WAY

Monday, January 7, 2013

BAADA YA KUTIKISA NA WASANII WACHANGA KATIKA FILAMU YA MAJANGA 2012 DK CHENI APANGA KUTAFUTA VIPAJI KUSINI VYA KUFANYA NAE KAZI YA FILAMU NYINGINE ITAKAYOKUJA ASEMA SASA NI MWAKA WA KUIBUA VIJAPI VILIVYOJIFICHA MIKOANI

GWIJI na nguli wa maigizo tanzania MAHSAN AWADH almaarufu kama DK,CHENI amesema aliamua kuwashirikisha wasanii wasio na majina katika movies yake ya majanga ili kuwaonyesh watu kuwa kuna vipaji ambavyo havipewi kipaumbele lakini wana uwezo mkubwa kufanya kazi huku akitolea mfano wa mzee ambae ameigiza kama baba yake katika movies ya majanga na kusema wengi walikua hawajui ni jinsi gani wataweza kumtumia mzee huyo kwenye filamu zao lakini kwa ukongwe wake ameweza kufanya hivyo na amefanya vizuri kushinda vile ambavyo alifikiria na kuipendezesha movies yake vile alivyotarajiwa.
                                                    DK CHENI
DK CHENI amesema baada yakufanya hivyo sasa ameamua kufanya kazi na wasanii chipukizi kwa kuwa wanajua kile wanachokifanya na hivyo baada ya kupakua filamu yake ya hukumu ambayo ndani atawashirikisha wasanii aliofanya nao katika majanga ataanda filamu nyingine ambayo atafanya na wasanii ambao atakuja kufanya search ya wasanii wanaochipukia ili kuweza kufanya nae filamu ambayo anaamini kwa usongo waliokua na wasanii wa mikoani ambao wakipata nafasi wataweza kuonyesha uwezo zaidi ili waweze kutoka na kuwa mastar katika filamu na tasnia ya uigizaji kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...