WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Wednesday, February 26, 2014

CHALZ BABA AJITAPA KUCHUKUA TENA TUZO TANO KWENYE KILI ASEMA USHAMBA MZIGO NA THAMANI YA MTU NI KAZI TOSHA KWA KUIBUKA KIDEDEA MWAKA HUU MBIONI KUKAMILISHA ALBUM NYINGINE AMBAYO WATAIZUNDUA KUANZIA MWEZI WA SABA

Rais wa mashujaa musica band amesema kwa mwa huu mfululizo watachukua tuzo tano tena kutoka kill music award kwa kuwa anaamini toka mwaka jana hakuna band iliyoweza kufanya vizuri zaidi yao tena na wameachia nyimbo mbili ikiwemo USHAMBA MZIGO pamoja na THAMANI YA MTU ambapo amesema nyimbo hizo mbili zinatosha kabisa kuweza kuwafanya kuwa vinara katika tuzo za kill award tanzania ambapo mwaka jana walichuku tuzo za BAND BORA YA MWAKA,WIMBO BORA WA DANSI,MUIMBAJI BORA WA KIUME,MTUNZI BORA WA MASHAIRI NA RAPA BORA WA BAND wote walitoka ndani ya mashujaa musica band hku akisemma na mwaka huu itakuna ni vile vile zaidi akiwaomba mashabiiki wao waendelee kuwapa sapoti kwa kuendelea kuwapigia kura.



                       CHALZ BABA KINGUNGE
Aidha CHALZ baba amesema wako katika maandalizi ya kumalizia kurekodo album yao ambapo nyimbo karibia zote ziko tayari kasoro kurekodi na kusema mpka ikifika mwezi wa saba watakuwa wameshakamilisha na itakua tayari kwa kufanya uzinduzi na kusema kuwa pia mwaka huu uzinduzi hautafanyika dar-es-salaam peke bali hata baadhi ya mikoa itaweza kushuhudia zinduzi za album hiyo ambayo haijapewa jina bado

Monday, February 24, 2014

VIJANA GWASUMA KUZINDUA TAR 28 BAADA YA WIMBO WAO WA WALE WALE KUJA NYINGINE KALI WASEMA JINA LA MATRIX MUSIC HALIKUSOUND VIZURI NDIO MAANA WAKAAMUA KUJIITA VIJANA GWASUMA!!!!

Ile band ya inayoundwa na vijana wengi waliojiengua kutoka band ya fm academia wazee wa ngwasuma na kuunda band ambayo waliita vijana ngwasuma ambayo inaundwa na wasanii waliotka fm academia kama vile BEN BIAVANGA,TOSCANE NZIMBU,CHEKDAR,PAPPY CATALOGY,KAMANYOLA na wengine ambao wameongeza katika kuweza kuipa nguvu band hiyo nakufanya kufika jumla ya wanamuziki 15 ambao ndio wanawasimamisha vijana ngwasuma,
Wakiwa tayari wameshachia wimbo wao wa WALE WALE sasa wako katika mpango wa uzinduzi utakaoenda kufanya mwishoni mwa mwezi huu wa pili ikiwa ni utambulisha rasmi wa band lakini baada ya hapo project nyingine za kurekodi nyimbo zinafanyika huku uzinduzi huo wakipewa shavu na bosi kubwa RUGE MUTAHABA


                      ME AND CHEK DAR

Akizungumza kwanini kwa mara ya kwanza walijiita matrix music na baadae sasa kuibukia kwenye jina la vijana ngwasuma mmoja wanamuziki wa band hiyo toscanee nzimbu amesema kuwa waliwasikiliza mashabiki na kupendekeza jina la vijana ngawasuma ndio jina ambalo litakua vizuri zaidi kwa kuwa wao wametoka kwenye band ya fm academia WAZEE WA NGWASUMA,

Friday, February 21, 2014

WAKIWA WANAELEKEA KWENYE UZINDUZI WA MTENDA AKITENDEWA KESHO ALLY CHOKI AFUNGUKA KUHUSU REDOCK MAUZO NA KABATANO ASEMA HAJAFANYA LOLOTE NDANI YA EXTRA BONGO NA HAWEZI KUWAZUNGUMZIA ASEMA NI WATU WASIOKUMBUKA FADHILA TAMAA ZA PESA ZA MARA MOJA NDIO ZIMEWAPONZA ASEMA SASA TIMU ALIYONAYO NDIO KIKOSI CHA MAANGAMIZI WATU WASUBIRI SUPRISE KWENYE UZINDUZI KAMA KAWAIDA YAKE

Mkurugenzi wa extra bongo nextlevel LE KAMARADE ALLY CHOKI MZEE WA KIJIKO IGWEE amefunguka kuhusiana na sakata la wanamuziki waliondoka kwenye band yake na kwenda kufanya show za nje bila ruhusa yake ingawa wao wanasema aliwaruhusu ila dakika za mwisho ndio akawakatalia kwanza kabisa choki alisema hawezi kuongea kuhusu kabatano kwa sababu hakuna kikubwa alichokifanya extra bongo kwa hivyo hata akiondioka hakuna kitakacho haribika ila amesema tamaa ndio imewapoza lakini pia wanasahau fadhila kwa sasa walikotoka katika band walioenda kuifanyia kazi walishwahi hata kutiwa ndani lakini ally choki ndio aliweza kuwasaidia na leo ndio wanaona sehemu nzuri ya kwenda kufanya kazi na pia ameongeza pia alishwapa taarifa toka awali kuwa wasiende katika hilo onyesho lakini mwisho wa siku waka kaidi amri yake na ndio mwisho wa siku akaamua aliyoaamua na ndipo alipofikiria kumchukua GREYSON SEMSEKWA kuweza kusaidiana nae katika sehemu za kurap na gery ni mmoja kati ya watu wa mwanzo sana ndani ya extra bongo.


Aidha ally choki amesema kuchelewa kwa uzinduzi huo kulitokana na kukamilisha viedo kwanza lakini na pia kutambua wanamuziki wa kweli ambao anaweza kufanya nao kazi kwa muda mrefu
Amezitaja nyimbo atakazokwenda kuzindua nazo kesho ni pamoja na MTENDA AKITENDEWA,WATU NA FALSAFA,BAKUTUKA,UFISADI WA MAPENZI,MAMA SHUU,NEEMA ambazo zilikuwa zimekamilika toka mwaka jana na pia amesema siku hiyo atasindikizwa na wasanii wengi akiwemo KHADIJA KOPA,AMINI,LINAH,MASHUJAA MUSICA band na itakua ndani ya ukumbi wa dar- live mbagala

BAADA YA KUKATAA BARUA YA KUOMBA MSAMAHA URUDI EXTRA BONGO REDOCK MAUZO AREJEA T.O.T ASEMA YALIYOPITA YAMEPITA SASA WANAANZA UPYA KUIZUNDUA BENDI RASMI BAADA YA MAONYESHO KADHAA YA CCM KATIKA BAADHI YA MIKOA ASEMA CHOKI ALIWAGEUKA DAKIKA ZA MWISHO

Aliekua mwanamuziki wa band ya extra bongo next level REDOCK MAUZO ambae yeye na mwenzake KABATANO waliweza kusimamishwa katika band hiyo baada ya kusemakana kuwa wamekiuka mkataba wao wa kufanya kazi nje ya band yao bila ruhusa ya kiongozi wa band amefunguka baada ya kumuuliza ilikuaje ameshindwa kuandika barua ya kuomba msamaha kama alivyoagizwa na mkurugenzi wake anasema mpka dakika za mwisho mkurugenzi huyo alikua amewaruhusu kwenda kufanya kazi na JOHN KOMBA lakini wakiwa wamekwisha chukua hela ya komba ndio siku chache tu kabla ya kwenda kufanya hiyo show ndipo choki alipowaambia wasiende katika maonyesho hayo lakini wenyewe kwa kuwawalikua wameshachukua pesa kutoka kwa boss huyo wa T.O.T ilibidi waende na ndipo waliporejea wakawa wameshongea na komba mwenyewe kuanzisha t.o.t mpya ambayo itakua inapiga hotel pamoja na kumbi zingine tofauti tofauti.pia redo aliongeza kuwa kila mwanamuziki anapenda maisha mazuri sasa kwa kuwa wameahidiana mambo mazuri na komba wameona bora waendelee na john komba katika kuanzisha band hiyo iliyokufa katika medani ya muziki.
                                                 REDOCK MAUZO
Redo amesema kwa sasa yuko katika mpango wa kukamilisha nyimbo yake lakini pia katika mpango wa kutafuta wanamuziki wengine ambao wataungana pamoja katika kuendeleza band hiyo amesema
Nilivyomuuliza kuhusu mikasa iliyowakuta wakati wapo T.O.T amesema kwa kuwa manegment imebadilika basi hawana budi kukubali kurudi hapo kwa kuwa watakuwa na maslah napo

Thursday, February 20, 2014

BAADA YA CHIMBO LA MUDA MREFU SASA ANCO VENA DIGITAL ALIEKUWA MWIMBAJI WA TWANGA PEPETA SASA AKABIDHIWA BAND NA JESHI LA POLISI IKIITWA SUPER KWATA INTERNATIONAL TAYARI WASHAKAMILISHA MBILI MBIONI KUITAMBULISHA RASMI

Aliekua  muimbaji kinara wa twanga pepeta ANCO VENA DIGITAL ambae alitoweka katika mazingira ya utata na hatimaye tukasikia kuwa yupo katika mafunzo ya jeshi la polisi sasa aibukia huko na kukabidhiwa band ya jeshi hilo mjini moshi ikiitwa SUPER KWATA INTERNATIONAL ambayo tayari wameshaanza kuingia studio na tayari wamekwisha kamilisha nyimbo mbili ambazo wataingia kurekodi moja ikiiwa DONT TRUST ANY ONE na nyingine ikiitwa JULIANA,


Akizungumzia ujio wake mpya amesema watu wasubiri mambo makubwa baada ya kukaa kimya muda mrefu huku wengine wakifikira kuwa maeacha muziki na kusema mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kwa sababu bendi ya super kwata itakua kama band nyingine za ushindani kwa kuweza kurekodi na kuingiza sokoni na kufanya show tofauti tofauti pia katika maeneo tofauti tofauti pia
huku akiongeza kuwa sasa wapo kambini kwa ajili ya kuweza kukamilisha album kabisa

Tuesday, February 18, 2014

ZAGREB BUTAMU SURA MVUTO WA AKUDO IMPACT AKAMILISHA ALBUM YAKE YA KIFUA MBELE ASEMA ATAZINDUA BAADA YA UZINDUZI WA ALBUM YAO YA AKUDO IMPACT KAA TAYARI

Mwanamuziki wa muda mrefu wa akudo impact ameweza kuibuka na kusema amewisha kamilisha ablum yake binafsi nje ya akudo impact ambayo kwa amesema kwa juhudi zake binafsindio maana amechukua muda kuitoa album hiyo na kusema tayari nyimbo sita zimekwisha kamilika huku akiendelea kuzifanyia video ili aweze kuanza kuzisambaza katika vituo mbalimbali vya televishen na kuahidi pia ataweza kuanza kufanya tour ambazo atatambulisha album yake hiyo ambayo ameipa jina la KIFUA MBELE huku akisema humumo ndani amechanganya ladha tofauti tofauti kiasi ambacho mtu yoyote hawezi kuichoka haraka kwa ladha zitakazokuwemo ndani yake,

                              ZAGREB BUTAM AND ME

Aidha Zagreb amesema kuwa kufanya kwake kazi kama solo artist haimanishi kuwa anaweza kutoka akudo impact ila amepta ruhusa na baraka za band yake kuweza kufanya hivyo kwa hiyo yeye ataendelea kubaki na band yke ya akudo siku zote mpaka hapo atakapoamua vingine lakini sio kwa sababu ya kutengeneza album yake nje ya kundi hilo ambalo hivi karibuni lilifnya makubwa katika show ya no bif ambayo ilifanyika siku ya valentine day

WASANII nchini wametakiwa kujiunga katika mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma –PSPF-ili waweze kujiwekea akiba kwa maaisha yao ya baadae.

2

WASANII nchini wametakiwa  kujiunga  katika  mfuko wa  pesheni  kwa watumishi wa  umma –PSPF-ili  waweze  kujiwekea  akiba kwa maaisha  yao  ya  baadae.

Hayo  yamesemwa leo  jijini Dar es Salaam na  Meneja  msaidizi  mpango  wa uchangiaji wa hiari –PSPF-Matilda  Nyallu wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa  habari  kuhusiana na  semina  ya wasanii  hao  inayotarajiwa  kufanyika  februari 21  mwaka  huu.

Matilda  amesema kuwa   katika  semina hivyo  ambayo  wataitoa kwa wasanii   inalengo la  kuwashawishi  kujiwekea  akiba  ambayo  itamsaidia  kwa baadae kwa sababu  asilimia kubwa ya wasanii  hawana  akiba ya  baadae.

Amesema kuwa  kabla  ya  kuwashawishi kujiunga  na mfuko huo  watatoa  elimu   ili  waweze kuelewa   kwa  undani umuhimu wa  kujiwekea akiba.

Kwa  upande  wake  Mwenyekiti wa  bongo  movie Stivu  Nyerere  amesema kuwa kinachotakiwa  wasanii wajitambue pamoja na  kuitaka  serikali iweke  sheria  kali  kwa  watu  wanaoiba  kazi  za wasanii kwa sababu   wanachangia kurudisha  nyuma  maendeleo  ya  wasanii.

Aidha  amewataka wasanii  wa hapa  nchini  waungane kwa  pamoja na  kupinga  hatua  ya  kuuza hati miliki  ya kazi  zao kwa  sababu  zinachangia kwa  asilimia kubwa  kukosa haki zao za msingi  za  kazi  wanazofanya

KAMATI kuu ya chama cha mpainduzi - CCM –imewapa onyo kali viongozi sita wa chama hicho kufuatia kubainika na tuhuma mbalimbali zikiwemo za kukiuka maadili ndani na nje ya chama hicho.



KAMATI   kuu  ya chama  cha mpainduzi - CCM –imewapa  onyo  kali    viongozi  sita wa  chama  hicho  kufuatia kubainika na tuhuma  mbalimbali  zikiwemo za   kukiuka  maadili   ndani na nje ya  chama hicho.

Hatua hiyo  imekuja baada ya kamati hiyo  kukutana  na viongozi hao na kuwahoji juu ya tuhuma hizo  na baada ya kuhojiwa  walibainika kuwa tuhuma hizo ni za kweli.

Hayo  yamebainishwa  leo  jijini  Dar es Salaam  na  Katibu  wa  halmashauri  kuu  ya taifa ,  itikadi  na uenezi  Nape  Nnauye wakati alipokuwa  akizungumza na waandishi wa  habari  kuhusiana   vikao  vya pamoja vilivyofikiwa  na kamati  kuu,   tume ya  udhibiti  na nidhamu na  kamati  ndogo ya udhibiti.

Amesema  kuwa  kwa mujibu wa kanuni za uongozi  na maadili  za CCM  toleo la  februari  2010 ibara  ya nane na  kuongeza  kuwa  tuhuma hizo  zilizobainika zinaukweli  ndani yake  hivyo  kupelekea  mapendekezo  hayo  kwenye  tume  ya udhibiti  na nidhau.
Amewata  viongozi hao  waliopewa  onyo  kuwa  ni Fredick Sumaye, Edward Lowassa, Stephano Wasira,  Benard  Membe , Januari  Makamba na Wiliam  Ngeleja.

Aidha   ameyataja  makosa  yao  kuwani ni  kuthibitika  kuanza  kampeni  za kuteuliwa   kugombea nafasi ya urais kabla  vya  wakati wake jambo   ambalo  ni kinyume  na kanuni  za uongozi  n  maadili  za  chama  hivho.

 18-FEBR-NAPE NNAUYE
Pia  amesema kuwa  mwanachama  aliyepewa  adhabu  ya onyo kali  atakuwa  katika  hali  ya  kuchunguzwa  kwa muda  wa  usiopungua  miezi  12  ili  kumsaidia  katika jitihada  za kujirekebisha.


Thursday, February 6, 2014

AKUDO IMPACT KUTAMBULISHA WANAMUZIKI KUMI WAPYA SIKU YA ONYESHO LAO LA NO BIF TUPENDANEWAKIWEMO WANNE WALIOTOKA MALAIKA BAND SASA KUANDAA ALBUM NYINGINE BAADA ILE YA HISTORIA NO CHANGE AMBAYO WASANII WENGI HAWAPO TARSIS ASEMA HAWAWEZI KUTAMBULISHA NYIMBO WAKATI NYINGINE HATA WALIOIMBA HAWAPO ASEMA MWAKA HUU NI KUWASHA MOTO WANAANZA NA NO BIF TUPENDANE NA MAPACHA

Akiongea na blog hii kiongozi na rais wa Akudo impact  TARSIS MASELA JOTO ambae alikuwa akizungumzia show yao ya tar 14 na mapacha watatu walioipa jina la NO BIF TUPENDANE amesema siku hiyo watatambulisha wanamuziki kumi wapya wakiwemo waliachishwa malaika band na kusema kuwa walienda kuomba kazi kwao na wamewachukua kwa kuwa ni wafanyakazi wazuri na wanaweza kuifanya akudo kuwa mpya kabisa akizungumzia wanamuziki hao kuwa ni FADY DIPIRONE,DADY DIPIRONE,COCO NGEMBA. na wengine watakao watambulisha ni sauti ya ng'ombe ambae ametokea morogoro,na wanamuziki engine ambao wamewachukua kutoka congo
Tarsisi amesema wameamua kuimarisha band yao na sasa wapo katika harakati ya kuweza kurekodi na wanamuzikik hao ili kuweza kutengeneza album nyingine baada ya ile ya kwanza wanamuziki wengi walifanya baadani ya nyimbo kuwa hawapo kama vile CRISTIAN BELLA,TOTOO ZE BINGWA,ANDREA SEKEDIA ambao ndio wameunda MALAIKA BAND,KANAL TOP ambae yupo nje ya nchi kwa shughuli zake binafsi sasa  tarsis amesema kwa wanamuziki watakao watambulisha siku hiyo ndio wanatarji kutengeneza album nyingine ambapo tayari wameshatengeneza wimbo wa penzi lako linazidi asali



                       CHOKORAA,TARSIS,JOSE MARA
 lakini tarsis amesema kuwa siku ya show hiyo pia watatambulisha wimbo wao mwingine unaitwa watu
NA amesema wameamua kufanya na mapacha watatu kwa sababu ni kweli no bif na sio kwamba wanabif na band nyingine ila ni kutokana na ratiba za band nyinginee kwa siku hiyo na kwa kuwa wanapiga uwanja wa nyumbani wa mapacha ambao wanapiga kila ijumaa

Wednesday, February 5, 2014

BAADA YA KUFANYA WIMBO AMBAO HAUKUFANYA VIZURI KAMA WALIVYOTARAJIA SASA SKYLIGHT BAND KUURIDOA WIMBO WA KARIAKOOO NA SASA VIDEO YA WIMBO HUO IPO KATIKA HATU ZA MWISHO KUTOKA BAADA YA ULE WA KWANZA KUWA NA KASORO KATIKA USIKUVU NI AFRO POP YENYE SEBENE KALI

Akiongea na blog hii kiongozi wa band ya skylight Aneth kushaba amesema wako katika hatua za mwisho za kukamilisha marudio ya wimbo wa kariakoo ambao waliutoa mwaka jana  lakini haukufanya vizuri sokoni kutokana na mixing zake kuwa mbovu lakini pia kuwana promo ndogo katika media sasa wameama kushirikiana na mameneja wa wanamuziki wa kizazi kipya kama BABU TALE ili kuweza kutanua soko lao la muiki wa live band tofauti na band zingine
Akizungumzia mpka sasa ulipofikia wimbo huo amesema wamekwishakamilisha video na ogopa djs na kilichobaki ni final touch na kuuachia kwa mara nyingine lakini pia amesema mtindo walioufanya katika marudio ya wimbo huo ni katika style za kiafrica zaidi na kuchezeka zaidi lakini waimbaji wataimba vile vile na joniko ataweka mbwembwe zake vile vile ila kwa sasa wanakuwa wamepiga kisasa zaidi


                      WANA SKYLIGHT BAND
Aidha amesema mipango mingine ya band mwaka huu ni kuachia wimbo walau tatu na baada ya hapo waweze kuachia album sokoni lakini pia kujiweka sehemu nzuri katika soko la muziki wa livena kusema kwa sasa wanataka kutoa ile dhana iliyojengeka kwa baadhi ya watu kuwa skyligt band ni band yavijana wa kishua peke yake

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...