WAY

Wednesday, October 31, 2012

SAJUKI AFADHALI SASA NA KUTOA SHUKURAN KWA SINGO moja kali sana get ready!!



Ni kitambo sasa  tangu kuwepo kwa taarifa kuwa staa wa Bongo Movie, Juma Kilowoko, 'Sajuki' ni mgonjwa , huku pia taarifa za karibuni zikidai kuwa  hali ya  nyota huyo  bado ni tete na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wake.

Taarifa rasmi ni kuwa hali nyota huyo kwa sasa  ni njema na  yuko tayari tena  kuanza kuwatumikia  watanzania  kupitia tasnia ya  filamu.


Kwenye Exclusive interview aliyofanya na teentz.com mapema leo Sajuki amewashukuru watanzania  kwa kuwa pamoja nae kwenye wakati wote wa  matatizo  mpaka sasa  anajisikia yuko vizuri tofauti na ilivyokuwa awali.

Nashukuru kuwa  sasa niko poa, watanzania  waelewe hilo, kwa sasa  naweza hata kuendesha gari na karibuni nitaanza  kucheza muvi tena  alisema Sajuki.

Katika kuonyesha kuwa anathamini mchango wa Watanzania Sajuki ameachia ngoma ambayo ameamua kuipa jina la Shukurani

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...