KAMATI kuu ya
chama cha mpainduzi - CCM –imewapa onyo
kali viongozi sita wa chama hicho
kufuatia kubainika na tuhuma mbalimbali zikiwemo za
kukiuka maadili ndani na nje ya chama hicho.
Hatua hiyo imekuja baada ya
kamati hiyo kukutana na viongozi hao na kuwahoji juu ya tuhuma
hizo na baada ya kuhojiwa walibainika kuwa tuhuma hizo ni za kweli.
Hayo yamebainishwa
leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa
halmashauri kuu ya taifa , itikadi na uenezi
Nape Nnauye wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari kuhusiana vikao vya pamoja vilivyofikiwa
na kamati kuu, tume ya udhibiti na nidhamu
na kamati ndogo ya udhibiti.
Amesema kuwa kwa mujibu
wa kanuni za uongozi na maadili za CCM toleo la februari
2010 ibara ya nane na kuongeza kuwa tuhuma hizo
zilizobainika zinaukweli ndani yake hivyo kupelekea
mapendekezo hayo kwenye tume ya udhibiti na
nidhau.
Amewata viongozi hao
waliopewa onyo kuwa ni Fredick Sumaye, Edward Lowassa, Stephano
Wasira, Benard Membe , Januari Makamba na Wiliam
Ngeleja.
Aidha ameyataja
makosa yao kuwani ni kuthibitika kuanza
kampeni za kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kabla
vya wakati wake jambo ambalo ni kinyume na kanuni
za uongozi n maadili za chama hivho.
18-FEBR-NAPE NNAUYE
Pia amesema kuwa
mwanachama aliyepewa adhabu ya onyo kali atakuwa
katika hali ya kuchunguzwa kwa muda wa
usiopungua miezi 12 ili kumsaidia katika jitihada
za kujirekebisha.
0 comments:
Post a Comment