WAY

Monday, October 15, 2012

NANI ANAMKUMBUKA AMINA NGALUMA JAPANES ALIEWAHI KUTIKISA KATIKA MUZIKI WA DANSI KIPINDI CHA DOUBLE M,YUPO THAILAND AKIENDELEA KUPIGA MUZIKI,ASEMA AKIRUDI BONGO KAMA MUNGU AKIJALIA LAZIMA AANZISHE BAND YA UKWELI

KAMA unakumbuka vizuri kipindi cha DOUBLE M,AFRICAN REVOLUTION,ukimzungumiza AMINA NGALUMA ni mmoja kati ya wanawake wachache walioweza kusimama katika muziki wa band na kipindi hicho unawakuta kina JESCA CHARLS,LUIZA NYONI MBUTU,KHADIJA MNOGA basi na eye ni mmoja kati ya waliosimama kipindi hicho
G .MBONGO nilifanya jitihada za kutaka kujua yuko wapi kwa muda mrefu au na yeye kaacha muziki kama wanavoachishwa wengine pindipo wanapopata mabwana ndipo hapo nilipokwenda kumchimbua toka huko THAILAND ambapo anapiga muziki wa hotel kwenye band moja inayoitwa THE JAMBO SURVIVER ambapo yupo na baadhi ya watanzania wenzake wakiendela kufanya muziki wao na copy pia.
                              AMINA NGALUMA  AKIWA NA WANA JAMBO SUVRVIVER
AMINA amesema bado anaendelea kutafuta lkn sio maisha ndio yatakua THIALAND hivyo pindipo atakapo rudi bongo ana mpango wa kuanzisha band ambayo itakua inapiga kwenye mahotel na nyimbo zake mwenyewe ambazo amesema atakuja kufanya yeye kama yeye lakini pia lengo al kuanzisha band ya kupiga kwenye hotel ni kwa kuwa inalipa sana kushinda band ambazo zinapiga kwenye makumbi ingawa anatumai band yake itakua tofauti sana na band zingine

 

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...