WAY

Tuesday, March 11, 2014

BAADA YA KUIWEKA PEMBENI SUPER STARS BAND NA KUTUA KWA WANAJESHI WA RUVU STARS BAND WATAKA KURUDISHA ENZI ZA MABAND YA SERIKALI LAKINI NA USHINDANI KAMA ILIVYOKUWA ZAMANI MAGEREZA,POLIS JAZZ BAND KIMALUMALI NA NYINGINE WAACHIA TATU KWA MPIGO NI BAND INAYOUNDWA NA WANAMUZIKI WAZOEFU WA DANSI TANZANIA AKIWEMO ROGERT HEGGE CARTAPILA JE WATAWEZAA???

Band inayoundwa na wakongwe kama Rogert hegga( cartapila kilimanjaro),Amigolas,muhina panduka(toto tundu)khadija mnoga(kimobitel)waziwa kalala,jojoo jummane toka twanga pepeta,sele momba toka twanga pepeta,champion aliekuwa mpiga drums wa malaika band,victor mkambi(profesional keyboard)ambapo kati yao walikuwa wanaunda super star band ambayo ilianza kazi kadhaa lakini bila kurekodi na mwisho wa siku ndio wakaweza kuignia mkataba na jeshi na kwenda kama walimu wa band ya ruvu star band ambapo wamechukua na vijana wengine ambao walikua wapo katika band hiyo ya jeshi na kuweza kuanza kazi ya muziki ambapo kwa kujibu wa Rogert anasema band hiyo itakua inapiga miziki tofauti tofauti,


Akiongea ba blog hii Rogert hegga amesema lengo la kuanzishwa kwa band hiyo ni kurudisha enzi za band za serikali zilizokuwa zinaushindani mkubwa miaka ya nyuma na kupata watu wengi kwenye show zao ikiwa nia pamoja na kutoa upinzani katika nyimbo za radioni huku akitolea mfano wa band izo za zamani zilizokuwa zinaleta ushindani ni kama polisi jazz,mwenge jazz,magereza na nyinginezo wakati huo zikiwapa tabu oss,msondo,sikinde na nyinginezo na sasa mapngo wao ndio huo na ndio maana wameweza kuchukua wanamuziki wakongwe wanaoweza mikiki ya muziki wa dansi ili kuweza kuleta upinzani zaidi.
Rogert amezitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo tayari ni SPIRIT ambayo ni utunzi wake mwenyewe na pia wimbo mwingine ambao ni utunzi wa waziwa kalala na mwingine ukiwa ni utunzi wake Muhina panduka TOTO TUNDU na kusema bado nyimbo zingine tangu ambazo wanaziandaa na kukamilish album.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...