WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Friday, October 31, 2014

SERIKALI YASEMA HAITAWAONDOA WANANCHI WA ARUMERU WENYE MGOGORO NA MWEKEZAJI

 
 Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. George Simbachawene
Serikali imesema haitawaondoa wanakijiji wa cha Singu kata ya Sigino katika Halmashauri ya Babati Mkoani Manyara nchini Tanzania ambao wana mgogoro na mwekezaji katika eneo hilo na kusema kuwa itawapanga katika utaratibu wa Mipango Miji.

Hayo yamezungumzwa na Naibu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. George Simbachawene wakati alipotembelea wilayani humo katika kutafuta ufumbuzi na kutatua migogoro ya Ardhi wilayani humo.

Mh. Simbachawene amesema kuwa wakazi wa eneo hilo itabidi wakubali kutanuka kwa mji na kuweza kupewa hatua za kufanya katika kupanuka kwa halmshauri hiyo hivyo kuwataka waanze kujipanga katika kukabiliana na changamoto za kupanuka kwa Mji.


HALMASHAURI ZATAKIWA KUACHA KUWALIPISHA WALIMU KODI KATIKA NYUMBA ZILIZONJENGWA NA SERIKALI


                     Naibu Waziri wa Elimu anaeshughulikia Elimu Mh. Kassimu Majaliwa

Serikali imesema kuwa Halmashauri ziache kuwatoza walimu kodi za mwezi katika nyumba ambazo zinajengwa na serikali kwa kuwa lengo la serikali kuwarahishia walimu kuweza kuishi karibu na maeneo ya Kazi na kufanya kazi kwa ufanisi.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Elimu anaeshughulikia Elimu Mh. Kassimu Majaliwa na kusema kuwa Halmashauri zinazowakata walimu mishahara yao kama kodi za pango za nyumba zilizojengwa na serikali ni makosa Makubwa.

Mh. Majaliwa amesema kuwa lengo la serikali kuzijenga nyumba hizo ni kuwajengea mazingira mazuri ya ufundishaji walimu na kuweza kuwapa urahisi wa kuhudhiria kazini ikiwa ni katika mpango wa kupata matokeo makubwa sasa katika sekta ya Elimu.


VIJANA WATAKIWA KUJITOKEZA KUOGMBEA NAFASI MBALIMBALI CHAGUZI ZIJAZO


                          Mbunge wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Neema Mgaya
Vijana nchini Tanzania wamehamasihwa kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi ya Serikali za Mitaa, Udiwani na Ubunge, pamoja na Urais katika chaguzi mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika kuanzia Mwezi Disemba mwaka huu na mwakani.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar es salaam na Mbunge wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Neema Mgaya wakati akiongea na East Africa Radio na kuongeza kuwa vijana ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu nchini na kuwataka kutumia fursa zilizopo ikiwemo ya uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Bi Mgaya amesema vijana wengi wamekuwa hawaaminiki katika uongozi kutokana na kutokupata mafunzo ya uongozi Pia amewataka vijana kuachana na utegemezi na tabia ya ubinafsi, badala yake wajiunge na vikundi ili waweze kuleta fursa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali nchini.


Friday, October 24, 2014

MIFUKO YA JAMII YATAKIWA KUSAIDIA JAMII NA SIKUNYANG'ANYA WANACHAMA

                     Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi Hawa Ghasia
Mifuko ya jamii hapa nchini imeshauriwa kuelekeza nguvu zaidi katika kuwahamasisha wananchi wasio katika sekta rasmi ili kuboresha maisha yao badala ya kuendelea kugombea wanachama walio katika sekta kama ilivyo hivi sasa.

Rai hiyo imetolewa na waziri wan chi ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Hawa Ghasi wakati akifungua mkutano wa saba wa LAPF jijini Arusha unaowakutanisha wanachama wa mfuko huo waajiri na wadau wengine muhimu wa mfuko huo.

Aidha waziri Ghasia ameiomba LAPF kutazama upya uwezekano wa kuanza kutoa fao la elimu kwa wategemezi wa wanachama ili kuwapunguzia mzigo mkubwa wanchana wa kusomesha watoto ambao kwa sasa ni changamoto kubwa.

MFUMO WA ELIMU NDIO TATIZO LA AJIRA AFRIKA MASHARIKI

                         Mwenyekiti Baraza la Biashara Afrika Mashariki
Mwenyekiti wa baraza la biashara la nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki bw. Felexs Mosha amesema jitihada za kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wakiwemo wanaomaliza Vyuo Vikuu zitakuwa na mafanikio kama serikali za nchi wanachama zitakubali kuwa na mfumo shirikishi wa elimu na unaozingatia mahitaji soko la ajira kwa sasa

Bw. Mosha ameyasema hayo katika mkutano wa baraza hilo la biashara na baraza la vyuo vikuu la afrika mashariki, ulioandaliwa kwa ushirkiano na benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki, unaofanyika Kigali, nchini Rwanda.

Katibu mtendaji wa Baraza hilo Prf. Mayunga Nkunya amesema pamoja na changamoto zinazowakaabili wahitimu wa vyuo vikuu katika nchi za Afrika Mashariki uchunguzi umeonyesha kuwa wana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kama mfumo uliopo utabadilika

KUNA WAFANYAKAZI WALIFANIKISHA WIZI WA BENKI YA STANBIC-KOVA

                Kamanda kanda maalumu Dar es Salaam Kamishina Suleimani Kova
Watu wasiofahamika wanaosadikiwa kuwa ni Mjambazi jana walivamia Benki ya Stanbic katika tawi la Myfair jijini Dar es Salaam nchini Tanzania na kupora kiasi cha fedha ambacho kiasi chake bado hakijafahamika.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa wa jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Kamishana Suleiman Kova ameziagiza benki zote za jijini humo kuhakikisha zinalindwa na askari polisi ili kukabiliana na uhalifu unaojitokeza mara kwa mara.

Kamanda Kova pia amesema wizi huo unaonekana ni mpango uliofanywa na baadhi ya watumishi wa banki hiyo kutokana na wezi hao kufanya tukio hilo na kuchukua fedha kwa Urahisi Zaidi.

Aidha ameongeza kuwa waajiriwa wa mabenki hayo watafanyiwa uchunguzi pamoja na kuchukuliwa alama muhimu ikiwamo alama za vidole ili kukabiliana na uhalifu unaofanywa na baddhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu.

Kova amesema kuwa katika uchugnuzi wa Awali wamegundua wizi wa mtandao wa ndani ya banki kwasababu hakuna nguvu iliyotumika na wakapata taarifa kutoka kuwa kuna watu wamefungiwa chooni lakini kuna vitufe vya kubonyeza vya hatari ili kutoa taarifa lakini havikubonyezwa.


Thursday, October 16, 2014

MATAIRI CHAKAVU CHANZO CHA AJALI BARABARANI


                       GARI NA TAIRI CHAKAVU
Idadi kubwa ya wamiliki na madereva wa magari nchini Tanzania hawafahamu umri wa matumizi ya matairi ya magari, kiasi kwamba wengi wao huishia kununua matairi ambayo muda wake wa kutumika umekwisha na hivyo kusababisha ongezeko la ajali za barabarani.

Uchunguzi wa East Africa Radio umebaini kuwa kutokana na ukosefu wa uelewa, wanunuzi wa matairi mara nyingi wamekuwa wakiangalia zaidi upya na mwonekano wa matairi, badala ya alama za kitaalamu zinazoonyesha tarehe ya kutengenezwa pamoja na mwaka wa ukomo wa matumizi wa matairi husika.

East Africa Radio imefanya mahojiano na mfanyabiashara wa matairi Bw. Aloyce Aron, dereva wa muda mrefu mzee Kassimu Msisi na fundi wa magari Bw. Machimu Ludovick ambao walikuwa na haya ya kusema.

                      PROF. JUMMANNE MAGHEMBE
Idadi kubwa ya wakazi wa Tanzania hasa waishio maeneo ya vijijini wapo hatarini kuendelea kukosa maji safi na salama kutokana na kushindwa kutunza vyanzo vya maji hali inayochangiwa na shughuli za binadamu.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano wa pamoja wa wadau wa sekta ya maji, wenye lengo la kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango wa miaka sita katika sekta hiyo.

Profesa Magembe amesema ni lazima serikali na wananchi kwa ujumla kutambua hali hiyo na kuchukua hatua za makusudi kutunza rasilimali hiyo kwa lengo la kuwa endelevu na amewataka wananchi kufuata sheria zinazoelekeza namna ya kuhifadhi vyanzo vya maji.

MASHIRIKA YA KUZUIA UKIMWI YAPANGA KUTOKOMEZA KABISA UGONJWA HUO AFRIKA MASHARIKI


Mashirika na Taasisi zisizo za kiserikali zinayohusika na masuala ya Ukimwi yametakiwa kuimarisha ushirikiano ili kuweza kuleta mafanikio ya kuhakikisha wanaufuta kabisa ukimwi Afrika mashariki.


Akizungumza na wadau wanaowakilisha asasi zinazounda Mitandao inayojihusisha na VVU na Ukimwi Kaimu Mratibu wa Tume ya Taifa yakudhibiti Ukimwi Visiwani Zanzibar ALLY Mbrarouk Omary amesema kamwe vita dhidi ya Ukimwi haitaisha kama hakuta kuwa na ushirikiano baina yao.



Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali kutoka nchini Uganda yanayojishughulisha na masula ya UKIMWI, Namanya Baram amesema mtandao wao wenye zaidi ya mika 18 sasa una imani na Tanzania kama nchi kubwa wataweza kubadilisha uzoefu katika masula ya kupambana na VVU, na UKIMWI.

Monday, October 13, 2014

ASILIMIA 35 YA WATOTO NCHINI TANZANIA WAMESHAFANYIWA VITENDO VYA UKATILI



                                        Mkurugenzi LHRC, Dkt Hellen Kijo- Bisimba
Asilimia 35 ya watoto chini ya miaka 18 nchini Tanzania wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kuolewa wakiwa na umri mdogo hali inayochangia kushindwa kumu kutunza familia.

Akizungumza jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa kituo cha Sheria na Haki za Bianadamu,Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amesema mkoa wa shinyanga unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya ndoa za utotoni kutokana na baadhi ya mila na desturi za wakazi wa mkoa huo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtandao wa Kupinga ndoa za utotoni TCEMN, Justa Mwaituke amesema tatizo la ndoa za utotoni ni kubwa na linaathiri maendeleo kwa watoto wanaoolewa wakiwa na umri mdogo.


SERIKALI YATAKIWA KUMUENZI NYERERE KATIKA KUREKEBISHA ELIMU




                                        Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Katika kumuenzi muasisi wa taifa la Tanzania mwl Julius Kambarage Nyerere hii leo wananchi nchini Tanzania wameitaka serikali kuendeleza maono ya muasisi huyo katika kuboresha mfumo wa elimu nchini.

Wakizungumza na EastAfrica Radio baadhi ya wananchi hao wamesema Mwl Nyerere alikuwa tayari katika kupambana na kuwashinda adui umaskini, maradhi na ujinga kwa kuboresha mfumo wa elimu nchini ikiwemo jitihada za kukubali kuyazika maslahi yake binafsi kwa ajili ya wengi.
Aidha wamesema kuwa suala la uoga ndio limekuwa adui mkubwa wa maendeleo ya elimu na Taifa kwa ujumla na limezuia mabadiliko chanya ambayo yangeweza kutokea ili kulikomboa taifa ikiwemo upatikanaji wa elimu bora ambayo inamjenga mwanafunzi kujitegemea.

wakati maadhimisho haya ya kitaifa yatafanyika mkoani Tabora, yakiambatana na kuzimwa kwa mwenge wa uhuru, familia ya Mwalimu, muasisi wa Taifa la Tanzania wao wameadhimisha misa ya kumuombea mwalimu anayetajwa kuwa mwenye heri na harakati za kumtangaza zikiendelea, familia hiyo imesalia kijijini Mwitongo, na kudai kuwa siku hadi siku kumbukizi hiyo inapoteza maana.

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...