WAY

Friday, October 31, 2014

VIJANA WATAKIWA KUJITOKEZA KUOGMBEA NAFASI MBALIMBALI CHAGUZI ZIJAZO


                          Mbunge wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Neema Mgaya
Vijana nchini Tanzania wamehamasihwa kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi ya Serikali za Mitaa, Udiwani na Ubunge, pamoja na Urais katika chaguzi mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika kuanzia Mwezi Disemba mwaka huu na mwakani.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar es salaam na Mbunge wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Neema Mgaya wakati akiongea na East Africa Radio na kuongeza kuwa vijana ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu nchini na kuwataka kutumia fursa zilizopo ikiwemo ya uchaguzi wa serikali za mtaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Bi Mgaya amesema vijana wengi wamekuwa hawaaminiki katika uongozi kutokana na kutokupata mafunzo ya uongozi Pia amewataka vijana kuachana na utegemezi na tabia ya ubinafsi, badala yake wajiunge na vikundi ili waweze kuleta fursa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali nchini.


0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...