WAY

Tuesday, December 4, 2012

SAJUKI NA WASTARA WAANDAA MATAMASHA KWA AJILI YA KUWASHUKURU WATANZANIA KWA DUA ZAO NA MICHANGO YAO,MWEZI WA KUMI NA MBILI HUU KUACHIA MOVIES YAO MPYA YA KIVULI LAKINI PIA SAJUKI ATOA ALBUM YA MUZIKI KWA AJILI YA WATANZANIA

WAkizungumza na mimi kwa njia ya simu leo huku sajuki akithibitisha kwa sasa ana afadhali sana kwani hata napoongea nae alikua akiendesha gari nguvu ambazo hata awali hakua nazo kabisa lakini kwa sasa kuna baadhi ya vitu anaweza kuvifanya kwa kuwa ananihisis anaelekea kupona kabisa hivyo basi kwa hali aliyoua nayo sajuki akishirikiana na mkewe wastara wameamua kuanzisha matamasha kuzunguka mikoa tofauti kwa ajili kuwashukuru watanzania na mashabiki wao ambao waliweza kutoa michango yao ya hali na mali na kumuwezesha kwenda kupata matibabu india na kurejea tanzania.
                                                        SAJUKI NA WASTARA
mbali na shukurani hizo kwa wananchi pia sajuki ameandaa album ya nyimbo kama nane hivi ambazo ndani yake kutakua na nyimbo zenye mahadhi tofauti tofauti kwa ajili ya kuwaonyesha watanzania uwezo wake mwingine katika uimbaji ambayo ni moja ya fani ambazo anazo pia lakini pia ni katika kuwaburudisha watanzanina na kutoa shukurani zake kwa njia ya muziki ambapo humo kuna nyimbo za kiyao alizochanganya na kihindi na nyingine nyingi zenye kuhuzunisha na kuliwaza pia.
MBALI na hilo pia sajuki na wastara wako mbioni kuachia movies yao wlioitengeza kipindi alichorudi kutoka kwenye matibabu ambayo wameipa jina la KIVULI ambapo kwa mujibu wa sajuki amesema ndani yake kuna vitu ameonyesha kidogo ili kuwajulisha watanzania kuwa bado anaweza kufanya sanaa
NAE wastara kwa upande wake amesema wameamua kufanya MATAMASHA YA SHUKRANI KWA WATANZANIA kwa kuwa hawezi kumfikia kila mtanzania kwa hiyo watafanya kwa mtindo huo wa matamasha kwa ajili ya kuweza kuonyesha hisia zao kwa waliowaombea dua na michango ya hali na mali lakini pia amesema hivi karibuni sajuki ataenda india kwa ajili ya kufanyiwa chek up ambayo ataweza kuruhusiwa kufanya kazi zake kama kawaida

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...