WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Thursday, January 31, 2013

BAADA YA KUACHIA VIDEO YA NGOMA YAKE YA KIPIMO CHA PENZI TOKA KATIKA ALBUM YA LOVE STORY YENYE NYIMBO 18 MSANII TOKA TAMADUNI MUSIC AZMA MPONDA APANIA MPAKA MWEZI WA SITA NYIMBO ZAKE ZOTE 18 AWE AMESHAZIFANYIA VIDEO

MSANII wa kizazi kipya katika miondoko ya hip hop anaekuja kwa sasa kutoka tamaduni music AZMA MPONDA ambae anatamba na wimbo wake wa kipimo cha penzi audio na jana aliweza kuachia video ya wimbo huo ambao umo ndani ya album yake ya love story amesema huo ni mwanzo tu lakini mapngo wake ni mpka kufikia mwishoni mwa mwezi wa sita anataka nyimbo zote zilizokua katika albmu yake hiyo ziwe ziwe kwenye dvd kwa hiyo kwa sasa project yake ni kufanya video zaidi ili kuendelea kusikuma album yake hiyo ambayo imekua gumzo.
AZMA ambae anasema kwa sasa kama tamaduni wanapush album zilizotoka hivi karibuni ili kuweza kubadilisha kabisa dhana ya kwamba muziki wa hip hop hauuzi
                                                           AZMA MPONDA

KITALE AHOFIA KUONDOKA DUNIA BILA KUOA SASA KUFUNGA NDOA JUMAPILI ASEMA PIA NI KATIKA KUMUENZI SHAROMILIONEA AMBAYE ALIKUA RAFIKI YAKE MKUBWA NA WALIPANGA KUFUNGA NDOA SIKU MOJA ILA MUNGU NAE ALIPANGA YAKE

MCHEKESHAJI NA MSANII WA BONGO FLEVER KITALE amesema panapo maajaliwa jumapili ya tar 3.01.2013 atafunga ndoa huku akiongeza kwa kusema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na maisha ya sasa kubadilika lakini pia hata maagzo ya mwenyezi mungu pia yanasema hivyo kwa sasa ameona ni bora aoe lakini sababu nyingine anasema ameamua kuoa kwa sababu ya kumuenzi  rafiki yake kipenzi MAREHEM HUSSEIN MKIETI almaarufu kama SHARO MILIONEA ambaye walipanga kufunga ndoa siku moja ya tar 14.02.2013 lakini mungu nae anamipango yake aliamua kumchukua na hivyo na yeye akaona bora awahi kuoa kama walivyopanga na rafiki yake.
                                                   KITALE TEJA AKIWA KAZINI
kitale amesema pia wasanii wengi huwa wanalisahau hilo kwa kuendekeza starehe huku wakijua kuwa wananafasi kubwa ya kuwa mifano bora katika jamii kwa kufuata yale yaliyo bora zaidi huku akisema tabia za wasanii wengi huwazinakua haziwafurahishi wanajamii na ndio hata kilichotokea kwa mke wake huyo mtarajiwa kuwachukia sana wasanii lakini mwisho wa siku alimuona kitale yupo  tofauti nawasanii wengine ndio maana hata wakifikia hatua ya kutarajia kufunga ndoa hiyo siku ya jumapili.

TOTOO ZE BINGWA APANIA KUPIGA MZIKI WA ASILI ZAIDI NA BAND YAKE YA SANA SANAA BAND KUIBUKA NA MTINDO WA MDUNDIKO KUIBUA VIPAJI VYA BAND ZINAZOPIGA KWENYE MABAR ILI KUENDELEZA MUZIKI WA KIAFRICA ASEMA NDOTO ZAKE NI KUWA KAMA KINA YOUSER NDOR NA SELIF SIO KUISHIA BONGO

MWANAMUZIKI wa siku nyingi alietamba na band mbali mbali nchini tanznaia ikiwamo AKUDO IMPACT,FM ACADEMIA na nyingine alizofanya miaka ya 2000 na kwa sasa ameibuka na band yake ya SANAA SANA BAND ambayo itakua ikipiga miziki ya asli ikiwemo mdundiko,sindimba na ngoma nyingine za asli za africa ambazo atakua anazipiga katika mtindo wa kisasa na tayari kama sana sanaa band amekwisha rekodi moja kwa ambayo itakua kwenye album yake binafsi na sana nsanaa band.
                  TOTOO ZE BINGWA AKIWAJIBIKA NA SANAA SANA BAND
MBALI na hilo totoo za bingwa pia maepania kusaidia band changa hasa zinazopiga muziki bure kwenye mabar na sasa kwa wale atakaoona wanavipaji anawachukua kisha kuwasaidia kurekodi ambapo kwa sasa amesha fanya na band moja changa alioichukua kutoka kwenye bar moja jijini dar-es salaam na kuweza kuwasaidia kurekodi na kuwabadilisha kutoka kwenyekuimba rhumba na kuifanya nyimbo hiyo kuwa katika mahadhi ya mdundiko
                TOTOO ZE BINGWA NA MWANAMUZIKI WKE NA SHABIKI
TOTOO amerejea hivi karibuni tanznia baada ya kufanya ziara fupi uerop ambapo alienda na wanamuziki wachache wa sanaa sana band na hiyo yote ni kutokana matatizo ya vyombo vyake ambavyo viliharibika na sasa yupo katika mchakato wa kurekebisha na kuanza band full

Wednesday, January 30, 2013

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA BLOG YA GMBONGOTHAINTERTAINER.BLOGSPOT.COM KUANZIA WIKI IJAYO KUWA WA KWANZA KUJUA HABARI ZA WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA,FILAMU NA MUZIKI WA KIAFRICA TOKA TANZANIA PIA KUWA WA KWANZA KUPATA NYIMBO MPYA KWA UHAKIKA ZAIDI LIKE MY PAGE G.MBONGO ILI UWE UPTODATE

Kutokana na mamombi ya mashabiki na wadau wengi wa blog yangu nimeaona kuwa ya kitanzniania zaidi lakini kwa upande wa burudani tu ambapo habari zote mpya utakua unazipata kwenye blog hii ya gmbongothaintertainer.blogspot.com lakini pia habari hizo utaweza kuzipata kwenye timeline yangu ya facebook. g mbongo tha intertainer lakini pia kwenye page yangu ya g.mbongo lakini pia utazipata kupitia group page ya g mbongo na extra africa lakini pia kwenye twitter page ya @GmbongoG lakini vile vile kwenye page ya safari radio media group
                   as my name G MBONGO THA INTERTINER dont miss all entertaiment event ambazo nitaweza kukutafutia dis is my new style kwa blog yangu in 2013 ur mostly n warmly welcome

Wednesday, January 23, 2013

EXTRA BONGO KUFAYA BIRTHDAY KWA KUZINDUA ALBUM YAO YA MTENDA AKITENDEWA AMBAPO WATAUZA AUDIO NA VIDEO PAMOJA NA VIDEO ZA LIVE SHOW WALIZOZIFANYA SEHEMU TOFAUTI ZIKIWEMO WALIZOPIGA NJE YA NCHI

BENDI ya muziki wa dansi inayotikisa katika medani ya muziki huo kwa sasa nchini tanzania imepaia kufanya birthday kwa ajili ya kusherekea miaka mnne ya band hiyo ambapo siku ya uzinduzi wa band hiyo ndio siku ambayo wameamua kuizindua album yao ya MTENDA AKITENDEWA ambayo itakua na nyimbo sita zikiwemo MTENDA AKITENDEWA,UFISADI WA MAPENZI,WATU NA FALSAFA,NEEMA,MAMA SHUU NA SEBENE liliandaliwa na super nyamwela na nyimbo zote hizo zitakua na video zake za live pamoja na studioa ili kuweza kuwapa mashabiki wao ladha tofautitofauti
                                         TIMU NZIMA YA EXTRA BONGO
Akizungumza na na blog hii mkurugenzi wa extra bongo ALLY CHOKI amesema wameamua kufanya mwishoni mwa mwezi wa pili birthday hiyo ingawa walisema ingekua mwishoni mwa mwaka jana lakini amesema kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya kazi imebidi wasogeze mbele zoezi hilo ili kuwapa nafasi mashabiki wao kupata nyimbo zilizokamilika ingawa kwa sasa wameshaanza maandalizi ya nyimbo mpya ambapo nyimbo mya ya khadija mnoga ya mgeni ndio wanayoifanyia mazoezi kwa sasa.

Thursday, January 17, 2013

BAADA KIMYA KIREFU BWANA MISOSI AIBUKA KIVYINGINE SAFARI HII AIBUKIA KATIKA STYLE YA KIAFRICA ZAIDI LAKINI VILE VILE AJITOSA KWENYE FILAMU ASEMA ANATAKA KUWA WA KIMATAIFA ZAIDI

MSANII wa kizazi  kipya aliewahi kutamba na nyimbo kama NITOKE VIPI,HESHIMA,na nyingine kibao baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kumbe kimya kingi kina mshindo mkuu sasa aibuka na style nyingine kabisa na wimbo wake umeanza kutikisa katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni wimbo ukiwa unaitwa IWEJE ambao ameimba katika mahadhi ya zouk ya asili kabisa amesema kwa yeye ana vipaji kibao hapo ameonyesha tu na kusema pia watu wasimkariri kwa style moja kwa anaweza ufanya kila aina ya muziki ila anaamini muziki wa kiafrica ndio wa kimataifa zaidi.
                                                    BWANA MISOSI
MISOSI amesema kazi yake hiyo imekubalika na wengi hata prof jay amempongeza kwa kubadilika huko na kumwambia kaze buti.

lakini vile vile misosi amesema kwa sasa yupo chini ya usimamzi wa kampuni ya hm ambao wanamsimamia kazi zake kwa hiyo mwaka huu utakua wake kwa kuwa amejiandaa vya kutosha na tazidi kuwashangaza watanzania kwa kazi ambazo atazitoa hapo mbeleni.
                                        MISOSI AKIWA NA MPENZI WAKE AMANDA PIA BWANA MISOSI amesema pia maeingia kwenye tasnia ya filamu na hvi karibuni ataibuka na vile moja kali ingawa amesema ni mapema mno kusema amefanya na nani ila kwa mwaka amesema atatimiza ndoto yake kufanya filamu kwa kuwa anaamini ana kipaji hicho cha uigizaji

KINARA WA SIRI YA MTUNGI NA FILAMU YA MAGIC MONEY AFUNGUKA NA KUSEMA MASUPER STAR NA WASAMBAZAJI WANACHANGIA UBOVU WA FILAMU KWA KUANGALIA NANI AMEFANYA NA SIO KIWANGO CHA MOVIES KIKOJE

KINARA anaetamba katika tamthilia ya SIRI YA MTUNGI na filamu yake ya MAGIC MONEY amesema kuna baadhi ya wasanii wakubwa ambao wameshaona game ni yao na hivyo wanaanda movies bora mradi movies na kuziingiza sokoni bila kujali stori wala quality za filamu kwa kujua watanzania ashajua wao ndio waigizaji na pia wasambaji ndio wanazitaka sana filamu za wasanii hao wakubwa matokeo yake unakuta kila mwezi filamu sokoni wakati swala hilo kikawaida haliwezekani na matokeo yake ndio filamu zinazoingia sokoni ni zilizile wakati kuna watu wanaofanya vizuri zaidi ya hao wengine.

aidha daudi ameongeza kuwa sasa imefika wakati kwawatanzania kuchagua kipi bora na baadhi ya watanznia washafunguka akili zao na kuanza kufatilia kipi bora kipi kibaya na mwisho wa siku wale wababishaji katika tasnia watabainika na kurudi chini kutokana na kufanya filamu bora zimefanyika bila kuwajali watanzania ambao ndio wateja.

DAUDI ambae yupo ndani ya tamthilia ya siri ya mtungi ambayo inaonyeshwa kwenye tv mbili ITV NA CHANEL FIVE amesema kwa hiyo ni tamthilia ya aina yake ambayo ni ya kipekee iliyokuja kufanya mapinduzi katika asnia ya uigizaji kutoka na waandaji wake kuwa na uwezo mkubwa na imechukua wasanii wenye uwezo mkubwa na sio majina na kuweza kufanya tamthilia hiyo miongoni ya tamthilia yenye viwango vya hali ya juu africa mashariki

Tuesday, January 15, 2013

BAADA YA UZINDUZI WA ALBUM YAO YA RISASI KIDOLE KUSHINDWA KUFANA KUTOKANA NA HUJMA KAMA WANAVYODAI SASA MASHUJAA KUFANYA UZINDUZI MWINGINE KWA AJILI YA KUITMBULISHA TENA ALBUM HIYO PAMOJA NA NYIMBO NYINGINE TATU MPYA ZA MWAKA 2013

MASHUJAA MUSICA BAND walifanya utambulisho wa album yao RISASI KIDOLE ndani ya ukumbi wa leaders  mwishoni mwa mwaka wa 2012 ambapo walisindikizwa na nguli wa muziiki africa J.B salvarola binadame shtuka baswahili ambapo uzinduzi huo uligubikwa na utata baada ya kila walipopanda jukwaani umeme ulikua unakatika kiasi chakupeleka kushindwa kupiga nyimbo zao zote
                              MENEJA MARTIN KULIA AKIWA MA MCD TUMBA
akiongea na blog hii meneja wa mashujaa musica MARTIN SOSPETER amesema kwa sasa wako kwenye mpango wa kufanya utambulisho rasmi wa album yao ya risasi kidole pamoja na kuanza kuiza siku hiyo ingawa hajasema ni lini ila amedokeza na kusema kuwa wanatarajia kufanya mwishoni mwa mwezi wa pili
AIDHA martini amesema kwa sasa anajipanga kuisuka tena band yake kwa kufanya usajili ingawa hajasema atawachukua wanamuziki gani lakini amesema hilo ni suprise ambayo ataifanya ndani ya mwaka huu wa 2013

Thursday, January 10, 2013

2013 KWELI UNA MAMBO NGULI WA TASNIA YA FILAMU ALIEGEUKIA MUZIKI SNURA MUSHI KAJIFUNGIA NCHINI KENYA,MOMBASA KWA AJILI YA KUJIANDAA NA SHOW ZA HIVI KARIBUNI ZA KIMUZIKI ZAIDI KUIBUKA NA NYIMBO MBILI KWA MPIGO DEBE LA VANGA NA MAJANGA ASEMA SASA NI MUZIKI NA FILAMU

MWANADADA anaetamba katika tasnia ya filamu kwa sasa na vile vile akiwa ameugeukia muziki na tayari anatamba na wimbo wake aliomshirikisha mcheza filamu mwenzie  WEMA SEPETU wa SHOGA YAKE MAMA amvbayo ipo kwenye mtindo wa mduara,snura ambae alikua rafiki wa karibu sana wa marehem hussein mkieti SHAROBARO amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake sehemu zote mbili ikiwa ni filamu pamoja muziki ili kuweza kujitengenezea kipato zaidi.
                                     SNURAH NA WEMA NA WIIMBO WA SHOGA
SNURAH amefunguka sababu ya kwenda kuweka kambi mombasa ni kuweka kuwa mbali na marafiki na kujikip busy zaidi na mazoezi kwa sababu mwaka huu amepanga mashambulizi zaidi katika muziki hivyo yeye na madancer wake wote wapo huko kwa ajili ya maandaliz ya show atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi wa pili pia.
                                              SNURAH KAZINI
Aidha snura amesema pindipo akirudi tu ataachia ngoma zake mbili ambazo watanzania watajua kipaji chake hali na hivyo wampokee na vibao kimoja atatoa audio na kingine video ambapo kimoja amekita MAJANGA NA KINGINE DEBE LA VANGA ambacho kapiga katika mtindo wa sebene, lakini vile vile amesema baada ya vibao hiyo kinachofuata ni album ambayo kwa kifupi ipo tayari lakini wako kwenye hatua za mwisho za kukamilisha.

TWANGA ACADEMIA YAANZA KUTOA MATUNDA,VICTORIA SOUND YACHUKUA MMOJA NI MTOTO WA KIKE ANAEAMINIKA KUWA MRITHI WA KINA LUIZA MBUTU,KHADIJA MNOGA,HALIMA NGALUMA NA WENGINEO WALIWAHI KUTAMBA KIPINDI HICHO

CYANA ni jina geni katika muziki wa dansi lakini ni kipaji kilichoibuka kutoka ndani ya twanga academia ambayo ilikua chini ya walimu wawili nyoshi el saadat na komando hamza kalala na ni band ambayo ipo chini ya aset club ambapo vile vile band hiyo ikiwa ni band dada ya twanga pepeta international ambao huwa ndi huwa wanatumbuiza mwanzo kabla na baada ya hapo band kuubwa hupanda na kuendelea na burudani,

CYANA ni msichana pekee aliweza kuingiza sauti katika wimbo wa twanga academia uitwao linda na kuonyesha kipaji cha hali ya juu na ndipo kocha muumini mwinjua alipokiona kipaji hicho na na alipoata mdhamini wa na kuweza kumpa band kuisimamia na kuiendesha ndipo alipoamua kumnyakua msichana huyo kutoka twanga academia na kuweza kuwa nae katika band yake hiyo ya victoria huku akisema kwa kuwa yeye ni mtu wa kuibua vipaji basi amepania kuweza kumtoa

CYANA kama vile alivyofanya kwa kina amina ngaluma japanese,kina chinese,na wengineo,
KWA mujibu wa cyana mwenyewe amesema kwa sasa anaona ndio safari yake ya mziki inaanza kwa kuweza kupata nafasi yaku fanya kazi na wasanii wakubwa na wenye uzoefu vile vile hivyo amepania kufanyamakubwa katika tasnia na medani ya muziki wakiafrica kwa ujumla.

na kwa sasa ndani ya victoria sound ameshapewa nafasi ya kuimba mabao atakuwepo kwenye wimbo mbili za mwanzo za victoria ikiwa ni SHAMBA LA BIBI,NA MAMA BAHATI.

Tuesday, January 8, 2013

ALIEAMINIKA KUZIBA PENGO LA KALALA JOUNIOR NDANI YA MAPACHA WATATU,JANUARY 11 ACHOMOKA NA KUTUA NDANI YA BAND MPYA YA VICTORIA SOUND ASEMA BADO MAPEMA KUELEZA KILICHOMTOA MAPACHA WATATU

JANUARY 11 si jina geni kwa mashabiki wa mapacha watatu na wadau wa muziki wa dansi alianza kuimba akiwa na mapacha watatu kama mwimbaji msaidizi kwa kuimba classico kabla ya mapacha kupanda lakini vile vile alianza kuimba kwa kufanya back up katika nyimbo tofautitofauti za mapacha watatu na alipoondoka kalala jounior yeye ndie alikua akiziimba verse za kalala ndani ya mapacha watatu,lakini pai january alikwishaanza kuimba baadhi ya nyimbo za mapacha watatu ambapo kwenye nyimbo yao ya mwisho kuiachia ya CHANZO MWANAUME januari aliweza kusikika na kuonyesha kipaji chake halisi.
                                   JANUARY ELEVEN WA KWANZA KULIA
Januari ambae leo ataweka bayana katika kipindi cha extra africa na kuweka kile kilichomtoa mapacha watatu na kujiunga na band mpya ya victoria sound ambayo ipo chini ya nguli wa muziki wa dansi PRINCE MUUMINI MWINJUMA ambayo imeweka kambi yake mkoani mtwara kwa ajili ya kuandaa nyimbo ambazo watakwenda kuzirekodi hivi karibuni
                                 JANUARY ELEVEN ALIETUA VICTORIA SOUND

MWIMBAJI MKONGWE WA DIAMOND MUSIC INTERNATIONAL JUICE YA MACHUNGWA KUIBUKA NA ALBUM YKE YA YA YATAKA MOYO AACHIA SINGLE AKIWA AMEMSHIRIKISHA BWANA MISOSI ASEMA DIAMOND MUSICA BADO IPO LAKINI BISI NDIO HAKUNA ASEMA HAKUNA DIAMOND BILA YEYE AU ALAIN MULUMBA ALIEANZISHA DIAMOND NYINGINE SIO ORIGINAL NI FAKE

Baaada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kufanya show lakini wakiwa wametoa nyimbo zinazofanya vizuri radio kama supu ya kongoro na abdul karimu lakini pia waliweza kutamba na wimbo wao wa mapenzi kitu gani mwanamuziki mmmoja kati ya waliokua wanaunda diamond musica international JUICE YA MACHUNGWA aibuka na kusema kwa mwaka 2013 amejipanga kupakua album yake binfsi alioipa jina la yataka moyo huku akiwa ametanguliza sokoni wimbo wake wa kivuli ambapo project yake hiyo anaifanya chini ya udhamini wa mtu aliejitolea baada ya kuona kipaji chake katika music wimbo huo akiwa amemshirikisha mwanamuziki wa kizazi kipya BWANA MISOSI AMBAE HUMO NDANI AMEEIMBA BADALA YA KURAP NI NYIMBO ILIYOKATIKA MAHADHI YA ZOUK RHUMBA.
                                                       JUICE YA MACHUNGWA
Aidha juice ya machungwa amefafanua kuhusu kuwepo kwa DIAMOND MUSICA mbili amesema kuwa diamond musica ni moja tu ambayo yupo yeye JUICE YA MACHUNGWA.ALAIN MULUMBA,KATANYAMA,SAUTI YA RADI LIVER HASSAN hiyo ndio diamond musica ila hyi iliyoanzishwa kwa sasa yeye haifahamu na kusema kuwa wanatumia jina hilo vibaya na kujiingizia kipato wakati diamond yenyewe bado ipo ila bosi ndio tatizo sio wanamuziki kwa hiyo pindipo watakapo pata mdhamini basi wataweza kurudi kama zamani.

Monday, January 7, 2013

BAADA YA KUTIKISA NA WASANII WACHANGA KATIKA FILAMU YA MAJANGA 2012 DK CHENI APANGA KUTAFUTA VIPAJI KUSINI VYA KUFANYA NAE KAZI YA FILAMU NYINGINE ITAKAYOKUJA ASEMA SASA NI MWAKA WA KUIBUA VIJAPI VILIVYOJIFICHA MIKOANI

GWIJI na nguli wa maigizo tanzania MAHSAN AWADH almaarufu kama DK,CHENI amesema aliamua kuwashirikisha wasanii wasio na majina katika movies yake ya majanga ili kuwaonyesh watu kuwa kuna vipaji ambavyo havipewi kipaumbele lakini wana uwezo mkubwa kufanya kazi huku akitolea mfano wa mzee ambae ameigiza kama baba yake katika movies ya majanga na kusema wengi walikua hawajui ni jinsi gani wataweza kumtumia mzee huyo kwenye filamu zao lakini kwa ukongwe wake ameweza kufanya hivyo na amefanya vizuri kushinda vile ambavyo alifikiria na kuipendezesha movies yake vile alivyotarajiwa.
                                                    DK CHENI
DK CHENI amesema baada yakufanya hivyo sasa ameamua kufanya kazi na wasanii chipukizi kwa kuwa wanajua kile wanachokifanya na hivyo baada ya kupakua filamu yake ya hukumu ambayo ndani atawashirikisha wasanii aliofanya nao katika majanga ataanda filamu nyingine ambayo atafanya na wasanii ambao atakuja kufanya search ya wasanii wanaochipukia ili kuweza kufanya nae filamu ambayo anaamini kwa usongo waliokua na wasanii wa mikoani ambao wakipata nafasi wataweza kuonyesha uwezo zaidi ili waweze kutoka na kuwa mastar katika filamu na tasnia ya uigizaji kwa ujumla.

SUPER NYAMWELA KUFUNGUA CHUO CHA KUFUNDISHA MADANCER ILI KUWAJENGA NA KUFANYA IWE KAZI YENYE PROFESIONAL,AANDAA PROJECT YA ALBUM YAKE NA AMINI T.H.T

DANSA aliejizolea umaarufu kutokana na uchezaji wake ambae pia alishawahi kuwa bingwa wa africa mashariki ambae kwa sasa anafanya kazi na band ya EXTRA BONGO akiwa kama muimbaji,mchezaji mtunzi wa show na baadhi ya nyimbo za extra bongo lakini pia ni muimbaji wa nyimbo za kiafrica na bongo flever pia amesema mwaka 2013 anataka kuufanya tofauti zaidi baada ya kuwaza kufungua chuo cha madansa ambapo atakua anawafundisha style mbalimbali za uchezeji ikiwa n bolingo,funky,hip hop na nyingine nyingi ili kuweza kutoa ajira kwa vijana kutokana na vipaji vyao.
                                             MIMI NA SUPER NYAMWELA
Aidha amesema kuwa ameamua kufanya ivo baada ya hsia za watu kuwa kazi ya udansa ni ya kubahatisha tu na hailipi ila anasema yeye toka alipotoka na mafaniko aliyokua nayo yanatokana na kazi yake ya show ambapo kwa ana mke na watoto wanaomtegemea kutoka na kazi yake hiyo na kusema itabidi vijana pia waeze kijikwamua kutokana na kazi hiyo isionekane kuwa ni kazi yawatu waliokosa kazi bali kazi kama kazi nyingine tu ambazo znaendesha maisha ya mwanadamu ya kila siku
                                         NYAMWELA KATIKA AKIWA KAZINI
LAKINI pia nyamwela amsema kwa mwaka 2013  amewaandalia mashabiki wake kazi nzuri ya solo akiwa na amin wa t.h.t ambapo wameshatengneza wimbo mmojawalioupa jina la kivuli ambapo video na oudio tayari vimeshatoka na kabla ya mwezi wa pili ataweza kuachia singo nyingine ambayo itafuatiwa na album ambayo ataitambulisha jina lake pindi itakapo kamilika.

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...