WAY

Friday, December 14, 2012

BAADA YA SHOW YAO YA KESHO YA KUSINDIKIZA KOFFI OLOMIDE TWANGA PEPETA WAMEANDAA BONANZA KUBWA LITAKALOITWA FAMILY DAY BONANZA YA TWANGA TAREHE 30-12-2012.




KATIKA Family Bonanza zote zilizowahi kufanywa na Twanga Pepeta, basi hili linalotarajiwa kufanyika Jumapili ya mwisho kabisa kwa mwaka huu, litakuwa halina mpinzani.
Tarehe 30 mwezi huu, bendi hiyo imeandaa onyesho kubwa la kifamilia ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, likiwa ni maalum kwa ajili ya kuuaga mwaka 2012, ambapo itapigwa show kali ya Twanga Pepeta, huku nyimbo zote mpya za albam ijayo zikitambulishwa kwa mashabiki kabla ya uzinduzi rasmi.
Lakini cha kufurahisha zaidi ni kwamba kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Aset inayomiliki bendi hiyo, Asha Baraka, kiingilio kinatarajiwa kupunguzwa kwa kiasi kikubwa ili kuwawezesha watu wengi kujumuika katika bonanza hilo la Funga Mwaka.
Asha Baraka ameiambia Saluti5 kuwa bendi kadhaa rafiki za Twanga, zitaalikwa katika onyesho hilo.
Twanga ambayo inasifiwa kwa kufukua wanamuzki wasiojulikana na kisha ikawatengeneza hadi kuwa masupa staa, itatumia onyesho hilo kufanya ‘surprise’ itakayozidi kudhihirisha kuwa Twanga Pepeta ni kisima cha burudani kisichokauka. 
“Tutafanya jambo moja kubwa, kwa sasa si wakati wake kulisema, lakini mashabiki wa bendi yetu na wale wote wanaotutakia mema watafurahi siku hiyo” alisema Asha Baraka na kuongeza kuwa Bonanza hilo litakaloanza saa 10 alasiri litakuwa ni tofauti kabisa na mabonanza yao ya kila Jumapili.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...