Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Katika
kumuenzi muasisi wa taifa la Tanzania mwl Julius Kambarage Nyerere
hii leo wananchi nchini Tanzania wameitaka serikali kuendeleza maono
ya muasisi huyo katika kuboresha mfumo wa elimu nchini.
Wakizungumza
na EastAfrica Radio baadhi ya wananchi hao wamesema Mwl Nyerere
alikuwa tayari katika kupambana na kuwashinda adui umaskini, maradhi
na ujinga kwa kuboresha mfumo wa elimu nchini ikiwemo jitihada za
kukubali kuyazika maslahi yake binafsi kwa ajili ya wengi.
Aidha
wamesema kuwa suala la uoga ndio limekuwa adui mkubwa wa maendeleo
ya elimu na Taifa kwa ujumla na limezuia mabadiliko chanya ambayo
yangeweza kutokea ili kulikomboa taifa ikiwemo upatikanaji wa elimu
bora ambayo inamjenga mwanafunzi kujitegemea.
wakati
maadhimisho haya ya kitaifa yatafanyika mkoani Tabora, yakiambatana
na kuzimwa kwa mwenge wa uhuru, familia ya Mwalimu, muasisi wa Taifa
la Tanzania wao wameadhimisha misa ya kumuombea mwalimu anayetajwa
kuwa mwenye heri na harakati za kumtangaza zikiendelea, familia hiyo
imesalia kijijini Mwitongo, na kudai kuwa siku hadi siku kumbukizi
hiyo inapoteza maana.
0 comments:
Post a Comment