WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Monday, March 30, 2015

MUGABE AWATAKA VIONGZI WA AFRIKA KUACHA KUWA VIBARAKA WA MATAIFA YA ULAYA NA MAGHARIBI NA WAJISHUGHULISHE KUINUA WANANCHI WAO



     Rais wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe
Rais wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe amewataka viongozi wa nchi za Africa kukataa kuwa vibaraka wa mataifa tajiri duniani na badala yake wajitoe katika kuwatumikia waafrika ili kufikia mafanikio ya kimaendeleo katika ustawi wa bara hili.

Rais Mugabe ametoa mwito huo wakati akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa viongozi Vijana kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika na China unaofanyika katika ukumbi wa mikotano wa Ngurdoto nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo Rais Mugabe ametumia muda mwingi kuwaasa na kutoa mwito kwa viongozi hao vijana akisistiza kuwa Bara la Afrika linategemea mchango wa Fikra zinazojali uwajibikaji na nidhamu ya hali ya juu katika utumishi.

Awali akizungumza katika Mkutano huo,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Kikwete ameonyesha imani aliyoanayo kupitia mkutano wa viongozi vijana kutoka Afrika na Uchina kwamba utatoa fursa ya kutoka na maazimio yatakayokuwa na tija kwa mustakabali wa watu wote

Tuesday, March 24, 2015

SERIKALI KUTUNGA CHOMBO CHA KUCHUNGUZA, KUPEKUA NA KUKAMATA WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA


            Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh. Jenista Mhagama
Serikali leo imewasilisha mswada wa sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za Kulevya ya mwaka 2014, kutokana na tatizo hilo kuongezeka zaidi kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kutishia uhai wa taifa kutokana na vijana wengi kujiingiza katika biashara na matumizi ya dawa hizo.

Akiwasilisha mswada huo Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh. Jenista Mhagama amesema matumizi ya dawa za kulevya yameongezeka ambapo takwimu zinaonyesha kuwa watumiaji wa dawa hizo kati ya laki mbili na 20 hadi laki nne na 20 hapa nchini wengi wakiwa ni vijana kati ya miaka 15 hadi 38.

Mh. Mhagama amesema ili kurekebisha matatizo ya kimfumo katika udhibiti ya dawa hizo serikali imekusudia kuanzisha chombo kinachojitegemea chenye mamlaka ya kiutendaji ya kuchunguza, kupekua na kukamata watuhumiwa tofauti na ilivyo tume kwa sasa.

Friday, March 6, 2015

WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUWAUA WATU WATANO KWA KUWATUHUMU WACHAWI


     Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, Philip Kalangi akizungumza na wanahabari
Jeshi la polisi mkoa wa mara limewakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili wa serikali ya kijij cha park nyigoti katika kata ya ikoma wilayani serengeti mkoani mara baada ya kutuhumiwa kuwakamata na kuwafunga vitambaa usoni watu wanane wanaowatuhumu kwa uchawi kisha kuwachapa viboko na kusababisha vifo vya watu watano.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mara,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Acp Ernest Kimola,amesema katika tukio hilo ambalo limesababisha watu wengine watatu kujeruhiwa kwa kuchapwa viboko hivyo na kulazwa katika hospitali teule ya nyerere ddh mjini mugumu wilayani serengeti.

Mbali na mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya kijiji hicho kukamatwa pia viongozi wawili wa jadi wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo

nao baadhi ya ndugu wa marehemu wameelezea jinsi unyama huo ulivyotekelezwa kwa kisingizio cha ushirikinai

hadi sasa askari wa jeshi la polisi kutoka makao makuu ya mkoa wa mara kwa kushirina na polisi mjini wilayani serengeti wanaendesha na operesheni kali katika kuwasaka watu wote walihusika kufanya mauaji hayo ya kinyama.

Tuesday, March 3, 2015

VIKONGWE WAUAWA MKOANI DODOMA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA ETI WANAZUIA MVUA ISINYESHE MAENEO YAO


     Kamanda wa Jeshi la Polisi Dodoma David Misime
Vikongwe watatu akiwemo mganga wa kienyeji Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma, wameuawa kwa tuhuma za kuzuia mvua isinyeshe Wilayani humo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kamanda wa polisi mkoa wa Dodma, David Misime inasema kuwa tukio la kwanza lilitokea Machi mosi mwaka huu majira ya saa saba usiku katika kitongoji cha Golani, kijiji cha Masinyeti, kata ya Iduo, tarafa ya Mlali.

Kamanda amesema katika tukio hilo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Saidia Chakutwanga (80) ambaye ni mganga wa kienyeji aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kutobolewa macho.

Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina wakimtuhumu marehemu kuwa anazuia mvua kunyesha katika eneo hilo.

Katika tukio lingine amesema tarehe hiyo hiyo majira ya saa nane usiku kwenye kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda Kata na Tarafa ya Mlali mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Peter Kaluli (85) akiwa na mkewe aitwaye Kaila Kaluli (80) wakazi wa kitongoji cha Majengo wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao ya tembe, waliuawa na watu wasiofahamika kwa kuangushiwa ukuta wa nyumba yao kisha kuchoma moto na kubomoa nyumba mbili za tembe.

“Watu hao walifanya uharibifu mwingine kwa kuwaua nguruwe mmoja na ng’ombe mmoja kumkata miguu ambao ni mali za marehemu hao,” alisema Misime.

Kwa mujibu wa Kmanda uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji na uharibifu huo ni imani za kishirikina wakiwatuhumu marehemu kuwa wanazuia mvua kunyesha.

Kutokana na tukio hilo watu wanne akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihanda na wazee wawili wa kimila wa kijiji wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo kwani taarifa zinaonyesha waliandaa vikao vya kutekeleza mauaji hayo.

Upelelezi wa matukio yote mawili unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika na matukio haya ili sheri aiweze kuchukua mkondo wake.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa amewataka viongozi wa dini mkoani hapa kuhubiri amani kwa waumini wao ili vitendo vya mauaji kwa vikongwe viweze kukomeshwa.

Monday, March 2, 2015

HATUA KALI ZINAFUATA JUU YA WAUAJI WA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI TAYARI ADHABU YA KIFO ISHATOLEWA KWA BAADHI YAO-KIKWETE


         Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikweteamesema kuwa Serikali haitafumbia macho suala la mauaji ya walemavu wa ngozi kama hali ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.

Akiongea katika Hotuba yake kwa wananchi kwa kila mwisho wa mwezi Rais Kikwete amesema kuwa matukio hayo ambayo yaliibuka mwaka 2006 Serikali iliweza kukabiliana nayo na mpaka kufikiwa mwaka 2011 kukawa hakuna tukio lolote la mauaji ya watu hao.

Aidha rais Kikwete ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwafichua watu wote wanajihusisha na biashara ya viungo vya watu wenye Albinsim ili kwa pamoja kukomesha mauaji ya watu hao.

Kikwete amesema ni ujinga uliokithiri kwa mtu kutegemea ushirikina hasa kuwa na viungo vya ulemavu wa ngozi ndio kuna kufanya mafanikio katika shughuli zao hivyo kutaka juhudi zifanyike kueleimisha juu ya kuacha watu kuamini imani potofu.

Aidha Rais Kikwete amesema atakuata na watu wenye Ulemavu wa ngozi wiki ijayo ili kusikiliza maoni yao juu ya nini kifanyike katika kusaidiana kukomesha mauaji dhidi yao.

Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete amesema kazi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchini kwa kutumia mfumo wa BVR katika Halmshauri ya Makambako mkoani Njombe imevuka lengo la tume hivyo kulazimu kuongeza muda ili wananchi wote waliojitokeza waweze kujiandikisha.

Tume ilitegemea kuandikisha wapiga kura 9541 katika halamashauri hiyo lakini kutokana na mwitikio wa wananchi wameandikishwa watu 13.042.

Aidha Rais Kikwete amewataka viongozi wa vyama vya siasa,Serikali,dini na asasi za kiraia kuungana na tume katika kuwahamasisha wananchi kujiandikisha badala ya kuwachanganya kwa kutoa taarifa zisizo za kweli.

ETI TANESCO WAMESEMA WATALETA MFUMO MWINGINE WA KUNUNUA LUKU BAADA YA TATIZO LA MITANDAO KUKOSA NETWORK YA KUNUNUA UMEME

Meneja Mawasiliano wa Tanesco Adrian Mvungi
Wakazi na wajasiriamali wa jiji la Dar es salaam wamelilalamikia Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanesco baada ya Mtandao wa kuuza umeme kwa njia ya Luku kugoma kufanya kazi toka juzi usiku,

Wakizungumzana kutoka makao makuu ya Tanesco Ubungo jijini Dar es salam huku wakiwa na jazba wamesema biashara zao zimehathirika sana na kuwa sababishia hasara kutokana na kushindwa kununua Umeme kwa njia ya Luku huku biashara zao zikitegemea umeme wakati wote,

Kwa Upande wake Meneja mwandamizi Teknolojia ya Habari na mawasiliano wa Tanesco Kusenha A. mazengo amesema wamelifanyia kazi tatizo hilo na kuhaidi hivi karibuni wataleta mfumo mpya wenye njia mbadala wa kununua Umeme,

Wakati huo huo Meneja Mawasiliano wa Tanesco Adrian Mvungi amewaomba radhi wateja wao kwa usumbufu walioupata na kuhaidi kutorudia tena.

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...