WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Monday, December 31, 2012

EXECUTIVE MASSAGE CENTRE MOJA KATI YA MASSAGE CENTER ZA KISASA NDANI YA MTWARA INAYOENDESHWA NA WATAALAMU WA MASSAGE KAMA INAVOJULIKANA MASSAGE NI MOJA YA DAWA NZURI TU KWA MWILI WA MWANADAMU KWA KUIFANYA MTWARA YA KISASA ZAIDI KARIBU NDANI YA EMC


                         MOJA KATI YA VYUMBA VYA KUFANYIA MASSAGE(EMC)
                                 Miss Nuru...one of the massage specialist at EMC MTWARA
 

Monday, December 17, 2012

MUUMINI MWINJUMA KUITAMBULISHA RASMI VICTORIA SOUND LEO NDANI YA MTWARA ACHUKUA WANAMUZIKI TOKA,FM ACADEMIA,MASHUJAA,TWANGA,MAPACHA NA WENGINE CHIPUKIZIAMEANZA MAZOEZI LEO.

MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi ambae alishwahi kutamba na band mbali mbali za tanzania, ambapo zingine aliweza kuzimiliki yeye mwenyewe na baadae kutua twanga pepeta ambapo ndipo alipotokea sasa ametua rasmi ndani ya mtwara kwa ajili ya kuweka kambi ya  kujiandaa namahsambulizi ya kuliteka jiji tena kama alivyofanya kipindi cha double m na band zingine,ambapo amesema kwa sasa anaamini band hiyo itaweza kufanya vizuri zaidik kuliko zilizopita ambapo management yote ilikua anaiongoza yeye hivyo vitu vingine vikakosa ufanisi wa kuweza kufanya kazi na kupelekea bad hizo kuweza kufa mapema lakini kwa sasa amesema ataweza kuzirekodi na nyimbo nyingine za bwagamoyo sound band ambazo hakuweza kuzitoa kutokana na ukata ulioikumba band hiyo.
 muumini aliwataja baadi ya wanamuziki ambao wataunda band yake hiyo ni pamoja na WAZIRI SONYO,KASSIM BASS(mashujaa band)SELE MOMBA,(twanga pepeta)mpiga druma kutoka MAPACHA WATATU na wacheza show wawili kutoka fm academia COBRA NA EVA SIMBA na wengine kutoka mashujaa CHIKU NA MARIAM na wengine wengi ambao ataendelea kuwatambulisha baadae.
                             RAIS WA VICTORIA SOUND MUUMIN MWINJUMA

Friday, December 14, 2012

BAADA YA SHOW YAO YA KESHO YA KUSINDIKIZA KOFFI OLOMIDE TWANGA PEPETA WAMEANDAA BONANZA KUBWA LITAKALOITWA FAMILY DAY BONANZA YA TWANGA TAREHE 30-12-2012.




KATIKA Family Bonanza zote zilizowahi kufanywa na Twanga Pepeta, basi hili linalotarajiwa kufanyika Jumapili ya mwisho kabisa kwa mwaka huu, litakuwa halina mpinzani.
Tarehe 30 mwezi huu, bendi hiyo imeandaa onyesho kubwa la kifamilia ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, likiwa ni maalum kwa ajili ya kuuaga mwaka 2012, ambapo itapigwa show kali ya Twanga Pepeta, huku nyimbo zote mpya za albam ijayo zikitambulishwa kwa mashabiki kabla ya uzinduzi rasmi.
Lakini cha kufurahisha zaidi ni kwamba kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Aset inayomiliki bendi hiyo, Asha Baraka, kiingilio kinatarajiwa kupunguzwa kwa kiasi kikubwa ili kuwawezesha watu wengi kujumuika katika bonanza hilo la Funga Mwaka.
Asha Baraka ameiambia Saluti5 kuwa bendi kadhaa rafiki za Twanga, zitaalikwa katika onyesho hilo.
Twanga ambayo inasifiwa kwa kufukua wanamuzki wasiojulikana na kisha ikawatengeneza hadi kuwa masupa staa, itatumia onyesho hilo kufanya ‘surprise’ itakayozidi kudhihirisha kuwa Twanga Pepeta ni kisima cha burudani kisichokauka. 
“Tutafanya jambo moja kubwa, kwa sasa si wakati wake kulisema, lakini mashabiki wa bendi yetu na wale wote wanaotutakia mema watafurahi siku hiyo” alisema Asha Baraka na kuongeza kuwa Bonanza hilo litakaloanza saa 10 alasiri litakuwa ni tofauti kabisa na mabonanza yao ya kila Jumapili.

Thursday, December 13, 2012

KUELEKEA SHOW YA KOFFI ZENGWE LAIBUKA ALAIN MULUMBA ASHTUSHWA KUSIKIA KUNA DIAMOND MUSICA ORIGINAL ITAKAYOSINDIKIZA SHOW YA KOFFI OLOMIDE ASEMA YEYE HANA TAARIFA YOYOTE KUHUSIANA NA BAND HIYO ILA DIAMOND MUSICA BADO IPO,LAKINI SIO AMBAYO ITASINDIKIZA SHOW HIYO

                                                       ALAIN MULUMBA KASHAMA
Ikiwa ni bado siku kadhaa kuweza kushudia show ya mwanamuziki nguli  katika muziki wa kiafrica KOFFI OLOMIDE  limeibuka zengwe la band itakayosindikiza show ya kofii olomide moja wapo ikiwa ni DIAMOND MUSICA ORIGINAL ambapo kwa mujibu wa kiongozi wa band ya diamond musica international ALAIN MULUMBA KASHAMA nilivyomuuliza kuhusiana band yake kusindikiza show hiyo alishtuka na kusema kuwa band yao wenyewe hawajapewa mualiko ila anashangaa kusikia kuwa kuna diamond musica oroginal ambayo hata nyimbo zake hazijulikani hivyo watu kudhani kuwa band itakayosindikiza show hiyo itakua ni ya akina alain mulumba na hivyo na kusema kuwa hapo wamejitafutia jina la kuweza uvuma lakini ingawa hajui kabisa band hiyo ya ya diamond musica original imetokea wapi lakini amesema inawezekana kabisa imeanzishwa na aliekua mwanamuziki wa diamond zamani ambae pia aliunda band ya shegheni LIVER HASSAN SULTAN ambae pia anamiinika kuwa ndio muanzishaji wa band hiyo nyingine
                                                      LIVER HASSAN SULTAN
 PIA alain mulumba amesema kwa sasa amemua kufanya kazi zake mwenyewe ambapo kwa sasa yupo mbioni kutengenza video ya wimbo wake wa kibinda nkoi remix ambayo itakua kwa jina lake mwenyewe na si diamond musica tena ingawa wao kama wao diamond musica anasema bado wapo ila wanatafuta tu mdhamini ili kuweza kuanza kufanya tena kazi.

Wednesday, December 12, 2012

MUUMINI MWINJUMA KUIVUNJA TWANGA NA MASHUJAA MUSICA AMCHUKUA MPIGA SOLO ANAETEGEMEWA KWA SASA TWANGA SELE MOMBA NA MPIGA BASS PEKEE WA MASHUJAA KASSIM BASS KUMRUDISHA KATIKA GAME WAZIRI SONYO KATIKA KUIMARISHA SAFU YA UIMBAJI VICTORIA SOUND KUWEKA KAMBI MTWARA

PRINCE MUUMINI MWINJUMA ambae pia ni rais mpya wa band ya VICTORIA BAND ambae kwa sasa amesema yuko kwenye makakati wa kusajili wanamuziki wapya wa band yake hiyo ambayo amesema itakua tishio katika medani ya muziki wa dansi na kusema kwa sasa yuko kwenye mchakato wa kusajili waimbaji chipukizi lakini tayari ameshawachukuwa wanamuziki wawili kutoka band kubwa ambapo amemchukua SELE MOMBA mpiga solo wa twanga pepeta ambae anakuja juu sana kwa sasa lakini vile vile na mpiga bass wa kutumainiwa wa MASHUJAA MUSICA,KASSIM BASS ambapo kwa mashuja mpiga bass ni mmoja tu na kuonyesha kwamba mashuja itabidi wafanye kazi ya ziada ya kuweza kumtafuta mpiga bass mwingine atakae weza kuziba pengo la kassim bass ingawa mwenyewe bado hajathibitisha kuondoka katika band hiyo.

                                                 SELE MOMBA KUTOKA TWANGA
                                    KASSIM BASS WA MASHUJAA BAND
PIA MUUMINI amesema lengo la kuweka kambi mkoani ni kwasababu ya usiriaz wa mazoezi ambayo watakua nayo kwa miezi kadhaa kwa ajili ya kutengeneza nyimbo mppya za band hiyo ambazo zitasammbazwa kwenye maradio baada ya kutka kurekodi huku kwa hiyo kambi yao inaweza kuwa ya miezi mitatu hadi minne kwa ajili ya kujiweka fiti na baada ya hapo wataweza kurejea dar kuweza kupambana na band nyingine jijini

IRENE UWOYA: AFUNGUKA NA KUSEMA KUWA KWA MWAKA 2012 HAJAFANIKIWA KABISA KATIKA MIPANGO YAKE KATIKA FILAMU




STAA wa filamu ambaye popote atakapopita shabiki lazima amshangae, Irene Uwoya, anasema kuwa mwaka 2012 unamalizika lakini asilimia kubwa ya mambo yake hayakutimia.

Anasema ndoto zake kubwa katika tasnia ya filamu ambazo kwa asilimia fulani anaamini hajazikamilisha, atazikamilisha mapema mwakani.

Kwa sasa kuna changamoto nyingi sana katika tasnia ya filamu ambazo kama msanii unatakiwa kuzikabili katika kulinda maslahi," alisema.

"Imenilazimu kupunguza muda wa kazi ili kupumzika na kufikiria filamu mpya ambayo itakuwa bora."

Irene anasema moja ya njia ya kuongeza maslahi kwa msanii wa filamu ni pamoja na kumiliki kampuni itakayojishughulisha na kazi ya kurekodi filamu na kufanya kazi za kampuni yake kwa kiwango kikubwa.

Kwa sasa watayarishaji wengi wanajitahidi kumiliki kampuni za utengenezaji wa filamu katika kujiongezea maslahi zaidi.

Tuesday, December 11, 2012

KUELEKEA SHOW YA KOFII OLOMIDE ZENGWE LA ASHA BARAKA KUTOTAKA MAPACHA WASHIRIKI ONYESHO HILO AFUNGUKA NA KUWEZA WAZI KUWA YEYE SIO MUAANDAJI HAWEZI KUPANGA MASHARTI YA BAND ZA KUIMBA ASEMA WASIWASI WAO KHALID CHOKORAA ASEMA BAND KUBWA HAZIJIAMINI NA PERFOMANCE ZAO NDIO MAANA WANAWAOGOPA ASEMA WATAAFANYA SHOW AMBAYO HAIJAWAHI TOKEA

WAKATI tukuelekea katika show ya KOFF OLOMIDE jumamosi ijayo mengi yameibuka kuhusiana na show hiyo ambapo kuna habari za chinichini zilizokuwa zinaungumzwa kuwa twanga wanataka kujitoa kutokana na mapacha watatu kuwepo katika show hiyo kwa aidha watoke wao au mapacha zengwe hilo nimelifatilia pande zote mbili ambapo niliweza kuongea na  DADA ASHA BARAKA ambae na yyeye ni mmoja ya waratibu wa tamasha hilo la koffi olomide na kusema yeye kapewa kazi tu ya kuratibu na si kusema band gani iimbe na band gani isiimbe kwa hiyo hilo ni swala la uongo ambalo watu wanaamua kutengeneza ili kumchafua lakini pia amesema yeye wamejiandaa kufanya hiyo show na watafanya nae show mbili nyingine watafanya nae tar 21 kilimanjaro.
                                             ASHA BARAKA MKURUGENZI WA ASET
LAKINI nae mkurugenzi wa mapacha watatu khalid chokoraa nilivyomuuliza kuhusiana hilo na akasema kuwa band nyingi zenye majina makubwa zinawaogopa kutoka na kuwa na perfmance ya chini hivo wanakuwa wanatilia zengwe ili wasiweze kushiriki katika matamamasha mbali mbali kutokana na kuogopa kufunikwa lakini hiilo lishashindikana kwa kuwa kwa sasa ndio wanapata show nyingi zaidi ya mwanzo na mungu anazidi kuwanyooshea.
                                                   WAKURUGEZNI WA MAPACHA WATATU

Sunday, December 9, 2012

FM ACADEMIA KUFANYA TAMASHA LA KUSHEHEREKEA MIAKA 15 KUZIALIKA BAND MBALIMBALI NA WANAMUZIKI WOTE WALIOWAHI KUPITIA FM ACADEMIA KUSHIRIKI KATIKA TAMASHA HILO ITAKUA NI SIKU MOJA KABLA YA KUPANDA JUKWAA MOJA NA KOFFI OLOMIDE

Band kongwe tanznia ya muziki wa dansi ambayo pia imejizolea mashabiki wengi kiasi cha kutosha wiki hii kufanya tamasha la kuadhimisha miaka 15 toka kuanzishwa kwa band hiyo ambapo  imepitia misukosuko mbali mbali moja wapo jela ambapo mapka wakaamua kujiita m academia wajelajela kabla ya kugawanyika na wengine kujiita wajelajela original na wengine wakijiita wajelajela gwaa.
                                     NIKIWA NA NYOSHI EL SAADAT
FM academia mbayo inaundwa na wanamuziki wengi wenye vipaji ila inayoongozwa na NYOSHI EL SAADAT lakini pia kuna wanamuziki kama PATCHO MWAMBA,MULE MULE,KING BLAISE,TOSCANEE NZIMBU,CHEK DAR,KALIDJO MWANA KITIKOLOLO,TOTOO KALALA,BARATEL DRUMS,EROMBEE KICHINJA NA WENGINE KIBAOOO.
 KATIKA sherehe hizo za fm academia band mbali mbali zitaweza kuhudhuria moja wapo ikiwa mapacha watatu,toto ze bingwa,na band nyingine ambazo zitatajwa hivi karibuni fm academia tyARI WANATAMBA NA ALBUM AMBAZO ZIMEKUA GUMZO SANA kama vile FREEDOM,DUNIA KIGEUGEU,VUTA NIKUVUTE LAKINI KWA SASA IPO JIKONI CHUKI ZA NINI AMBAYO ITAENDA KUTAMBULISHAWA RASMI SIKU HIYO.
                                             WAZEE WA NGWASUMA

Friday, December 7, 2012

BAND INAYOZIDI KUNG'ARA TANZANIA KWA SASA MAPACHA WATATU a.k.a WAKALI WA TOWN KUSIMAMA JUKWAA MOJA NA GWIJI WA MUZIKI AFRICA KOFFI CHALS ANTONIE OLOMIDE TAR-15 MWEZI HUU

MAPACHA WATATU 'WAKALI WA TOWN' WATAPANDA JUKWAAA MOJA NA MFALME WA MUZIKI WA MAYENU KUTOKA JAMHURI YA DEMOKRASIA YA KONGO, KOFII OLOMIDE, DESEMBA 15 KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB. 
                                                  WAKURUGENZI WA MAPACHA
AIDHA MAPACHA KUPITIA FACEBOOK WATATOA COMPLIMENTARY MOJA KAMA UTAJIBU SWALI HILI, TAJA MAJINA KAMILI YA WAKURUGENZI WA MAPACHA WATATU, JOSE MARA NA CHOKORAA
KWA MIJIBU WA MENEJA WA MAPACHA KWA SASA WAKO KATIKA MAZOEZI MAKALI YA KUWEZA KUWANGOKA MASHABIKI WATAKAOFIKA UWANJANI HAPO NA KWEZA KUPATA VITU VIPYA KABISA AMBAVYO VITAKUWEPO KWENYE ALBUM YAO IJAYO AMBAYO IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO KABISA 
IKUMBUKWE PIA KWA SASA KOFFI ANATIKISA NA ALBUM YAKE YA ABRACADABRA NA ITAKUA KWA MARA YA KWANZA  VILE VILE KUJA KWA NA MWANAMUZIKI WA KIKE AMBAE KWA SASA NI TEGEMEO LA KOFFI CIDY LE CUER PAMOJA NA KUNDI LAKE JIPYA LA QURTEN LATIN LE MAINER AMBAPO KUNA VIPAJI VIPYA VITANAVYOFANYA VIZURI NA KOFII OLOMIDE

Thursday, December 6, 2012

MUUMINI MWINJUMA KUZIVUNJA BAND KUBWA TANZANIA KUIIMARISHA VICTORIA BAND,KUJICHIMBIA KUSINI KUANDAA MASHAMBULIZI TAYARI WIMBO KADHAA KWA AJILI YA YA MASHABIKI WAKE NA VICTORIA JE BAND GANI NA GANI KUBOMOLEWA NA MUUMINI!?

Baada ya kurejea kutoka kenya bila vipaji alivyoenda kuvitafuta muumini amesema kwa sasa ili kuweza kuinda band yake iwe bora kama zingine anafanya mpnago wa kuweza kuzibomoa baadhi za band kubwa tanzania ikiwemo TWANGA PEPETA,EXTRA BONGO na nyingine ambapo amesema tayari anayotimu kilichobaki ni kuwasainisha tu halafu aweze kuiingia nao kambini aidha iringa au mtwara ambapo hivi karibu atatembmela ili aweze kupata sehemu nzuri kwa ajili ya kuweza kuweka chimbo katika kuandaa nyimbo ambazo  watakwenda kuzirekodo na kuanza nazo kazi baada ya kurejea dar-es-salaam ambapo anaamini ataweza kutikisa kwa kiwango kikubwa na kuweka band nyingine za kihistoria
LAKINI nilivyomuuliza kuhusiana na kufa kwa band ambazo alizianzisha akasema kwa mafano band ya mwisho yeye ndio alikua mkurugenzi na kila kitu kwa hiyo hakuweza kuhimili vishindo lakini kwa sasa kapata muwezeshaji sa ivi yeye ni rais wa band tu ambae anapanga mipango ya mashambuli katika muziki ila kuna muwezeshaji ambae ataweza kusimamia kwa kila kitu ambacho kitakua kinahitajika!
 aidha muumini alizitaja nyimbo ambazo zilizoandaliwa nia mpamoja na mapambano ya kipato ambayo alitokana twanga pamoja na utafiti wa mapenzi ambazo wataanza nazo katika band hiyo baada ya kupata wanamuziki anaowahitaji

Tuesday, December 4, 2012

SAJUKI NA WASTARA WAANDAA MATAMASHA KWA AJILI YA KUWASHUKURU WATANZANIA KWA DUA ZAO NA MICHANGO YAO,MWEZI WA KUMI NA MBILI HUU KUACHIA MOVIES YAO MPYA YA KIVULI LAKINI PIA SAJUKI ATOA ALBUM YA MUZIKI KWA AJILI YA WATANZANIA

WAkizungumza na mimi kwa njia ya simu leo huku sajuki akithibitisha kwa sasa ana afadhali sana kwani hata napoongea nae alikua akiendesha gari nguvu ambazo hata awali hakua nazo kabisa lakini kwa sasa kuna baadhi ya vitu anaweza kuvifanya kwa kuwa ananihisis anaelekea kupona kabisa hivyo basi kwa hali aliyoua nayo sajuki akishirikiana na mkewe wastara wameamua kuanzisha matamasha kuzunguka mikoa tofauti kwa ajili kuwashukuru watanzania na mashabiki wao ambao waliweza kutoa michango yao ya hali na mali na kumuwezesha kwenda kupata matibabu india na kurejea tanzania.
                                                        SAJUKI NA WASTARA
mbali na shukurani hizo kwa wananchi pia sajuki ameandaa album ya nyimbo kama nane hivi ambazo ndani yake kutakua na nyimbo zenye mahadhi tofauti tofauti kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania uwezo wake mwingine katika uimbaji ambayo ni moja ya fani ambazo anazo pia lakini pia ni katika kuwaburudisha watanzanina na kutoa shukurani zake kwa njia ya muziki ambapo humo kuna nyimbo za kiyao alizochanganya na kihindi na nyingine nyingi zenye kuhuzunisha na kuliwaza pia.
MBALI na hilo pia sajuki na wastara wako mbioni kuachia movies yao wlioitengeza kipindi alichorudi kutoka kwenye matibabu ambayo wameipa jina la KIVULI ambapo kwa mujibu wa sajuki amesema ndani yake kuna vitu ameonyesha kidogo ili kuwajulisha watanzania kuwa bado anaweza kufanya sanaa
NAE wastara kwa upande wake amesema wameamua kufanya MATAMASHA YA SHUKRANI KWA WATANZANIA kwa kuwa hawezi kumfikia kila mtanzania kwa hiyo watafanya kwa mtindo huo wa matamasha kwa ajili ya kuweza kuonyesha hisia zao kwa waliowaombea dua na michango ya hali na mali lakini pia amesema hivi karibuni sajuki ataenda india kwa ajili ya kufanyiwa chek up ambayo ataweza kuruhusiwa kufanya kazi zake kama kawaida

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...