WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Tuesday, March 25, 2014

JE WAJUA MITIHANI ALIYOPITA DOGO RAMA KATIKA MUZIKI JE WAJUA ASHAWAHI KUWA ANAPANDA JUKWAANI AKIMBA SAUTI HAITOKI NA MARA NYINGINE HATA KUKOHOA DAMU HIYO WAKATI AMEINGIA TU TWANGA PEPETA JE WAJUA ALIKUWA MPIGA DEBE NA MCHOMA CHIPS JIJINI MWANZA KUPITA BLOG HII AMEFUNGUKA

Dogo rama mwanamuziki anaesimama vizuri kwa sasa ndani ya twanga pepeta katika safu ya uimbaji akishirikiana kwa ukaribu na kina kalala junior, luiza mbutu,badi bakule na wengineo anasema katika changamoto ambazo hawezi kuzisahau maishani mwake ni pamoja kuamini alikuwa anarogwa pindi tu alipifika twanga pepeta huku akiwashukuru kina Marehemu MCD,ABUU SEMHANDO lakini pia kina JOJOO JUMANNE NA LUIZA MBUTU kwamba avumilie na ndio mapka leo yupo twanga.
Kwa mujibu wa maelezo ya dogo rama mwenyewe anasema wakati anafika twanga pepeta mwanzoni kabisa ambapo kipindi hicho alikuta twanga imekamilika walikuwepo kina Chalz baba,kalala junior,khalid chokoraa,furguson,amigolas na wengine sasa walati huo akitafuta nafasi alijikuta wakati mwingine akikohoa damu baada ya kushuka jukwaani lakini pia kuna kipindi sauti ilikua inakauka bila kujielewa na kusema alipata wakati mgumu sana wakati huo lakini baadae akweza kueleweka na kutokatamaa na ndio mpka leo bado yupo twanga,


Lakini changamoto nyingine ambayo anasema anaikumbuka sana ni pamoja na kupiga debe jijini mwanza pia kuchoma chips na kushona viatu yote akitafuta pesa ili aweze kutoka na hatimae ndipo alipoweza kuanza uimbaimba katika mabdn tofauti tofauti jijini mwanza na hatimaye ndipo alipoweza kuja dar na kuendeleza kazi aliyokuwa akiwaaza na kuiota kila siku,

Monday, March 24, 2014

JONIKO FLOWER ASEMA WATU WASIFIKIRI KARUDI CHUCHU SOUND YEYE ALIWEZA KUFANYA SIKU MOJA KWA AJILI YA KUMBUKUMBU ILA HAWEZI KUPIGA TENA NAO KWA SIKU ZOTE ASEMA KITU AMBACHO HAKISAHAU KATIKA MAISHA YAKE NI WAKATI CHUCHU SOUND INAKUFA WALIWEZA KUPIGA VYOMBO VYA MZIKI KICHWANI TOKA MANZESE MPAKA MWANANYAMALA NI KITU ASICHOKISAHAU KATIKA MAISHA YAKE YA MUZIKI

Joniko flower ambae kwa sasa anaimbia band ya skylight band asema watu wasifikiri ataendelea kupiga na chuchu sound ila alifanya vile kwa kuwa kuwa ulikuwa ni  mkataba wa show ya siku moja ya kumbukumbu ya ya wenzao waliopoteza masiha kipindi hicho lakini pia kukumbuka kule walikota na chuchu sound kwa kuwa ni band iliyotengeza historia katika maisha yake,

Joniko asema kitu ambacho kinamkumbusha chuchu sound ni kitendo wakati band inaelekea kufa wanamuziki waliweza kugawana vyombo kubeba kuvirudisha kwa tajiri mwananyamala kutoka sinza huku yeye akibeba drums na wengine wakibeba vyombo vingine,nakuongeza kuwa hiyo ni changamoto ambayo amweza kukutana na na kutoisahau katika tasnia ya muziki

Aidha  joniko amefunguka kuhusiana na wanamuziki kubebwa na media wkati hawana uwezo wa kufanya kazi jukwaaani kwa kuwafurhisha watu na kusema hali hiyo imeenea sana hapa tanzania wengi wanafanya kazi kwa mazoea na sio uwezo wa kazi

Wednesday, March 19, 2014

MSANII WA FILAMU KUTOKA KENYA ANAEFANYA SHUGHULI ZAKE NCHINI UJERUMANI AKANA KUWA DEMU WA WASANII NA AKANUSHA MADAI YA KUTAKA KUIVUNJA NDOA YA BOB JOUNIOUR ASEMA WASANII WA AAFRIKA MASHARIKI YEYE NDIO HUWA ANAWAPA SAPPORT WAFIKAPO UJERUMANI

Msanii naekuja juu katika tasnia ya filamu afrika mashariki ambae anafanya shughuli zake ujerumani ASHLEY TOTOO amefunguka kuhusiana na skendo yake inayomkabili kuwa ni demu wa wasanii wa kutoka afrika mashariki ambao huwa wanaenda kufanya show nchini ujerumani na kusema kuwa yeye kule huwa anakua kama mwenyeji wao wa kuweza kuwatembeza sehemu mbalimbali ni marafiki wakawaida na wala si kama watu wengine wanavyofikiria kuwa kila msanii anaenda nchini humo basi lazima atoke na ashley.



Mbali na hilo pia ashley amekana kama alihusika na na kutaka kuvunja ndoa ya bob junior kwa kuwa ye alikua karibu nae kipindi amekuja nchini kenya na kusema kuwa wasanii wengi wa afrika mashariki ni rafiki zake na sio bobo jounior tu ila kuna kina ALLY KIBBA na wengineo kwa maswala ya bob juniour na mkewe ilikua ni mambo yao ya ndani wenyewe wala yeye hakuhusikaka kama ilivyokua imesambaa katika vyombo vya habari.
Kwa sasa amesema ameconcetrate katika kuandaa movies yake mpya ambayo atafanya na wasanii wa tanzania ili kuweza kupanua zaidid soko la filamu la afrika mashariki huku akiamini kuwa tanzania imepiga hatua kubwa katika tasnia ya swahili filamu afrika mashariki.

Tuesday, March 11, 2014

BAADA YA KUIWEKA PEMBENI SUPER STARS BAND NA KUTUA KWA WANAJESHI WA RUVU STARS BAND WATAKA KURUDISHA ENZI ZA MABAND YA SERIKALI LAKINI NA USHINDANI KAMA ILIVYOKUWA ZAMANI MAGEREZA,POLIS JAZZ BAND KIMALUMALI NA NYINGINE WAACHIA TATU KWA MPIGO NI BAND INAYOUNDWA NA WANAMUZIKI WAZOEFU WA DANSI TANZANIA AKIWEMO ROGERT HEGGE CARTAPILA JE WATAWEZAA???

Band inayoundwa na wakongwe kama Rogert hegga( cartapila kilimanjaro),Amigolas,muhina panduka(toto tundu)khadija mnoga(kimobitel)waziwa kalala,jojoo jummane toka twanga pepeta,sele momba toka twanga pepeta,champion aliekuwa mpiga drums wa malaika band,victor mkambi(profesional keyboard)ambapo kati yao walikuwa wanaunda super star band ambayo ilianza kazi kadhaa lakini bila kurekodi na mwisho wa siku ndio wakaweza kuignia mkataba na jeshi na kwenda kama walimu wa band ya ruvu star band ambapo wamechukua na vijana wengine ambao walikua wapo katika band hiyo ya jeshi na kuweza kuanza kazi ya muziki ambapo kwa kujibu wa Rogert anasema band hiyo itakua inapiga miziki tofauti tofauti,


Akiongea ba blog hii Rogert hegga amesema lengo la kuanzishwa kwa band hiyo ni kurudisha enzi za band za serikali zilizokuwa zinaushindani mkubwa miaka ya nyuma na kupata watu wengi kwenye show zao ikiwa nia pamoja na kutoa upinzani katika nyimbo za radioni huku akitolea mfano wa band izo za zamani zilizokuwa zinaleta ushindani ni kama polisi jazz,mwenge jazz,magereza na nyinginezo wakati huo zikiwapa tabu oss,msondo,sikinde na nyinginezo na sasa mapngo wao ndio huo na ndio maana wameweza kuchukua wanamuziki wakongwe wanaoweza mikiki ya muziki wa dansi ili kuweza kuleta upinzani zaidi.
Rogert amezitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo tayari ni SPIRIT ambayo ni utunzi wake mwenyewe na pia wimbo mwingine ambao ni utunzi wa waziwa kalala na mwingine ukiwa ni utunzi wake Muhina panduka TOTO TUNDU na kusema bado nyimbo zingine tangu ambazo wanaziandaa na kukamilish album.

Tuesday, March 4, 2014

DEKULA KAHANGA 'VUMBI' APANIA KURUDISHA LADHA ZA MUZIKI WA DANSI ZILIZOPOTEA KATIKA KIZAZI KIPYA YUKO MBIONI KUACHIA ALBUM YAKE YA THE BEST OF DEKULA,ASEMA MEDIA NDIO ZILIKUZA MUZIKI WA TANZANIA NA NDIO ZINAZOKANDAMIZA MUZIKI HUO KWA SASA

Mwanamuziki wa siku nyingi ambae aliondoka nchini miaka ya 90 akitokea band ya Mrquis original baada ya kutoka congo na kuweza kufanya kazi kwa muda mchache na band waliyoianzisha ya CHAMWINO JAZZ na ndipo alipovutika na mariquis na kwenda kuomba kazi na kupokelewa na mfalme NGUZA MBANGU VIKING ambapo aliweza kufanya kazi kwa mafanikio ya hali ya juu huku akiacha kumbukumbu ya wimbo mkali kama NGALLULA na ndipo alipopata deal la kwenda kurekodi nchini uingereza lakini mwisho wa siku akweza kuangukia katika nchi ya sweeden ambapo awali walianzisha band iliyoitwa MAKONDE BAND ambayo waliweza kufanya nayo sehemu tofauti ikiwemo uganda lakini baadae aliweza kujitoa na kuweza kuanzisha band yake mwenyewe ambayo ameipa jina la dekula band ingawa wa afrika mashariki wengi waishio sweeden wanapenda kukuita kwa mzee VUMBI,katika kile alichosema kuwa muziki wa tanzania kuna ladha imepotea ikiwemo ya upigaji wa tarumbeta na kusema sasa anataka kutoa album ambayo itakua na ladha zote zilizokuwa zinapigwa katika muziki wa dansi wa nezihizo tanzania,


AIDHA dekula amezitumia lawama baadhi ya media kwa kuweza kuua muziki wa dansi wakati kipindi hca nyumba walikuwa wanasapport sana kwa nguvu hivyo ameomba media ziweze kurudisha airtime za muziki wa dansi kama ilivyokuwa zamani, na kusema kwa kufanya hivyo na wanamuziki wa sasa wakiwa wabunifu basi muziki wadansi utakua kazi tosha na kurudi katika kiwango cha zamani ambapo zamani hadi nchi za kenya na uganda  dansi ya swahili ilikuwa inatamba

Monday, March 3, 2014

MJUE TABU MAMBO SASA MCHEZA SHOW WA ENZI HIZO ALIEGEUKIA MIC NA KUWA MKALI WA MASAUTI SASA ANAPIGA NA BAND YA HOTELI LAKINI ASEMA YUKO MBIONI KUACHIA NYIMBO ZAKE MWENYEWE ASEMA MZIKI WA DANSI UNARUDI KWA KASI

TABU MAMBOSASA si jina geni katika ulimwengu wa muziki wa dansi kam mfatiliaji ila kwa wale ambao inawezekana hawafahamu kabisa TABU ni mcheza show wa zamani(DANCER) mwanzoni mwa kiaka ya 90 hadi mwishoni mwa miaka ya 2000 ambapo alipitia kama dancer katika band nyingi ikiwemo BANTU GROUP iliyokuwa ikiongoza na komando hamza kalala lakini pia Marqus orchestre ya lakini hata baadae kumalizia show zake akiwa na band ya DOUBLE M SOUND iliyokuwa ikiongozwa na PRINCE MUUMINI MWINJUMA kipindi hicho ambapo baada ya hapo ndio aliamua kugeuka katika uimbaji na mwisho wa siku akaweza kuwa na band ya hoteli lakini ambapo anafanya kazi hiyo mpaka sasa huku akisisitiza kuwa mziki wa hoteli una uhakika wa malipo kuliko mziki wa kupiga kutegema waingiaji na yote hii ni kutokana na mziki wa dansi kipindi cha kati kushuka kutokana na media kutoka ipa kipaumbele miziki ya aina hiyo,

                                                   TABU MAMBOSASA
Aidha kuhsu ya kwamba miziku ya copy kuwa vipaji amesema sio kweli inatokana na mwanamuziki mwenyewe jinsi utakavyojiweka ndio kipaji kitakufa na kwa kusisitiza kuwa kipaji kipo ndipo hata alipoonyesha uwezo kwenye wimbo wa cheza Kidansi ambapo ndani yake wameimba wanamuziki ngulli akiwemo NYOSHI EL SADAAT,KHALIDI CHOKORA,ALAIN MULUMBA,KABATANO,MUUMINI MWINJUMA na yeye ameweza kuweka sauti yake humo na kuonyesha uhalisia kuwa licha ya kupiga mziki wa hotl lakini na filing nje ya muziki wa copy zipo bado
Pia amesema kwa sasa yuko njiani kurekodi kazi zake mwenyewd ambazo zitamtambulisha rasmi kipaji chake ambapo amesema katika nyimbo zake hizo atawashirikisha wanamuziki mbalimbali wa dansi

Saturday, March 1, 2014

Interview That Kid Bill meets #Christine Michelle from #Merita movement!! Christine Michelle is a 28 year old philanthropist, hairdresser, sound, art and style enthusiast. Impartial to academia, she spent the greater part of her youth creating and experimenting with art, crafts and textiles. Many blessed opportunities to travel internationally imbedded the travel bug deep in her soul which eventually landed Christine in the “heart of Africa” a city called Goma on the East border of Democratic Republic of Congo. Since time, she has spent an accumulated 19 months on the ground and several years moving back and forth between Vancouver and DRC. Christine’s second visit to the continent of Africa was one in which forever changed her life and as a result, her creative interests (plus a love of scissors and sewing machines) provided her the opportunity to develop a program called Healing Arts. A fixed class room at the hospital in Goma as well as rural community outreach spaces where women who have experienced sexual violence come together joyfully and learn a variety of skills and trades to create opportunities and income for themselves while they are within their healing process. Promoting community and individual growth through holistic development or an ‘appreciative inquiry approach’. The link to the four minute video of our conversation done at the #BavubukaHeadQuartersDynasty

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...