GARI NA TAIRI CHAKAVU
Idadi
kubwa ya wamiliki na madereva wa magari nchini Tanzania hawafahamu
umri wa matumizi ya matairi ya magari, kiasi kwamba wengi wao
huishia kununua matairi ambayo muda wake wa kutumika umekwisha na
hivyo kusababisha ongezeko la ajali za barabarani.
Uchunguzi
wa East Africa Radio umebaini kuwa kutokana na ukosefu wa uelewa,
wanunuzi wa matairi mara nyingi wamekuwa wakiangalia zaidi upya na
mwonekano wa matairi, badala ya alama za kitaalamu zinazoonyesha
tarehe ya kutengenezwa pamoja na mwaka wa ukomo wa matumizi wa
matairi husika.
East
Africa Radio imefanya mahojiano na mfanyabiashara wa matairi Bw.
Aloyce Aron, dereva wa muda mrefu mzee Kassimu Msisi na fundi wa
magari Bw. Machimu Ludovick ambao walikuwa na haya ya kusema.
0 comments:
Post a Comment