WAY

Thursday, January 17, 2013

KINARA WA SIRI YA MTUNGI NA FILAMU YA MAGIC MONEY AFUNGUKA NA KUSEMA MASUPER STAR NA WASAMBAZAJI WANACHANGIA UBOVU WA FILAMU KWA KUANGALIA NANI AMEFANYA NA SIO KIWANGO CHA MOVIES KIKOJE

KINARA anaetamba katika tamthilia ya SIRI YA MTUNGI na filamu yake ya MAGIC MONEY amesema kuna baadhi ya wasanii wakubwa ambao wameshaona game ni yao na hivyo wanaanda movies bora mradi movies na kuziingiza sokoni bila kujali stori wala quality za filamu kwa kujua watanzania ashajua wao ndio waigizaji na pia wasambaji ndio wanazitaka sana filamu za wasanii hao wakubwa matokeo yake unakuta kila mwezi filamu sokoni wakati swala hilo kikawaida haliwezekani na matokeo yake ndio filamu zinazoingia sokoni ni zilizile wakati kuna watu wanaofanya vizuri zaidi ya hao wengine.

aidha daudi ameongeza kuwa sasa imefika wakati kwawatanzania kuchagua kipi bora na baadhi ya watanznia washafunguka akili zao na kuanza kufatilia kipi bora kipi kibaya na mwisho wa siku wale wababishaji katika tasnia watabainika na kurudi chini kutokana na kufanya filamu bora zimefanyika bila kuwajali watanzania ambao ndio wateja.

DAUDI ambae yupo ndani ya tamthilia ya siri ya mtungi ambayo inaonyeshwa kwenye tv mbili ITV NA CHANEL FIVE amesema kwa hiyo ni tamthilia ya aina yake ambayo ni ya kipekee iliyokuja kufanya mapinduzi katika asnia ya uigizaji kutoka na waandaji wake kuwa na uwezo mkubwa na imechukua wasanii wenye uwezo mkubwa na sio majina na kuweza kufanya tamthilia hiyo miongoni ya tamthilia yenye viwango vya hali ya juu africa mashariki

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...