WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Wednesday, October 31, 2012

SAJUKI AFADHALI SASA NA KUTOA SHUKURAN KWA SINGO moja kali sana get ready!!



Ni kitambo sasa  tangu kuwepo kwa taarifa kuwa staa wa Bongo Movie, Juma Kilowoko, 'Sajuki' ni mgonjwa , huku pia taarifa za karibuni zikidai kuwa  hali ya  nyota huyo  bado ni tete na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wake.

Taarifa rasmi ni kuwa hali nyota huyo kwa sasa  ni njema na  yuko tayari tena  kuanza kuwatumikia  watanzania  kupitia tasnia ya  filamu.


Kwenye Exclusive interview aliyofanya na teentz.com mapema leo Sajuki amewashukuru watanzania  kwa kuwa pamoja nae kwenye wakati wote wa  matatizo  mpaka sasa  anajisikia yuko vizuri tofauti na ilivyokuwa awali.

Nashukuru kuwa  sasa niko poa, watanzania  waelewe hilo, kwa sasa  naweza hata kuendesha gari na karibuni nitaanza  kucheza muvi tena  alisema Sajuki.

Katika kuonyesha kuwa anathamini mchango wa Watanzania Sajuki ameachia ngoma ambayo ameamua kuipa jina la Shukurani

Tuesday, October 30, 2012

JACKLINE PENTEZEL a.k.a JACK MABANGO a.k.a JACK MABANGO :ASEMA KWA KIWANGO CHAKE SASA NA JINSI SANAA INAVYOKWENDA KWA SASA BILA MILIONI SITA SICHEZI FILAMU.



Kama ni mpenzi  wa kucheki filamu za Kibongo, haina shaka utakuwa unaifahamu orodha ndefu ya mastaa wa kike wanaofanya vizuri kwenye tasnia  hiyo.

Kwenye exclusive interview aliyofanya mwishoni mwa wiki iliyopita staa wa Jumba la Dhahabu, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuzi’, amefunguka kuwa sasa anajihisi milionea kufutia mshiko hevi anaoingiza kwa mwaka kupitia  uigizaji.





Jack wa Chuzi ‘super star’ wa muvi asiyekaukiwa matukio ameiarifu media kuwa sasa anauhakika wa kuingiza kiasi cha shilingi za kibongo milioni 18 kwa mwezi  kupitia malipo ya shilingi milioni 6 kwa kila muvi anayoigiza.


“Kwa sasa mtu akija na kazi yake sichezi chini ya shilingi milioni 6, ni kiwango ambacho ninaamini kiko kwenye hadhi yangu, ninafuraha kwa sababu sasa najihisi milionea”  alisema Jack wa Chuz.

Monday, October 29, 2012

SNURA MUSHI ASEMA MAGAZETI YALIMZUSHIA KUANDAA MOVIES AMBAYO YEYE HAKUIONGELEA ,AWACHANA WANAOVAMIA FANI SIO WOTE WANAOFANYA MUZIKI WANAWEZA KUFANYA FILAMU NA SIO WOTE WANAFANYA FILAMU WANAWEZA KUFANYA MUZIKI,KWA HIYO WAACHE TAMAA

SNURA MUSHI sio jina geni masikioni au midomoni ai machoni mwa watu ni msanii aliewahi kutamba sana ndani ya jumba la dhahabu na sasa anatikisa katika ulimwengu wa muziki ambapo hivi karibuni nilipoongea nae kuhusiana na movie ambayo ilikua ikiongeleak sana kwa vyombo vya habari ambayo kwa juju juju ilijulikana kama UCHAFU WA MASTAR WA BONGO

                                                     SNURA NA WEMA
na kusema kuwa yeye alikua hajaanda movie kama hiyo ila magazeti kama kawaida yao ya uzushi na kusema kuwa tumemtafuta hakupatikana ndio walioanzisha kuandika story ya movie hiyo ambayo kwa mujibu wa snura amesema kwa amesimama kufanya movie hiyo na kiufupi tu kwa amesiama kucheza movies zake na atakua nashiriki tu kwenye movies tofauti tofauti.
AIDHA SNURA akiongelea game ya filamu amesmea kwa sasa kuna watu wachache ambao wnalipualipua kazi na mwisho wa siku tasnia ya filamu inaonekana ya watu fulani na movies wanazozitengeneza zinakua hazzzina  mashiko.
                                                    SNURA MZIGONI
KWA sasa SNURA anaetambana kibao chake cha SHOGA YAKE MAMA akiwa amemshirikisha WEMA SEPETU amesema wapo watu ambao wana tamaa ya kuvamia fani means mtu akijiona anatamba kwemye movies basi atataka na kuingia kwenye muziki wakati hana uwezo wa kuuimba na wengine wanatamba kwenye muziki wanaingia kwenye filamu wakati hawana uwezo ila wanaforce tu!
                                     MABEST HAO SNURA,WEMA,JACK WOLPER

Thursday, October 25, 2012

AFRICAN SANAA GROUP WAPANIA KUIKOMBOA KUSINI KATIKA TASNIA YA FILAMU WAANDAA MOVIES YAO IITWAYO MADUVALA HATA MIKOANI SANAA IPO SIO TU KUSINI

KIKUNDI cha sanaa za maigizo,ngoma za asili,sarakasi kutoka mkoani mtwara AFRICA SANAA GROUP limepania kuikomboa kusini katika upande wa uigizaji babada ya kuandaa movie zao mbili moja ikiwa haikufanya vizuri sana sasa waja na MADUVALA ambayo wanasema inakuja kuteka soko kabisa na kuweza kuweka wazi kuwa sanaa sio dar-tu hata mikoani inapatikana  na inafanya vizuri pia
                                          AFRICA SANAA GROUP
Nikiongea na kiongozi wa kikundi hicho MOHAMED FUNDI a.k.a BARAKA amesema lengo la kuweza kutengenezea filamu zao huku huku kusini ni kutaka kuweza kuitangaza kusuni na watu kujua mikoa ya kusini hususani mtwara kuan tamaduni nyingi sana ambazo zinaweza kufanya story nzuri kabisa na za kuweza kuuzika sokoni ingawa amekuri kuwa kuna changamoto nyingi zinawakabili ikwamo rasimali pesa ili kuweza kufaniskisha kazi nyingine kwa haraka
 Kwa mujibu wa kiongozi huyo wamesema hivi karibuni watazindua filamu yao wa MADUVALA ambayo wataifanya kama preview ambapo wadau watapa kuiona kwanza kabla ya kuipeleka sokoni.

Wednesday, October 24, 2012

COLETA AIKUNGUKA KUHUSIANA NA ISHU ZA SKENDO ZA BONGO FILAMU

COLETA RYMOND ASEMA ANATAMASNI KUWASAIDIA UNDERGROUND WA FILAMU

Tuesday, October 23, 2012

ALLY CHOKI ALIA NA MEDIA KUUA SOKO LA MUZIKI WA DANSI ASEMA RADIO ZENGINE ZIMEAMUA KUVUNJA KABISA VIPINDI VYAO VYA MZIKI WA KIAFRICA. KUFANYA SHOW NNE MIKOA YA KUSINI

MKURUGENZI NA MUIMBAJI WA EXTRA BONGO NEXT LEVEL le KAMARADE ALLY CHOKI amesema kuwa media ndizo zinazochangia soko la muziki wa dansi kufa baada ya kuzipa kipaumbele nyimbo za mbele na bongo flever na kusahau muziki wa asili wa dansi na hivyo kufanya hata kutoa album wanakua wanasuasua kutokana na kukosa promo ya kazi zao kwenye radio au tv na hivyo kutegemea show zaidi ambazo wanapiga mikoani na kuweza kupata kipato kuliko mauzo ya album ambayo anasema kwa sasa yameshuka sana kusema zamani radio ilikua moja tu tena tanzania lakini bado nyimbo za nymbani kama msondo sikinde kina marijani walikua wanasika lakini kwa sasa radio ni nyingi lakini mzimki ndio haupewi kipaumbele kabisa.
Wakati huo huo extra bongo wanatarajia kufanya maonyesho kariobu manne kusini mwa tanzania katika mkoa wa lindi na mtwara ambapo wataanzia kilwa,ruangwa,masasi na kumalizia lindi mjini siku ya jumamosi na baadae mwezi wa kumi na mbili extra bongo wataenda kufanya birthday ndio siku ambayo watakwenda kuuza cd za albium yao mpya
                                    ROGERT HEGGA,BANZA STONE,ALLY CHOKI

Monday, October 22, 2012

TUESDAY KIHANGALA .a.k.a MR CHUZI ASEMA WATANZANIA NDIO WANACHANGIA SOKO LA FILAMU KUWA LA WASANII WA AINA MOJA KUTOKANA NA KWENDA KUULIZA FILAMU KACHEZA NANI SIO MTUNZI NI NANI KWA HIYO WANAFATA WASANII SIO STORY,AACHIA RASMI SIRIES ZAJUMBA LA DHAHABU,RED APPLE IPO NJIANI

Msanii anemiliki kampuni ya kusambaza kazi zake na ku ndi la wasanii la tuesaday intertaiment amefunguka na kuweka wazi kuwa watanzania wengi hawaangalia story pindipo wanapoenda kununua filamu za kibongo na mwisho wa siku wanaenda kuuliza nia nani ka act na hivyo ma underground kukosa nafasi ya kuweza kuwavinara kutokana na tayari watanzania wana vinara wao ambao wanataka kuwaona wakicheza katika kila filamu hivi kufanya biashara ya filamu kuegemea upande mmoja kwa wale wanovuma tu.

                                                     MR.CHUZI
AIDHA MR CHUZI amesema kwa sasa ameamua kutoa tamthilia ya JUMBA LA DHAHABU katika mtindo wa siries kutoka na wadau wengi kuomba tamthilia hivyo lakini pia akiwa ni msanii wa kwanza kutengeneza siries tanzania ambazo zitakua zinapatika katika episode tofauti tofauti ambazo tayari JUMBA LA DHAHABU SEASON ONE EPISOD 1-8 kwa sasa ipo madukani.

MBALI  NA JUMBA LA DHAHABU pia yuko mbioni kuikamilisha siries nyingine ya RED APPLE lakini hayo yakiendelea pia kwa sasa ameshawakusanya wasanii wake wote wa TUESDAY FILM PRODUCTION kwa ajili ya kuigiza siries nyin gine ambayo amesema itakua moto zaidi na ambayo pia itaonyeshswa kwenye television ya taifa TBC ambayo itakwenda kwa jina la HIGH HILLS.
PIA MR CHUZI kutoka kwenye production yake ameachia movies moja kali ambayo inakwenda kwa jina MKALI MO ambapo ndani yake amemshirikisha gwiji wa uigizaji tanzania MZEE MAJUTO
Wakati MKALO MO ikiwa sokoni lakni vile vile kwa sasa anaanda filamu ambayo bajeti yake ni kubwa sana iliyochezwa kwenye mazingira ya baharini sana movies hiyo ikiitwa DIRTY GAME ambayo anasema itakuna ni kiboko kwatika action film kwa sababu ina michezo ya hatari sana
NDANI YA DIRTY GAME


Saturday, October 20, 2012

LICHA YA KUONDOKA TWANGA LAKINI KWA KUONYESHA UPENDO KHALID CHOKORAA, AISHA MADINDA, ALLY AKIDA NA LILLIAN INTERNET WAAHIDI KUSHIRIKI TWANGA FACEBOOK FANS PARTY 2012.



WAKALI wa Muziki wa Dansi Bongo African Stars Band "Twanga Pepeta" Jumapili hii 21-10-2012 katika ukumbi wa Mzalendo Pub inatarajia kufanya Patty maalum kwa ajili ya mashabiki wake wa mitandao ya Kijamii (Facebook, Twitter,BBM, Blogs N.k).

Patty hiyo itafanyika katika ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama na matayarisho yote yamekwisha kukamilika na itaanza kuanzia saa tatu usiku mpaka tisa za usiku.

Nia ya kuandaa tafrija ya Twanga facebook Fans Party ni kutambua, kuwathamini na kuwatambua marafiki wote wanaoisapoti Twanga Pepeta kupitia mitandao ya kijamii.

Sambamba na hilo pia Twanga itatumia fursa hiyo kuwathamini wale wote waliotoa mchangu mkubwa (wakiwemo wanamuziki waliopo sasa na waliopita, Vikundi vya mashabiki, Mtu mmoja mmoja, Wanahabari, wanaoendesha Blog mbalimbali, Kumbi mbalimbali , BASATA, Mapromota,  na wengine wote waliotoa sapoti kwa namna moja au nyingine)  kwa kufanikisha mafanikio ya Twanga toka kuanzishwa kwake mpaka leo.

Burudani itatolewa na African Stars Band "Twanga Pepeta" wakishirikiana na baadhi ya wanamuziki waliowahi kuitumikia Twanga Pepeta toka inaanzishwa mpaka leo. Baadhi ya wanamuziki waliothibitisha kushiriki ni Ally Akida, Khalid Chokoraa, Soud Mohammed au MCD na wengine wameahidi kuthibitisha hapo baadae kabla ya kufanyika kwa onyesho.

Friday, October 19, 2012

BAADA YA KUFANYA SHOW YA VODACOM KARIBU MIKOA YOTE YA TANZANIA KWA MAFANIKIO MAPACHA WATATU WASASA WAREJEA DAR LEO KUTAMBULISHA WANAMUZIKI WATATU WAPYA VIPAJI TOKA MIKOANI WAKISINDIKIZWA NA ISHA MASHAUZI NDANI YA MANGO GARDEN

Mapacha watatu baada ya ziara mikoani ktk kuitangaza vodacom m-pesa..sasa 

wamerudi dar kwa kishindo kwa kuandaa bonge la show 

ya utambulisho wa wanamuziki wapya ambao ni..samaduu,john cena,papii 

pamba,hwa ni waimbaj madencerz ni mwamgeni na frank na 

show itfanyika mango garden tukisindikizwa na isha mashauzi..wanamuziki 

wetu wametoka bebdi za mitaani huko mikoani tulipo kua na ni 

wagen kabisa ktk jiji la dar nia na madhumuni kuchukua wanamuziki wa 

Toka mikoani  moja ikiwa ni kuwa hawataki beaf na  na maband mengine lakini 

pia kunyanyua vipaji vingine kutoka mikoani na pia kutengeneza band          

itakayokua tofauti na band nyingine 

                          MAPACHA WATATU KATIKA MUONEKANO MPYA

show ni ijumaa tar 19-10-2012 mango garden,mapacha ambayo kwa sasa 

inaongozwa na KHALID CHOKORAA,AJOSE MARA.JANUARY,KAMBI PAMOJA NA 

FIRST LADY WAO CATHERIN wanatikisa na vibao vyao kwa sasa cha naonewa 

ambacho wameshirikisha ALLY KIBA NA CHANZO WANAUME ambachO 

wameshirikisha malkia wa mipacsho tanzania KHADIJA OMARY KOPA

Thursday, October 18, 2012

KUTOA MIMBA KWA WASANI WA BONGO MOVIE NI KAMA FASHION-MAINDA



Msanii wa kike asiye na skendo mjini hapa MWANAIDI SUKA (MAINDA) amefunguka na kusema kitendo cha kutoa mimba kwa wasanii wa kike ni cha kawaida kabisa kwani usipofanya hivyo unaonekana hauko kwenye fashion,,,,Mainda alisema kuwa wasichana wamekuwa hawajihurumi pamoja na kuwa madhara wanayajua ikiwa wapo wengi waliopoteza maisha na wengine kutokuweza kuzaa kabisa kwa sababu hizo lakini hawakomi

ISSA MUSSA .a.k.a CLOUD AIACHIA FILAMU YAKE YA PENZI LA GIZA SOKONI KWA SASA INAPATIKANA MADUKA ASEMA NI YA KIWANGO CHA HALI YA JUU

MTUNZI,MUONGOZAJI HODARI WA FILAMU ZA KITANZANIA CLOUD KUPIITIA KAMPUNI YAKE AMAIACHIA RASMI KAZI YAKE YA PENZI LA GIZA MAMBAYO KWA SASA INAPATIKA RASMI MADUKANI AMBAYO INAWAIGIZAJI AMBAO SI MAARUFU SANA ILA WAMEFANYA KAZI NZURI SANA NDANI YA FILAMU HIYO
                                                COVER LA PENZI LA GIZA
CLOUD AMESEMA WATANZANIA KWA SASA WAONYESHE UZALENDO WA KUNUNUA KAZI ORIGINAL. NA KWA SASA YUKO MBIONI NA YUPO KWENYE FINAL TOUCH ZA KUMALIZA MOVIE YAKE NYINGINE YA FUNGATE AMBAYO ANASEMA NAYO ITAKUA  TISHIO SAANA!

Wednesday, October 17, 2012

BAADA YA TOTOO ZE BINGWA NI ZAMU YA CRISTIAN BELLA ANADAIWA KUONDOKA BILA KUAGA NDANI YA BAND YA AKUDO IMPACT INASEMAKANA NA YEYE SIO TENA AKUDO IMPACT ILA TARSISI MASELA ASEMA AKUDO ITAENDELEA KUWEPO HATA IWEJE

Ukirudi nyumaa utaweza kukumbuka nyimbo kama SAFARI SIO KIFO,MAMA VANNESA,na nyingine nyingi zilizopigwa na akudo impact ambayo kwa siku za hivi karibun inaonekana kususa sua babada ya wanamuziki wake kila mmoja kuamua kufanya kazi kivyake na kundu kuwa pale pale lakini waanzilishi wawili wa kundi hilo kcristiana bella ambae pia alikua ni rais wa band NA TOTOO ZE BINGWA ambae nae alikua kiongozi wa band kusemekana kuachia ngazi baabda ya kwenda nchi za nje ambapo pia tayari ameshaachia kazi zake mbili moja ikiwa ni USILIE NA MSALITI ambazo zinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio ambapo pia masema akiridi ataikamilisha album yake.

CRISTIAN BELLA MASAUTI
LAKINI kwa upande wake kiongozi wa AKUDO kwa sasa TARSIS MASELA JOTO amesema tayari wameshaongeza safu yao ya uimbaji na uchezaji kwa kuchukua wanamuziki wengine wapya  ambao watakuwepo kwenye nyimbo kadhaa ambazo watakwenda kuziweka kwenye album ya AKUDO ijayo ambayo tayari nyimbo nyingi zishakua tayri bado chache za wageni ambazo ziko mbioni kumalizika na baada ya hapo watakwenda kuzindua album yao kama kawaida ambayo itakua na nyimbo NANE

TARSIS alizitaja nyimbo zitakazokuwemo kwenye album hiyo ni UBINAFSI,USIWAFATE WAMBEA  NA MWIKO AMBAZO NI UTUNZI WAKE MWENYEWE,UMEJIFICHA WAPI,USIKATE TAMAA,UBINADAMU KAZI,PONGEZI KWA WANANDOA,UTAMU KUZIDI ASALI ambapo kwa sasa wanamalizia wimbo wa mwisho wa utamu kuzidi asali


 

Tuesday, October 16, 2012

JACOB STEVEN a.k.a J.B a.k.a DJ BEN a.k.a TAX DRIVER AMESEMA WASANII WANAOCHIPUKIA WAWE NA SUBIRA SIO KUKURUPUKIA UMAARUFU AU KUTAKA KUFANYA KAZI NA WATU MAARUFU BILA KUPITA HAUA ZINAZOTAKIWA,AJIFANANISHA NA DENZEL WASHINGTON NA KUSEMA HATA YEYE HAWEZI KUTAKA KUFANYA KAZI NA DENZEL GHAFLA GHAFLA LAZIMA AHANGAIKE KWANZA HATA WAO WALISOTOA IVO IVO,ASEMA FILAMU YAKE MPYA YA UKURASA MPYA NDIO FUNGA KAZI

GWIJI wa tasnia ya maigizo nchini anaetamba na filamu za DJ BEN,TAX DRIVER,NAENDA KWA MWANANGU na hivi sasa akiwa mbioni kuingiza sokoni moive yao mpya kutoka jerusalem iitwayo UKURASA MPYA ambayo ndani yake kutakuna na msanii BANANA ZORO, muingiza mkongwe DAVINA na IRENE PAUL wakati huo huo wakiwambioni kufanya movies nyingine.

                                     JACOB STEVEN KATIKA POZ TOFAUTI

akifunguka kuhusina na ubaguzi wa wao kutoshiriki katika au kukataa kufanya movies na underground amesema kila kitu kina process kwa hiyo itakua ngumu kwa wao kufanya hivi na vile vile wao kuwashirikisha underground kwenye filamu zao na inakua ngumu kuwachukua wengi kutokana na soko lilivyo sasa ambapo wasambazaji wanataka majina  makubwa katika uuzaji wa movies hizo.
                                                JACOB IN ACTION
AIDHA JB amefunga na kiusema wasanii wanaochipukia kutaka umaarufu kwa ghafla ndio matokeo yake yanawakuta mabalaa  ya kashfa na kutakwa kimapenzi kwa kuwa wanapupa na umarrufu huku akisema kuwa umaarufu huwa unakuja pole pole na kazi ndio inayoweza kumfanya msanii awze kutafutwa kwenye movie mara kwa mara na mwisho wa siku kuwa super star na kutoa mfano wakina jacline wolper kuwa nao wameanza chini mpka sasa wanapata hela nzuri basi na wengine wakitaka kutoka lazima wafate taratibu ambazo zitawafanya kujlikana kwa kazi si kama livyosasa wengi wao wakiwa wanakurupuka

Monday, October 15, 2012

NANI ANAMKUMBUKA AMINA NGALUMA JAPANES ALIEWAHI KUTIKISA KATIKA MUZIKI WA DANSI KIPINDI CHA DOUBLE M,YUPO THAILAND AKIENDELEA KUPIGA MUZIKI,ASEMA AKIRUDI BONGO KAMA MUNGU AKIJALIA LAZIMA AANZISHE BAND YA UKWELI

KAMA unakumbuka vizuri kipindi cha DOUBLE M,AFRICAN REVOLUTION,ukimzungumiza AMINA NGALUMA ni mmoja kati ya wanawake wachache walioweza kusimama katika muziki wa band na kipindi hicho unawakuta kina JESCA CHARLS,LUIZA NYONI MBUTU,KHADIJA MNOGA basi na eye ni mmoja kati ya waliosimama kipindi hicho
G .MBONGO nilifanya jitihada za kutaka kujua yuko wapi kwa muda mrefu au na yeye kaacha muziki kama wanavoachishwa wengine pindipo wanapopata mabwana ndipo hapo nilipokwenda kumchimbua toka huko THAILAND ambapo anapiga muziki wa hotel kwenye band moja inayoitwa THE JAMBO SURVIVER ambapo yupo na baadhi ya watanzania wenzake wakiendela kufanya muziki wao na copy pia.
                              AMINA NGALUMA  AKIWA NA WANA JAMBO SUVRVIVER
AMINA amesema bado anaendelea kutafuta lkn sio maisha ndio yatakua THIALAND hivyo pindipo atakapo rudi bongo ana mpango wa kuanzisha band ambayo itakua inapiga kwenye mahotel na nyimbo zake mwenyewe ambazo amesema atakuja kufanya yeye kama yeye lakini pia lengo al kuanzisha band ya kupiga kwenye hotel ni kwa kuwa inalipa sana kushinda band ambazo zinapiga kwenye makumbi ingawa anatumai band yake itakua tofauti sana na band zingine

 

Sunday, October 14, 2012

TX MOSHI WILLIUM AKIWA SAMBAMBA NA ROMARII WAKIFANYA VITU

HIVI NDIVYO MSONDO NGOMA WALIVYOFANYA MTWARA WEEKEND HII KUMBEE MZEE GURUMO BADO YUMO SANAAA AWAKONGA MASHABIKI NYOYO

                                   MZEE MAALIM SALEH GURUMO AKIFANYA VITU
                                 JUMA KATUNDU NA TX JOUNIOR WAKIFANYA VITU
                                 BAADHI YA MASHABIKIWAKIBURUDIKA NA MSONDO
        
                                      ROMARI AKIKONGA NYOYO ZA MASHABIKI
                                  NIKIWA NA KIONGOZI WA MSONDO SAID MABELA
                                   NIKIWA NA MKONGWE SHAABAN DEDE "ANCO"
      HAWA NDIO WAPULIZA MIDOMO YA BATA WA MSONDO WAKIJIACHIA NA MIMI
 
   
                                  TX JONIOUR AKIMUENZI BABA

                                           MZEE GURUMO"BABU"
                                            NIKIWA NA TX JOUNIOR

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...