WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Wednesday, March 28, 2012

CHALZ BABA AZIDI KUNG'ARA SASA NDIE RAIS MPYA WA MASHUJAA MUSIC BAND

Mwanamuziki anaetikisa sasa katika ulimwengu wa music wa dansi tanzania CHALZ BABA a.k.a KINGUNGE a.k.a TORRES ameukwaa urais wa mashujaa music band katika uchaguzi uliofanyika siku ya jana katika ukumbi wa mashujaa pub uchaguzi ambao uliwahusisha wanamuziki katika upigaji kura huku uchaguzi huo ukisimamiwa na wadau wawili pamoja na mnenguaji sweet baby.chalz alipata kura 19 kati ya 26 nae chalz baba amesema ataliongoza kundi hilo kwa usawa kwa wanamuziki wote chalz baba ni rais wanne tangu kuanzishwa kwa mashujaa KAJO ambaye alichukua urais kutoka kwa JADOH hayo yamefanyika katika kwa ajili ya kuendelea kuliiiimarisha kundi linalotishia uhai wa makundi mengine nchini na tanzania na kuleta upinzani mkali kwa makundi kongwe nchini na huku moja ya mafaniko yao kwa sasa ni kuingiza nyimbo yao inayotikisa katika vituo mbalimbali vya radio na tv HUKUMU YA MNAFIKI ambao umeingia katika kinyang'anyiro cha nyimbo bora ya band wakati huo nyimbo nyingine ambayo ilitungwa na chalz baba UNGENIELEZA nayo ikiendelea kutikisa pamoja na wimbo waliomshirikisha nguli wa muziki wa dansi na wakiafrica PAPA WEMBA uliopewa jina la UMENINYIMA ukiendelea kutesa.
      LE PREZDAA OR RAIS YA MASHUJAA BAND CHALZ BABA KINGUNGE
Wakati huo huo chalza baba amweza kutoa ofa kwa walemavu wawili wa macho wenye vipaji vya kuimba kuweza kurekod wimbo ambao utawashirikisha mapacha watatu katika studio za sophia record walaemavu hao ambao nao wanatikisa kumbi mbali mbali za starehe  nao ni WAKUZIBA INTERNATIONAL PAMOJA NA MANJEGEKA ambao leo wameingia studio kurekod wimbo wao wa PIGO LA MOYO hii ikiwa ni remix ya ule wa kwanza ambao haukufanya vizuri wakuziba tarekod pamoja na khalid chokoraa pamoja na kalala jounour yote kwa udhamini wa PRESDENT CHALZ BABA
    CHALZ AKIPOKEA TUZO KUTOKA KWA KING KIKII MZEE WA KITAMBAA CHEUPE
   RAIS CHALZ BABA AKIWA NA 33 WOTE WA MASHUJAA BAND.

Monday, March 12, 2012

JE WAJUA ALIPO STAR WA MUZIKI WA DANSI WAZIRI SONYO BAADA YA KUTOKA JELA SASA ANARUDI KIVINGINE NA BAND NYINGINE

Aliewahi kutamba na band ya T.O.T plus kipindi hicho ikiwa chini ya LE GENERAL BANZA STONE wakati huwa akiwa na TOTO TUNDU NA ABDUL MISAMBANO  Band ambayo ilitikisa ulimwengu wa dansi nchini kwa vibao kama MTAJI WA MASIKINI,ELIMU YA MJINGA lakini ukiacha yote hayo kibao kilichowahi kushika hatu ya muziki ni MASIMANGO ambacho kilitungwa na WAZIRI SONYO a,k.a KOMANDO sasa amerudi tena baada ya kutoka jela .WAZIRI SONYO alishwahi kutamba na band kama MVIKO SOUND,T.O.T PLUS,.AFRICAN REVOLUTION NA NYINGINE KIBAO KIBAO
      WAZIRI SONYO ENZI ZAKE AKITIA MASAUTI
Kwa sasa WAZIRI SONYO yupo mkoani Tanga ambapo yupo na band ya NYUMBANI CLASSIC BAND ambao itakua ni band ya hotel huku wakisubiri ukumbi wao mkubwa wa jijin Dar-es-salaam uishe ili wahamishie majeshi jijini na kuanza upinzani na band zinazotamba na kutikingisha jiji lakini kwa mujibu wa waziri sonyo amesema tayari wapo mbioni kuitoa album ya nyumbani clasic band ambayo itakua na nyimbo sita ikiwamo NAZIHESABU HATUA ZANGU ambao ni utunzi wake mwenyewe huku band hiyo ikiwa na mwanadada anaejulikana kwa jina la lady ambae ni mzoefu wa nyimbo za copy  inagawa vile vile akitegemea kutengeneza nyimbo ambayo itaingia katika album ya NYUMBANI CLASSIC BAND
    WAZIRI SONYO AKIWA NA LE GENERAL BANZA STONE WAKIKUMBUSHIA ENZI KIDOGO KABLA SONYO HAJAPATA BAND.
SONYOamesema pamoja na mashabiki wake kummis toka alivyoenda jela lakini kwa sasa anaamini kuwa mwanzo mzuri wa kung'ara tena ndio huu na mashabiki wake wavute subira mengi mazuri yaja kwa waziri sonyo na band yake ya NYUMBANI CLASSIC.
                          WAZIRI SONYO a.k.a komandoo!

Sunday, March 11, 2012

UJIO MPYA WA NDANDA KOSOVI NA WATOTO WA TEMBO AACHIA MBILI HEWANI NA AJIPANGA NA ALBUM

Nani anependa muziki wa dansi na hamjui ndanda kosovo kichaa mtaalamu wa muziki wa dansi aliewahi kutikisa nchini kwa rap na vibao tofauti tofauti toka akiwa fm academia international kipindi hicho kbla ya kutawanyika na mafahari wawili yaani ndanda na nyoshi kila mmoja kushika hamsini zake basi yeye ndio aliweza kukitunga kibao cha kwanza cha fm academia baada ya kutoka jela kipindi hicho akiwa na kina NYOSHI EL SADAAT,MALUU STONCH,MULE MULE FBI,KING BLAIZE,PATCHO MWAMBA na wengina kama KINA CARDINAL GENTO hapo walitamba na kibao cha WAJELAJELA  lakini baadae ndanda alitoka fm academia na ikaundwa fm academia wajelajela gwaa na ndanda akaanzisha STONO MUSICA yyeye akiita wajelejela Original ambapo aliweza kutamba na kina MALUU STONCH,CHAI JABA,PATCHO MWAMBA NA WENGINE ambapo vibao vilivyoweza kutamba kipindi hicho kikiwemo BINADAMU ambapo ni utunzi wake ndanda huku wakitamba na RAP ZA KIDEDEA,NA KAOKOTA BI G
          NDANDA KOSOVO KICHAA KIONGOZI WA WATOTO WA TEMBO
Ndanda hakuishia hapo aliweza kuachana na stono musica na kuelekea nchini marekanai ambapo kwa mujibu wa yeye mwenyewe aliweza kwenda kwa shughuli za kimuziki ambazo zilikua na mafaniko makubwa sana na baadae akarejea nchini tanzania ambapo akawa anaendela na shughuli za kawaida lakni ndipo hapo alipoweza kuanzisha kundi la watot wa tembo kwa mara ya kwanza ambapo aliweza kuchukua wanamuziki toka kcongo ambao mwisho wa siku waliweza kumkimbia kutokana na kutoelewana ambao wote wamekimbilia mashujaa musica ambao nao kwa sasa wapo kweye ramani ya muziki wa dansi na kutishia band nyingine kongwe!
      NDANDA KOSOVO AKIWA NA WATOTO WA TEMBO AKIPIGA SHOW
 Yote ya yote sasa ndanda kosovo kwa sasa maeachia nyimbo mbili ambazo zinasumbua katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni moja ambayo itabeba jina la album akiipa jina la FOCUS kwa kiswahili kizuri alisema malengo na nyingine akiita KWANINI ambazo moja maepiga katika mtindo wa sebene tupu huku nyingine akipiga katika mtindo wa rhumba sebene huku akisema  mashabaiki ambao wanasema ndanda amekwisha basi wasikilize ujio mpya wa wa album yake ambapo atakua na watoto wa tembo!
    NDANDA  AKIWA NA WANAE KAZINI
JE NDANDA ANAWEZA KUWA AMERUDI AU NDIO SIKIO LA KUFA  AU KIMYA KINGI 

Friday, March 9, 2012

MKALI WA MUZIKI WA KIAFRIKA TOKA KUSINI AMBAE PIA NI MLEMAVU WA MACHO(KIPOFU) WAKUZIBA INTERNATIONAL AACHIA MOJA KIDEONI IKIITWA I WANNA KNOW

Mkali wa muziki wa dansi mzee wa masauti wa kusini WAKUZIBA INTERNATIONAL ambaye pia ni mlemavu wa macho kwa sasa akifanya kazi jijini dar na band tofauti tofauti kama solo artist ikiwamo fm academia,extra bongo na nyinginezo ameachia video yake mpya kabisa ambayo itaanza kucheza katika vituo vya televishion. wimbo huo ambao ameachia akiwa na mlemavu wa macho mwenzake MANJEGEKA umeibwa kwa lugha mbili ikiwa kiswahili na lugha ya kingereza na zouk rb ambayo inapatikana katika album yao inayoitwa MWAKA WA HASARA album ambayo imejaa aina tofauti za ladha ikiwemo bongo flever,zouk.rhumba,sebene wakiwa wamtengenezea studio tofauti tofauti
          WAKUZIBA INTERNATIONAL MLEMAVU MWEYE KIPAJI CHA AJABU


album ya MWAKA WA HASARA kuna nyimbo kama PIGO LA MOYO,MWANOLA,MALAIKA,KUMUKO aliyoimba kwa mtindo wa zouk, kwa mujibu wa wakuziba anasema video yao imetengenezwa na producer zed hii ikiwa ni katikaa maandali ya kutoa album yao nyingine ambayo itawashirikisha wasanii tofauti tofauti
      WAKUZIBA AKIFANYA SHOW NA TWANGA PEPETA

Wednesday, March 7, 2012

LUIZA AFUNGUKA KUHUSIANA KUCHAFULIWA KWA TWANGA PEPETA NA WATU KUJIPATIA UMAARUFU KUPITIA BAND YAO JE WAJUA TWANGA NI BAND INAYOOGOPWA KUPITA ZOTE!?

Kiongozi wa Twanga pepeta luiza nyoni mbutu afunguka kuhusiana na shutuma kila mwanamuziki akihama basi wa twanga pepeta hasa kuhusiana na mwanamuziki aliekuwa huru kwa muda mrefu ALLY AKIDA kuwa ametokea twanga pepeta amsema hiyo ni kutafuta biashara kupitia wao na  na sio kitu kizuri katika muziki lakini amesema yote ya yote amsema mwisho wa ubaya ni aibu kwa hayo yanaoongelea kwani mambo ya kuipaka tope twanga pepeta ingawa amesmea twanga ni kama mti wa matunda ambao watuchuma matunda lakini mwisho wa siku utazaa mengine
luiza amezungumza hayo wakati akiongea na mimi katika kiopindi cha extra africa na kusema mbinu za kuichafua zimebainika na wao wamejipanga vya kutosha ikiwamo kuongeza wanamuziki wengine na wacheza show wengine ambao wengi wao wanamaliza mikataba yao oman.
        nikiwa na kiongozi wa band ta twanga pepeta luiza nyoni mbutu kbla ya show mtwara
Aidha luizaalizungumzia kuondoka kwa dansa wa kike LILIAN INTERNET TUNGARAZA aliehamia mashujaa masema amendoka kwa kuaga na kwenda kuangalia upepo sehemu nyingine na yeye kamapa bless zote ingawa kama msanii kamamdogo ake hajapenda lakni ndio masiha ingawa pia kasema kama akiona kule hakumfai milango ya kurudi twanga pepeta ipo wazi wakati wowote kwa sababu pale ni kama kwa mama yake kwa kuwa amelelewa katika band hiyo.

      lilian internet aliehamia mashujaa mushujaa band kuimarisha safu ya ushambuliaji
aidha luiza amesema wamekwisha anza machakato wa kuandaa album ya kumi na mbili huku wakiwa tayari na nyimbo moja ambayo bado haijapewa jina lakini tayari washaanza kuperfom kwenye kumbi mbalimbali

        hao ndio wana wa kutwanga na kupepeta walipoangusha balaa mtwara ndani ya makonde.

Tuesday, March 6, 2012

PAMOJA NA NYIMBO BAND YAKE KUWEKWA KWENYE NYIMBO BORA ZA BAND KATIKA KILI MUSIC AWARDS ALI CHOKI ASEMA HATOSHIRIKI KATIKA TUZO HIZO

MKURUGENZI ambae pia ni muimbaji wa band inayotikisa jiji la bongo kwa extra bongo LE KAMARADE ALLY CHOKI aweka wazi kuwa kamwe hatoshiriki katika tuzo hizo kwa sababu kuu mbili moja ikiwa ni ubabaishaji wa waandaji na vile vile yupo kwenye mkataba na kampuni ya bia ya SBL wakati tuzo hizo zinawezeshwa na kampuni ya bia TBL kwa hiyo hicho pia ni kiwazo tosha kwakwe kushiriki katika kinyang;anyiro hicho ambapo siku hizi kinakwenda kwa mtindo wa kupiga kura.
kwa mujibu wa alli choki amesmea toka tuzo hizo zianze pampja na ukali wa nyimbo zake hajawahi kupokea tuzo hata mara moja na hata wakati alipotoa album akiwa na twanga pepeta ambayo iliitwa mtaa wa kwanza na  baada kuibuka n ushindi lakini mtunzi ikaja kusemekana kuwa mtunzi wa nyimbo hiyo ni ASET kwa hiyo jina lake ni nadra sana kukubaika kwa waandaaji wa kili music awards kwa hiyo kamwe na milele daima hawezi kushiriki katika tuzo hizo labda zianzishwe nyingine.
       G.MBONGO NIKIWA NA MZEE WA KIJIKO LE KAMARADE ALLY CHOKI
lakini hata hivyo ally choki amesema amemruhusu rapa wake ferguson kushiriki tuzo hizo kwa kuwa yeye ni mwanamuziki anaejitegemea mua wowote anweza kuamua ni wapi anataka kwenda kufanya muziki lakin badn kama band haitaweza kushiriki katika tuzo hizo.
 aidha alichoki ameliongela sakata la mwanamuziki ambae ni mpiga magita yote aliekuwa twanga pepeta katika kipindi cha nyuma na aliewahi kupiga katika band yake kwa muda kuhamia mashujaa kwa mujibu wa ally kasema kuwa ALLY AKIDA aliwahi kupiga kama day worket tu lakini sio kama mwajiriwa rasmi kwa hiyo kuhamia kwake mashujaa si kutoka katika band yake bali alikua katika shughuli nyingine mbali na mziki na pia amesmea ally akida kwa sasa kiwango chake cha kupiga kimepungua snaa kutokana na kuwa nje ya muziki kwa muda mrefu
    CHOKI AKILIONGOZA KUNDI LAKE KATIKA SAFU YA UIMBAJI
Aidha kwa mujibu wa ally choki amesema ana mpango wa kuibomoa tena twanga pepeta ambapo jumatatu atwatambulisha rasmi wanamuziki hao ambao atawachukua kutoka twanga pepeta ingawa amekataa katakata kuzungumzia ni kina nai ambao atawachukua kutoka kandi band hiyo kongwe.
     LE KAMARADE ALLY CHOKI MZEE WA KIJIKO AKIWA KATIKA POZI




Monday, March 5, 2012

HILI NDILO BALAA WALILOFANYA TWANGA -LINDI NA MTWARA- JAMAN MH!


Bendi kongwe nchini Tanzania na yanye mashabiki lukuki nchini pia yenye vipaji lukuki vya waimbaji wa kitanzania na na wanaopiga muziki wa kitanzania wamefanya bonge moja la show na kuwaacha watu wa kusini wakisimulia kila kukicha kumbe twanga hata aondoke nani moto wake ni ule ule fatilia picha za show hizo lindi na mtwara
        MIMI NDIO NILILIANZISHA KWA KUWATAMBULISHA WANA TWANGA

                       KAZI ILIANZA HAPA HUYU NI J4 ALIANZA KWA KUWAPANGA KWANZA
    ANCO VENA AKAMFUATA J4 KUJAZA VOCAL ZA UKWELI TWANGA BANA!
  MZUKA ULIZIDI KUPANDA BAADA YA KUPANDA RAPA GREYSON SEMSEKWA
   VOCALIST WA TWANGA DOGO RAMA ALIKUJA KUZIDISHA MASHAMBILIZI DUH!
    HAPA VIONGOZI WA TWANGA AMIGOLAS NA LUIZA WAKIWAPANGA WACHEZA  SHOW
    HAPA SASA VIONGOZI WA TWANGA NAO WAKAVAMIA KUIMARISHA MASHAMBULIZI DUH! HII NI MTWARA BANA

      Hapa sasa kuanzia kushoto kwenda kuliani ni Asha sharapova kiongozi,mary kimwana manywele,vicy buree,pamoja na maria salome walinza kushambilia jukwaa wengine wanasubiri wewe hatariiiiiiiii

         ah! dada luiza nyoni mbutu akasonga kusherehesha aisee ilikua balaaaa
     nae khadija mnoga kimobitel jembe alikamua kama kawa
      Hapo chacha akapanda tetemente grace akiwa na waziri mkuu wa shows madela mwanadada mrembo fashaaa na kiongozi wa show wakiume saidi sharooo
   hapa sasa watu wa kusini tunapenda kusema kumnogeaaaaaaaaaaaaaaaa hahahahaha
  aikutanie mtu bana mizuka ikipanda ni balaaaaaaaaaa c jui kama utaamini ilivyokua?
   mkongwe mcd handsome akizikung'uta tumba loh!
  mkongwe jojoo jumanne aki[iga kwa sataili ya aina yake bass gitaaaaaaaaa
   stage master le por du drums James kibosho akiliwa
   mkali kutoka kusini ni mlemavu wa macho lakini ni mwenye kipaji cha hali ya juu wakuziba international alikuwepo kuwasindikiza twanga

 BAADA YA HAPO SASA BALAA SI LIKAHAMIA LINDI
      BALAA LILIHAMIA OCEANIC WE ACHA TU AISEEE DUUH!@
          KAZI ILIKUA KUBWA KWELI KWELINI GRACE.SAIDI NA FASHAA NA MANDELA
     show ilikuaa bomba vibaya viabya iasee duh!
       mashabiki wa lindi wakipagawisha na shangwe la twanga ni hatari tupu
NB Twanga pepeta walizindua siongle yao ambayo bado haijapewa jina lakini wameshaanza kuiperfom kwenye stage ambayo imetungwa na raper GREYSON SEMSEKWA ITAKUWEPO KWENYE ALBUM YA KUMI NA MBILI YA TWANGA PEPETA YA KIMATAIFA DATS WATS UUUUUUUUP HAV A GUD DAY WAPENDWA


Friday, March 2, 2012

TWANGA PEPETA KUTIKISA KUSINI MTWARA IJUMAA,JUMAMOSI LINDI

Wanajulikana kama african stars kwa sasa ni TWANGA PEPETA INTERNATIONAL wakiwa chini ya wakali kibao akiwemo mkongwe MUUMINI MWINJUMA mmoja kati ya wakongwe waliowahi kujizolea mashabiki kwa kiwango kikubwa sana nchini tanzania akiwa na Banb tofauti taofauti zikiwemo alizoweza kuzimiliki mwenyewe na kama DOUBLE M,BWAGAMOYO SOUND na ht alikoaptia sana jina na heshima AFRICAN REVOLUTION TAMTAM alipotamba na kibao cha TUNDA
     MUUMINI AKIFANYA BALAA AKIWA TWANGA
PIA TWANGA WATAKUJA NA MOJA KATI YA WAKALI WANAOCHIPUKIA KATIKA MUZIKI WA DANSI DOGO RAMA vuala PAMOJA NA WENGINE KIBAO WAKALI WA KUCHEZA NA KUIMBA PIA!
                         NIKIWA NA DOGO RAMA JEMBE LA TWANGA PEPETA
       WAKALI WA TWANGA NA WARMBO PIA JANET NA LUIZA NYONI WAKIJIACHIA

    MUIMBAJI NGULI WA TWANGA PEPETA LILIAN TUNGARAZA INTERNET

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA CRISTINA BELLA WA AKUDO IMPACT AACHIA MOJA KALI

Mkali wa masauti na presidaa wa akudo impact cristian bela aptocalpto bela baada ya kutamba na album yake binafsi ya DONT PANIC  yenye nyimbo kali zilizotamba kama YAKO WAPI MAPENZI,MUZAMIL KATUNZI huku styl ya rap ikiwa ni BOMOA BOMOA sasa aja kivingine akimshirikisha ngili wa masauti tanzania BANANA ALY ZAHIR ZORO kutoka B BAND ngoma inayoitwa USILIE ambayo ipo kwenye staily ya rb rhumba kama mnavomjua bela na rhumba na kama unavojua rhumba lazima uwe na masauti na rb lazima uwe na masauti hapo ndipo utapoona utamu wa wimbo huo wa USILIE

         NIKIWA NA PRESIDAA YA AKUDO PRESIDAA YA MASAUTI, BELLA
      CRISTIAN BELLA AKITUMBIZA MASHABIKI

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...