu wa Nyumbani ni Nyumbani' nasema Kurudi nyumbani siyo kosa hivyo jamii na wadau wampokee Aisha kwa mikono miwili.

Thursday, September 12, 2013

KALALA JONIOUR ASEMA TWANGA ALBUM 12 ZIMEWEZA KUTOKA KATIKA BAND HIYO KUTOKANA NA WATUNZI WENGI WALIOWEZA KUPITA KATIKA BAND HIYO NA HAKUNA HATA ALBUM MOJA KATI YA HIZO ILILIPULIA

Akizungumza na blog hii kuhusu show yao ya KALALA JUNIOUR amesema kutoa album kila kwa mwaka kwa twanga pepeta ni jambo ambalo limewezekana kutokana na watunzi wazuri wengi kupita katika band hiyo kwa kipindi tofauti na band nyingine kongwe ambazo zimekaa na wanamuziki kwa muda mrefu bila kuchanganya changanya ndio maana hata album zinakua chache ila twanga wamweza na pia ndio band ambayo imekomaa zaidi kiusanii kuliko band nyingine yoyote ya kisasa ukiachilia mbali za wazee wa zamani kama msondo na sikinde hakuna band nyingine iliyodumu kama twanga pepeta na ndio maana kuna watu wanaenda wanarudi na wasanii wengi hata walioanzisha band tofauti tofauti wamepitia twanga pepeta
Aidha amesema album ya nyumbani ni nyumbani ni album ambayo imekaa vizuri sana kutokana na mchanganyiko wa wasanii wanaunda safu ya wanamuziki wa twanga pepeta na kusema kuna wengine wamezidi kabisa kikazi.

Tuesday, September 10, 2013

SNURA MUSHI ASEMA WASICHANA WANAOCHEZA BILA KUVAA NGUO ZA NDANI HAWAJIAMINI NA HATA KAMA WANADHANI NA YEYE YUMO SASA AMEKUJA STYLE MPYA YA UVAAJI KWENYE JUKWAA GAUNI NDEFU LINA MPASUO NA KISHA NDANI PENSI NDANI NA BURUDANI ITATOKA KAMA KAWAIDA HATAKI KUPATA UMAARUFU KWA KUJIDHALILISHA sikiliza hapa

MWANADADA anaekuja kwa kasi katika medani ya muziki wa kaifrica na bongo flever tanzania snura mushu a.k.a snu sex majanga amesema kuwa wanaodhani wao huwa hawavai nguo za ndani kisha kupanda stejini kwa kudhani kuwa ndo kunawavuta wengi wanakosea na sasa yeye kuthibitisha hilo amesema kwa sasa atakuja na style mpya ya kushona gauni ndefu halafu ndani atavaa pensi itakayoonekana ili washindwe kusema yale wanaosema na kusema yyeye yupo kwenye muziki kwa kupata sifa kwa ajili ya kazi na sio kujidhalilisha kama wanavyafanya wengine
katika mahojiano na mimi hvi karibu nilimuuliza swali hilo kutokana na yale yanayojiri kwa baadhi ya waotot wa kike kupanda jukwani wakiwa watupu  ili kuweza kuonekana wanafanya kitu na hivi karibuni iliweza kumtokea mwadada shilole katika moja ya maonyesho ya fiesta ambapo aliweza kucheza na kuonyesha kila kitu cha ndani ambapo kilimfanya aweze kuandikwa sana kwenye magazeti lakini snura amesema kwake hilo halipo kabisa na ndio maana show zake zote huwa navaa nguo ndefu mpka chini na kwaku wamesema pamoja na kuwa

Monday, September 9, 2013

MUIMBAJI NGULI WA MUZIKI WA DANSI ROGERT HEGGA CATAPILA AFUNGUKA NA KUSEMA MAISHA NDIO YAMEMFANYA KUONDOKA EXTRA BONGO NA KUANZISHA BAND YA SUPERSTAR NA WALA HANA UGOMVI NA ALLY CHOKI INGAWA KAMARADE HAKURIDHIA AONDOKE

Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi ambae amewahi kutamba katika mabd tofauti tofauti na mara hii akitokea extra bongo na kuunda band ya super star ambayo itakua ikiongozwa na magwiji mbali waliwahi kutamba kipindi cha nyuma na bado wakiwa wanaendelea kufanya muziki vizuri kwenye game hiyo ya muziki a dansi ambapo aliweza kuwaorodhesha wanamuziki baadhi watakaounda superstar ni AMIGOLAS BABA NA SOPHII,VICOTR MKAMBI,MSAFIRI DIOF na wengine ambao watakuwa wanawasaidia katika uimbaji


AIDHA ROGERT  amesema kuondka kwake extra bongo ni kama alikua ana ugomv na ally choki hapana ila ameondoka kimaslahi zaidi kutoka na kwamba masiha yanaendelea wwadau na mashabiki wasimchukulie vibaya ila kila mt akifanya kitu ana malengo yake kwa hiyo kwa sasa ameona jia nyingine ya kujiingizia kipato kuliko  mwanzo ni kutokana na band yao hiyo ambayo amesema bado hawajaitangaza rasmi kuanza kwake kwa kuwa wako katika hatua za mwisho za kuweza kuirekebisha safu ya waimbaji na wapigaji ingaw amesema mpka sasawameshaanza mazoezi na kwa kuanza tu wataanza kupiga katika mahotel huku wakijipanga kuja kuanza kupiga sehemu mbali mbali.


Friday, September 6, 2013

WIMBO WA DIAMOND MY NUMBER ONE WAZIDI KUZUA KIZAZAA BAADA YA DYNA KULALAMIKA AMEIBIWA BEAT NA DIAMOND NA MKIGOMA MWENZIO BABA LEVO ASEMA DIAMOND KAMUIBIA CHOURUS YA WIMBO WAKE MPYA WA MY NUMBER

Huku ikiamina wana lekalutigite ni wamoja hivi karibuni umezika utata babada ya diaomnd kuachia wimbo wake wa my number one ambao ndio gumzo la mji kwa sasa mwanadada dyna alilalamika kuibiwa wimbo huo beat yake na alikua akitaka kufanya na diamond mwenyewe lakini mwisho wa siku kaja kuisikia kwenye wimbo huo wa diamond, hayo yakiwa bado ya moto mkigoma mwenzie waliokwenye kampuni moja ya kigoma all stars BABA LEVO ameibuka na kusema kuwa diamond kamuibia chourus ambayo walipanga kuimba wote kwenye wimbo wake mpya ambao alitaka kuutoa na kuuita SWITIE SWITIE lakin diamond kaiba kidogo na kuitengeneza my number one.
akizungumza na mimi leo baba levo anasema habari ya wimbo huo amekuja kuipata babada ya kuambiwa na baadhi ya wanachoa cha ifm ambaowalikuwa wa kwanza kuusikia huku yeye akiwa ameshawahi kuumba sehemu mbalimbali na hivyo na yeye kuwaomba aweze kuupata ili ausikilize na mwisho wa siku kaja kuusika baada ya kuuachia wimbo huo na ndipo alipamua kushatikia mashabiki wake kuwa DIAMOND kamubia chrous ya wimbo ambao yeye baba levo alitaka amshirikishe,

LAKINI nilipomuuliza kuwa diamond ni mmoja kati ya wana lekallutigite je aliweza kumtafuta kumuuliza aone anasemaje kuhusiana na hilo baba level kasema diaomond ndio wa kumtafuta yeya kwa kuwa anajua alichokifanya ila kwa sasa hawezi kusema lolote na wimbo huo aliotaka kuutoa meghairi na hawezi kuutoa tena kwa kuwa yeye ndio ataonekana kuwa amemuiga diamond,
huu ni wimbo wa pili ambao DIAMOND anashtumiwa kuuba wa kwanza ukiwa ule wa NATAKA KULEWA ambapo PASHA alikua ameshatolea wimbo wa AMEKUA.
 sasa hapa je DYNA NA BABA LEVO WANATAFUTA KICK KWA DIAMOND AU KWEL JAMAA ANAWEZA KUWA AMEIBA KWELI

Thursday, September 5, 2013

NEY WA MITEGO ASEMA MADAM RITHA HATA HELA YA KUMLIPA YEYE KUWA JAJI BONGO STAR SEARCH NA KUONGEZA KUWA AMEOGOPA KWENDA MAHAKAMANI KWA KUWA ANAJUA ANACHOKIFANYA NA ANGEENDA NDIO ANGEONA KAMA HAWEZI KUMLIPA,PIA ASEMA WALIOMTISHIA KWA SMS WAMEOMBA MSAMAHA ILI ASIWATAJE

Mwanamuziki wa hip hop anaetikisa kwa sasa na wimbo wake wa SALAM ZAO, Ney wa mitego amefunguka baada ya shutuma za kuwa madam ritha amesema hata akimpeleka mahakamani kuwa hana hela za kumlipa kwa yale aliosema, ney amevimba kama ana uhakika na kesi hiyo  angeenda mahakamn ashinde aone kama hata mlipa hiyo hela ila kwa kuwa anajua anachokifanya katika  bongo starsearch ndio maana hajaenda huko mahakamani huku akiongeza kwa kusema madam ritha mwenyewe ndio alimatafuta ili aende kuwa jaji ndani ya bongo star search hali ambayo amesema kuwa hawezi kwenda kamwe kwa kuwa hana pesa ya kumlipa hata kidogo kwa hivyo kama la salam zao limegusa bora akae kimya tu,
AIDHA ney amesema kuwa kwa sasa amewasaemeh wale waliokuwa wanampa vitisho kwa kuwa amesema wamekula hela za rambirambi za msiba wa albert mangea na steven kanumba ambao aliahidi endapo wangeendelea kumfatafata basi angewaanika hadharani hivyo wamekaka wameyasuruhuisha na sasa kazi zingine zinaendela kama kawaida na
Pia ney amesema hivi karibuni ataachia video yake ya salam zao ambao itakua tofauti na watu wanavyofikiria

CRISTIAN BELLA AFUNGA ASEMA MALAIKA BAND HAITOKANI NA VICTORIA SOUND NA WALA HATAGEMEI KUCHUKUA WANAMUZIKI KUTOKA BENDI HIYO NA BAND HIYO IKO CHINI YAO ILA MKURUGENZI WA VICTORIA NI MMOJA WA WADHAMINI WA BAND YAO

KWA sasa anajulikana zaidi kama king of the melodies ambae alikua rais wa akudo impact na hatimaye kwa sasa kusimama kama solo project amefunguka na kuweza wazi kuwa ameajiriwa ili kutengeneza band ya pembeni ya vicoria sound na kuibadilishajina kuita malaika badn na kusema hilo suala sio la ukweli malaika band ni band inayojitegemea na wala haitokani na victoria na wala hafikirii kuchukua wanamuziki wa victoria labda waweze kuomba ili aweze kuwasajili kwa kuwa bado ypo kwenye mchakato wa kutafuta wasaidizi katika band hiyo wakiwemo wapigaji wapya na waimbaji wengine wa back up kwa kuwa band hiyo yeye,totoo,na andrew sekidia ndio waanzilishi na wamepweza kupata udhamini tu kutoka kwa wadau wa muziki iliwaweze kuendelea kufanya nao kazi na huku akisisitiza kuwa yeye ataendelea kubaki solo ila solo wa musiki wad dansi lazima uwe na kundi ambalo linakupa back up katika show na yeye kama mwanamuziki inamulazimu kufanya show nyingi sana live kwa kuwa kuimba kwa back up sio kiwango chake katika muziki.
aidha bella amesema mpka sasa hajafanya interview yoyote kuhusiana na band yao hiyo kwa kuwa kuna mambo bado wanaendelea kufatilia ila pia watu wajue kubme yeye hajaajiliwa ila wamepata mdhamini aliewapa vyombo ili waweze kufanya kazi pamoja kwa makubaliano maalum na wadhamini hao ni mkururgenzi wa zamani wa akudo bw michael na aliekua mkurugenzi wa victoria sound DANIEL DENGA 
 amesisitza kuwa malaika band haihusiani kabisa na victoria band.

Wednesday, September 4, 2013

BAADA YA KUACHIA WIMBO WAKE WA CHUKI BILA SABABU DOGO RAMA A.K.A BULLDOZA ASEMA WADAU WATARAJIE MAKUBWA ZAIDI KUSHINDA ALBUM YAKE YA KILOMETA 10000

MWANAMUZIKI wa dansi anaekuja juu sana katika medani ya muziki huo hapa nchini akiwa anafanya kazi na band ya TWANGA PEPETA lakini wakati huo huo akitengeneza kazi zake mwenye ambazo anasema kwa lengo la kuonyesha kipaji chake na zaidi lakini pia kujiongezea kipato kwa kuwa uongozi wa band hiyo umekubaliana na suala na kwa sasa tayari ameshaipeleka sokoni album yake aliyoiachia mwakajana ya KILOMETA 10000 ambayo anasema imefanya vizuri na ndio iliyompa nguvu ya kuweza kufanya album nyinginemwaka huu ambayo hata hivyo imechelewa kutokana na kusubiri kwanza album ya NYUMBANI NI NYUMBANI iweze kusogea na yeye aweze kuapt nafasi ya kufanya yake
DOGO RAMA amesema kwa sasa maeutanguliza wimbo wa chuki bila sababu na kusema ameufanya kama utambulisho wa album hiyo ambayo nyimbo karibu zote zipo tayari kasoro wimbo mmoja tu ambao ataumalizia hvi karibuni na kusema kwa sasa ameamua kupunguza urefu wa nyimbo ili aweze kupata airtime ya kutosha katika media ingawa kwa bendi kufanya hviyo kunawabana sana

Tuesday, September 3, 2013

MKALI ALITEMBA NA STONO MUSICA AMBAE KWA SASA NI MWALIMU KUTOKA JUMBA LA VIPAJI T.H.T KARDINAN GENTO AACHIA NGOMA YAKE KAMA SOLO ASEMA HANA MPANGO WA KUANZISHA BAND KUIBUA ALBUM YAKE HIVI KARIBUNI

Mwanamuziki alitemba katika miaka ya 2000 KARDINAL GENTO ameachia ngoma yake baad ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo lakini alishughulika zaid katika kuwaandalia wasanii kutoka jumbal avipaji t.h.t sasa ameamua kurudi tena kwenye medani ya muziki na ameweza kuachia ngoma moja aliyoipa jina la NYUMA YAKO na kusema huo ni utangulizi katika utambulisho wa album yake mpya ya UWEZO ambayo atairekodi katika mitindo tofauti tofauti ikiwemo rhumba,na bongo flver na style nyingine tofauti
gento amesema alikua kimya kwa kuwa alikua anatafakari kuweza kupunguza urefu wa nyimbo kwa kuwa zamani walikua wakirekodi dk nyingi sasa ili na yeye wimbo zake ziweze kupewa airtime ya kutosha ameona bora aje kivingine apige muziki wa kiafrica lakini ukiwa una dakika ambazo media nyingi zinataka na si hivyo tu ili isimchoze msikilizaji na vitu vingine
Ameongeza kuwa kwa sasa wadau wa muziki wampokee kama mwanamuziki baada ya kufanya kazi ya kuwanoa wasanii katika jumba la vipaji na sio kwamba ataacha ila ataendelea zaidi kufanya hivyo lakini wakti atkua akiendelea na kufanya muziki

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...