Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, Philip Kalangi akizungumza na wanahabari
Jeshi la polisi mkoa wa mara
limewakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili wa serikali
ya kijij cha park nyigoti katika kata ya ikoma wilayani
serengeti mkoani mara baada ya kutuhumiwa kuwakamata na
kuwafunga vitambaa usoni watu wanane wanaowatuhumu kwa uchawi
kisha kuwachapa viboko na kusababisha vifo vya watu watano.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa
mara,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Acp Ernest Kimola,amesema katika tukio hilo ambalo limesababisha watu
wengine watatu kujeruhiwa kwa kuchapwa viboko hivyo na
kulazwa katika hospitali teule ya nyerere ddh mjini mugumu
wilayani serengeti.
Mbali na mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya
kijiji hicho kukamatwa pia viongozi wawili wa jadi
wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo
nao baadhi ya ndugu wa marehemu
wameelezea jinsi unyama huo ulivyotekelezwa kwa kisingizio cha
ushirikinai
hadi sasa askari wa jeshi la
polisi kutoka makao makuu ya mkoa wa mara kwa kushirina na
polisi mjini wilayani serengeti wanaendesha na operesheni
kali katika kuwasaka watu wote walihusika kufanya mauaji
hayo ya kinyama.
0 comments:
Post a Comment