Wakazi na wajasiriamali wa jiji la Dar
es salaam wamelilalamikia Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanesco
baada ya Mtandao wa kuuza umeme kwa njia ya Luku kugoma kufanya kazi
toka juzi usiku,
Wakizungumzana kutoka makao makuu ya
Tanesco Ubungo jijini Dar es salam huku wakiwa na jazba wamesema
biashara zao zimehathirika sana na kuwa sababishia hasara kutokana na
kushindwa kununua Umeme kwa njia ya Luku huku biashara zao
zikitegemea umeme wakati wote,
Kwa Upande wake Meneja mwandamizi
Teknolojia ya Habari na mawasiliano wa Tanesco Kusenha A. mazengo
amesema wamelifanyia kazi tatizo hilo na kuhaidi hivi karibuni
wataleta mfumo mpya wenye njia mbadala wa kununua Umeme,
Wakati huo huo Meneja Mawasiliano wa
Tanesco Adrian Mvungi amewaomba radhi wateja wao kwa usumbufu
walioupata na kuhaidi kutorudia tena.
0 comments:
Post a Comment