WAY

Thursday, January 10, 2013

2013 KWELI UNA MAMBO NGULI WA TASNIA YA FILAMU ALIEGEUKIA MUZIKI SNURA MUSHI KAJIFUNGIA NCHINI KENYA,MOMBASA KWA AJILI YA KUJIANDAA NA SHOW ZA HIVI KARIBUNI ZA KIMUZIKI ZAIDI KUIBUKA NA NYIMBO MBILI KWA MPIGO DEBE LA VANGA NA MAJANGA ASEMA SASA NI MUZIKI NA FILAMU

MWANADADA anaetamba katika tasnia ya filamu kwa sasa na vile vile akiwa ameugeukia muziki na tayari anatamba na wimbo wake aliomshirikisha mcheza filamu mwenzie  WEMA SEPETU wa SHOGA YAKE MAMA amvbayo ipo kwenye mtindo wa mduara,snura ambae alikua rafiki wa karibu sana wa marehem hussein mkieti SHAROBARO amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake sehemu zote mbili ikiwa ni filamu pamoja muziki ili kuweza kujitengenezea kipato zaidi.
                                     SNURAH NA WEMA NA WIIMBO WA SHOGA
SNURAH amefunguka sababu ya kwenda kuweka kambi mombasa ni kuweka kuwa mbali na marafiki na kujikip busy zaidi na mazoezi kwa sababu mwaka huu amepanga mashambulizi zaidi katika muziki hivyo yeye na madancer wake wote wapo huko kwa ajili ya maandaliz ya show atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi wa pili pia.
                                              SNURAH KAZINI
Aidha snura amesema pindipo akirudi tu ataachia ngoma zake mbili ambazo watanzania watajua kipaji chake hali na hivyo wampokee na vibao kimoja atatoa audio na kingine video ambapo kimoja amekita MAJANGA NA KINGINE DEBE LA VANGA ambacho kapiga katika mtindo wa sebene, lakini vile vile amesema baada ya vibao hiyo kinachofuata ni album ambayo kwa kifupi ipo tayari lakini wako kwenye hatua za mwisho za kukamilisha.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...