WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Wednesday, February 27, 2013

VICTORIA SOUND KUTAMBULISHWA RASMI IJUMAA HII NDANI YA MANGO GARDEN TAYARI WANATIKISA NA MBILI HEWANI SHAMBA LA BIBI NA MWISHO WA SIKU kusindikizwa na extra bongo wazee wa kizigo na jahazi morden taarab

BAND ambayo imekua gumzo kwa muda mfupi iliyochini ya kocha wa dunia prince muumini mwinjuma kufanya utambulisho wa band yao siku ya ijumaa ya tar 1.03.13 pale mango garden ambapo wataweza kuzitambulisha pia nyimbo zao mpya na zile ambazo zimeanza kutikisa kwa vituo vya radio kama vile shamba la bibi ambayo imezua sana gumzo kwamba ni dongo kwa band ya twanga pepeta ambapo ndipo alipotoka mtunzi na kiongozi wa band hiyo muumini mwinjuma lakini na wimbo mwingine wa wazri sonyo uitwao mwisho wa siku ambao uko katika mahadhi ya rhumba huku wakitegemea kuzitambulisha nyingine ambazo  zipo tayari lakini bado kwenda kurekodiwa kama vile MAMA BAHATI,UTAFITI WA MAPENZI
                             VICTORIA SOUND KWENYE MOJA YA MAONYESHO
 Akizungumza na blog hii meneja wa victoria khamis amesema kila kitu kimekamilika huku akiwataja wanamuzi waimbaji wanaounda band hiyo ni pamoja na JANUARY alietoka mapacha watatu,CIANA ambae ametoka TWANGA ACADEMIA,MUSA KARENGA Aambae ni rapa pia AMETOKEA T.OT. RAMSON BUSHOKE pamoja na WAZIRI SONYO NA MUUMINI MWINJUMA
aidha meneja ameongeza kusema kuwa baada ya utambulisho wataingia tena kambini kwa ajili ya maandalizi ya album yao ya kwanza kabisa

Tuesday, February 26, 2013

MAPACHA KUZINDUA ALBUM YA YARABI NAFSI TAR 02.03.2013 BUSNEES PARK SASA WAPO KAMBINI BAGAMOYO WAKIJIFUA KWA MAZOEZI MAKALI KWA AJILI YA UZINDUZI HUO UNATARAJIWA KUTIKISA JIJI kusindikizwa na mashujaa,lina na khadija kopa

Nikiongea na mkurugenzi wa mapacha watatu KHALID CHOKORAA amesema uzinduzi wa album ya YARABI NAFSI ambayo itakua na nyimbo nane zikwemo NAONEWA walimshirikisha ALLY KIBA ambao upo katika mahadhi ya bongo flever CHANZO WANAUME waliomshirikisha MALKIA WA MIPASHO KHADIJA OMARY KOPA,NYINGINE NI WOSIA WA BABU,na nyinginezo huku akitanabaisha kuwa album yao itakua ya tofauti zaidi ambapo itakua ina ladha mbali mbali ikiwemo mduara,sebene,rhumba,bongo flever

                                       WAKURUGENZI WA MAPACHA 3
aidha khalid aliitaja timu yake ya waimbaji ambayo itafanya mauaji siku hiyo ni pamoja mwanadada mwenye sauti ya kipekee CATY a.k.a FIRST LADY WA MAPACHA,JOHN CENA,KAMBI SETH pamoja na wao wwakurugenzi JOSE MARA, KHALID CHOKORAA
AIDHA show hiyo ya uzinduzi itasindikizwa na band kama mashujaa musica,khadija kopa,pamoja na linah msanii wa bongio flever  huku akisema kuwa wamamua kusindikizwa na wanamuziki hao kutokana na kila mmoja ana mashabiki wake hivyo kuongeza mvuto zaidi katika uzinduzi huo utakaofanyika bussness park makumbusho

Wednesday, February 20, 2013

BAADA YA KUTIKISA NA CAROLINA SKYLIGHT KUACHIA NYINGINE MPYA

BAND inayokuja kwa kasi sasa nchini ya skylight band yenye maskani yake jijini adr-es-salaam ambao kwa sasa wanatikisa na wimbo wao wa carolina band ya skylight ambayo kwa mujibu wa kiongozi wa band hiyo aneth amesema wameamua kuachia wimbo mwingine hiyo ikiwa ni katika mipango ya kuanda album ambayo itawatambulisha kama skylight lakini vile vile na kuweza kujitangaza zaidi na kuweza kulikamata game la muziki wa dansi huku akiamini kuwa kwa sasa muziki wa kiafrica umeanza kuibuka tena baada ya watu wanaounda band kuweza kujipanga zaidi ili kuweza kufikia mafanikio ya miziki ya kimataifa zaidi
LAKINI pia ANETH ambae ameshawahi kupiga katika band tofauti tofauti hapa nchini kama viile b band,machozi band na baadae kushiriki tusker proct fame amesema kwa sasa wameandika nyimbo nyingi zaidi na wataanza kufanya show mikoa tofauti na wataanzia mwanza hivi karibuni
SKYLIGHT BAND KAZINI

Monday, February 18, 2013

RAMA PENTAGONE AELEZEA KILICHOMTOA EXTRA BONGO NA KUHAMIA TWANGA PEPETA

Msanii wa siku nyingi katika kundi la extra bongo ambae kwa siku ya jumamosi alitambulishwa rasmi katika band ta twanga pepeta ameweka bayana kile kilichomtoa katika band hiyo na kuhamia twanga pepeta.
RAMA PENTAGON ambaye ameshiriki vyema katika albuma mbili za extra bongo kiwemo mjini mipango na mtenda akitendewa amesema kuwa ameondoka extra bongo kwa sababu ya kimaslahi kwa kuwa ameweza kukaa muda mrefu katika bannd hiyo ambapo alikua akilipwa kidogo lakini kutokana na mwenendo wa band inavyokwenda ndipo alipoamuia kumuomba mkurugenzi amuongezee kipato lakini majibu aliyoyapata hayakumridhisha ndipo  mkataba wake ulipoisha akaamua kujiunga na twanga pepeta ambapo alikua na mazungumzo nao kwa muda mrefu na kusema wamekubaliana vya kutosha na rasmi ataanza kazi na twanga hivi karibuni.

Thursday, February 14, 2013

TWANGA PEPETA KUZINDUA LEO VIDEO YA SHAMBA LA TWANGA PEPETA LEO NDANI YA MZALENDO PUB KATIKA SIKUKU YA WAPENDANAO

Wakiwa katika maandalizi ya kuachia album yao ya kumi na 3 mwaka huu ambapo wamekwishakamilisha nyimbo takribani nne mmoja wapo ni ambao unatikisa sasa katika vituo mbali mbali vya radio ambao umetungwa na rapa geryson semsekwa wimbo ukiitwa SHAMBA LA TWANGA PEPTA ambapoo inasemeka ndio unaweza kubeba jina la album ingawa badi hajafahamika rasmi kuhusiana hilo lakini leo rasmi ndani ya mzalendo pub katika siku hii ya wapendanao wanaenda kuzindua video ya shamba la twanga pepeta.

TIP TOP CONECTION WAHAMIA UPANDE WA FILAMU WATIA FILAMU MOJA SOKONI HUKU ZENGINE ZIKIFATA JUMAPILI KUFANYA USAILI WA KUSAKA VIPAJI VYA WAIGIZAJI WATAKAOKUA CHINI YA TIP TOP NA SASA NI MUZIKI NA FILAMU

KAMPUNI ya tip top conection iliyo chini ya abdu boge ambayo ilikua inalisimamiza kudi zima la tip top conection ambalo linaundwa na MADEE,TUNDA MAN,PINGU,na wengiine kibao sasa mkurugenzi wa kundi hilo ameweza kugeukia upande mwingine ambapo kwa sasa imeundwa tip top film ambayo itakua na waigizaji kama HUSNA SAJENT ambaeni muigizaji maarufu pia aliwahi kushiriki mashindano ya kimwana wa twanga pepeta lakini kwa sasa ndio msemaji wa tipo top conection film ambao leo ameweza kufunguka na kusema sasa wameshaingia rasmi katika tasnia hiy ambapo film yao ya kwanza inayoitwa ASINA
                                                            HUSNA SAJENT
HUSNA amesema siku ya jumamosi watafanya usaili wa kusaka wasanii watakaoweza kuwa chini ya tip top na kuweza kuanza kuigiza katika filamu zinazokuja sio kama sasa ambavyo filamu zao walikua wanachukua wasanii kutoka sehemu tofauti  na usaili huo utafanyika siku ya jumamos magomeni kgera kwenye maskani ya tip top connection kuanzia saa mbili asbhi na kuendelea na watakaopatikana hapo ndio watakaoweza kujiunga na tip top conection film.

BAADA YA KUPATA AJALI BUIBUI ASEMA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA HAWANA UMOJA WALA USHIRIKIANO MAANA AMEKAA WIKI MOJA HOSPITAL BILA HATA MWANAMUZIKI MMOJA KWENDA KUMUONA

Msanii wa kizazi kipya kutoka nyumba ya vipaji tanzania t.h.t aliepata ajali ya pikipiki hvi karibuni na kuvunjika miguu yote miwili amefunguka na kuseam wasanii wa muziki wa kizazi kipya hawana ushirikiano sio kama wa bongo movies baada ya kukaa kimya bila ya mwanamuziki yoyote hata kutoka ndani ya t.h.t alieweza kwenda kumuona hosptalini hapo japo kumjulia hali zaidi ya mwalimu wake kardinal gento pamoja na bosi wake alienda kulipa hela ya matibabu zaidi ya hapo ni marafiki zake wakribu na mafans wake na hata baba yake mdogo ameweza kujitokeza na kusema wasanii wa bongo flever waige mfano wa wasanii wa bongo movies ambao kwenye matatizo huwa wanajitahidi sana kusaidia.

hata hivyo bui bui amesema kuwa atamalizia video ya wimbo wake mpya wa BORA UNGESEMA akiwa na mihogo kenye miguu na kwenye baiskeli iwe kama kumbukumbu lakini vile vile na uharaka wa video wenyewe ambapo wimbo wake ameutoa mwishoni mwa mwaka jana hivyo wadau wanahitaji ngoma mapema kabla hajaachia ngoma nyingine kwa kwa sasa album yake imekwisha kamilika

ROSE NDAUKA AKANA KUTAPELI!



KIMYA kingi na stori kibao mtaani juu ya kuingia mitini na ‘mkwanja’ wa  waigizaji  wapya,  hatimaye staa  kutoka  tasnia ya filamu  Bongo, Rose Ndauka kwa  mara nyingine  ameibuka na  kutupilia mbali taarifa  kuwa  amekuwa akiitisha usahili kwa wasanii chipukizi na kuwachukulia fedha kisha  kutokomea kizani  bila kuwashirikisha katika filamu zake.

Akizungumza na  na cloudsfm.co mapema leo  kufuatia uwepo wa  habari kuwa  kuna kundi la wasanii wamefika kwenye  ofisi zake zilipo maeneo ya Kinondoni  Jijini Dar kudai fedha  zao  baada ya kushinda usaili uliofanywa na  Rose  na kuambulia  patupu pasipo kushirikishwa katika filamu yoyote ya msanii huyo.

“Sijawahi kuchukua fedha ya mtu na kumnyima nafasi, kinachotokea ni tatizo la wasanii kukosa uvumilivu kwani si rahisi kumchukua kila mtu aliyeshiriki na kushinda usahili na  kumuweka kwenye filamu,   tunachokifanya ni kutoa nafasi moja  kutokana na kipaji halisi kisha wengine wanafuata, lakini ajabu naona wengine wanalalamika bila  kuelewa  lakini sijawahi kula hela ya mtu”  alisema  Rose.

Saturday, February 9, 2013

BAADHI YA MATUKIO YALIYOJIRI KWENYE BIRTHDAY YA LUIZA MBUTU JANA

LUIZA MBUTU AKIWALISHA KEKI BAADHI YA WANAMUZIKI WA TWANGA

Friday, February 8, 2013

TUNDA MAN AFUNGUKA KUHUSIANA NA KUVUJA KWA NGOMA YA MAREHEM SHAROMILIONEA NA YEYE ASEMA WATU WA KARIBU NDIO HUWA WANAHUSIKA KUVUJA KWA KAZI ZAO LAKINI ASEMA SASA ATATOA NGOMA MBILI KWA MPIGO KWA KUWA AMEKAA KIMYA SANA,

MSANII wa miondoko ya bongo flever tunda man asema kuvuja kwa ngoma zao kunatoka kwa watu wa karibu ambao mtu unakua umemwamni kama mshkaji lakini mwisho wa siku unaikuta ngoma mtaani na ndivyo ilivyotokea kwenye ngoma ya vuluvulu au nawavuruga ya marehem hussein mkieti A.K.A sharomilionea aliyoshirikishwa yeye kuwa mtaani na kusema kuwa hana taarifa yoyote kuhusiana na kutoka kwa ngoma hiyo kwa kuwa ilikua bado kufanyiwa mixin na vitu vingine na kusema kwa sasa ni bora nyimbo ukamsikiliz mshkaji mmoja tu ili hata ikivujua ujue  ni nani kaivujisha kilichopo sana ni kukiamini tu utakachokitengenza baasi
AIDHA TUNDA amesema kwa mwaka huu ataachia ngoma mbili mfululizo moja akiwa amemshirkisha msanii toka kiumeni CHEGE CHIGUNDA na nyingine akiwa amemshirikisha msanii mchanga anaemsimami yeye mwenyewe anaekwena kwa jina la sungura.
                                         TUNDA MAN A.K.A CAPTAIN
tunda ameongeza kwa kusema kuwa ameamua kutoka ngoma mbili kwa mpigo i kutokana na ukimya wake toka mwaka jana mwezi wa nane na demu sio hivyo imebidi awape mashabiki wake kitu kipya lakini si hivyo tu anatoa ngoma nyingine kwa ajili ya kumsaport msanii anamsimamia kwa sasa sungura  ambae anaamini anakuja kufanya mapinduzi katika game

Wednesday, February 6, 2013

TWANGA KUMFANYIA LUIZER MBUTU BIRTHDAY jumamosi

 


MWIMBAJI na Kiongozi wa Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” Luizer Mbutu anataraji kufanyiwa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (Birthday Party) siku ya Jumamosi tarehe 09-02-2013 katika ukumbi wa Mango Garden uliopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar es salaam.

Luizer Mbutu hii ni mara ya pili kufanyiwa sherehe hiyo huku kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana, sherehe ilifanyika katika Club ya Maisha iliyopo Oysterbay.

Ikumbukwe ASET Imeamua kumfanyia Luizer Mbutu sherehe hiyo kwa mara yapili mfululizo kwa kutambua mchango wake mkubwa alioutoa katika bendi ya Twanga Pepeta kwa kudumu kwa muda mrefu bila kuhama na kwa kufanya kazi kwa kujituma bila ya kuchoka toka aanze kazi rasmi ndani ya Bendi mpaka leo.

Sambamba na sherehe hiyo Twanga Pepeta kama ilivyo kawaida yao watainogesha sherehe hiyo ya Kiongozi wao kwa masebene matamu yatayoendana na nyimbo nzuri zilizo na meseji zilizojitosheleza kutoka kwa wanamuziki wenye vipaji vya viwango vya hali ya juu kabisa.

Wadau mbalimbali wamealikwa kuhudhuria sherehe hiyo ili kutoa sapoti kwa Kiongozi huyo wa Bendi katika siku yake ya kuzaliwa kwa kuwa utatumika utaratibu kama wa mwaka jana wa kulishwa keki kwa wadau na marafiki walio karibu na bendi ya Twanga Pepeta.

Monday, February 4, 2013

HATIMAYE TEJA KITALE ACHUKUA JIKO PANDE ZA MWANANYAMALA SASA SIO KAPELA TENA

MSANII wa tasnia ya filamu za comedy na maigizo pamoja na muziki wa bongo flever hatimae jana mchana ameuaga ukapela rasmi na kuweza kuingia katika maisha ya kifamilia zaidi baada ya siku ya jana ya 03.02.13 kufunga ndoa maeneo ya mwananyamala harusi ambayo ilihudhuriwa na mastar kibao wa bongo flever na filamu hivyo kufanya kitale kuwa mmoja kati ya wasanii wachache walioa katika tasnia hiyo ambayo inasemekana kuwa inaongoza wasanii wake kwa kuto ingia katika suala la ndoa mapema zaidi huku wengi wao wakitawalia na skendo za hapa na pale
                                     KITALE AKIWA NA MKEWE
akiongea na blog hii KITALE amesema ameamua kuchukua uamuzi huo kutkana wasanii wengi kujisahau nafasi zao katika jamii kama ni mfano bora lakini pia ni katika kutimiza mari za mwenyezimungu pamoja na kujiongezea thawabu ila pia akisema ni bora kufanya hivyo mapema kwa kuwa maisha yenyewe haya hayatabiriki kwa sababu walipanga kuoa wote yeye na rafiki yake kipenzi sharomilionea lakini hatimaye mungu akamchukua bila kutimiza ndoto zake.
kitale amesema anafuraha sana sasa kuitwa mume wa mtu.

Sunday, February 3, 2013

MAPACHA KUINGIZA SOKONI ALBUM YAO YA "YARABI NAFSI" WAMESHAMALIZA VIDEO YAO NA ALIKIBA -NAONEWA SAS KUFANYA BONANZA KILA JUMAPILI NDANI YA MIKOCHENI RESORT


Album hii mpya ya mapacha watatu inakwenda kwa jina la "yarabi nafsi"na ina nyimbo sita nyimbo ya kwanza kuotoka iliitwa..USIA WA BABU..(2)CHANZO WANAUME..feat KHADIJA KOPA(3)NAONEWA Feat ALI KIBA(4)ni amba yo inabeba jina la album ambapo tayari imekwisha kuwa tayari na itaingia mitandaoni siku ya ijumaa..inaitwa YARABI NAFSI ..humu utaskia waimbaji chipukizi wa mapacha watatu..KAMBI SETI na mwanadada CAHTERIN CINDY
                                       JOSE AND KHALID CHOKORAA
BAND inayoongizwa na magwiji wawili wa muziki wa dansi tanziania JOSE MARA,KHALID CHOKORAA pamoja na wanamuziki wengine kama caty tha first lady,kambi seti na wengineo ambao wanaunda kundi la mapacha watatu wameshakamilisha video ya wimbo wao mpya wenye mahadhi ya bongo flever ambao wamemshirikisha mkali wa bongo flever tanzania ALLY KIBA na katika wimbo ambao umekua gumzo sana kwa wadau wa mziki kutokana nauwezo ulifanyika katika colable hiyo ya naonewa ambapo jose na khalid wameonyesha uanamuziki wao na sio  uimbaji na hivi karibuni wataanza kuisambaza video hiyo ya naonewa,
                       FIRST LADY MAPACHA CATHERINE CIDY
MAPACHA WATATU ambao wameshakamilisha album yao ya YARABI NAFSI ambapo ndani yake kutakua na nyimbo sita  wataenda kuzindua mwanzoni mwa mwezi wa tatu baada ya kuahirisha kuizindua valentine kuwa kuweza kwanza kukamilisha maandalizi mazuri zaidi.

                                 KAMBI SETHI WA MAPACHA WA 3
MAPACHA WATATU ambao siku hizi kila jumapili wanapiga bonanza lao pale mikocheni resort ambapo linaanzia mchana kwa kuwa na mchanganyiko wa buradani nyingine nyingi na hii nikuweza kuwapa buradani wapenzi wao wa rika zote

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...