WAY

Thursday, January 31, 2013

KITALE AHOFIA KUONDOKA DUNIA BILA KUOA SASA KUFUNGA NDOA JUMAPILI ASEMA PIA NI KATIKA KUMUENZI SHAROMILIONEA AMBAYE ALIKUA RAFIKI YAKE MKUBWA NA WALIPANGA KUFUNGA NDOA SIKU MOJA ILA MUNGU NAE ALIPANGA YAKE

MCHEKESHAJI NA MSANII WA BONGO FLEVER KITALE amesema panapo maajaliwa jumapili ya tar 3.01.2013 atafunga ndoa huku akiongeza kwa kusema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na maisha ya sasa kubadilika lakini pia hata maagzo ya mwenyezi mungu pia yanasema hivyo kwa sasa ameona ni bora aoe lakini sababu nyingine anasema ameamua kuoa kwa sababu ya kumuenzi  rafiki yake kipenzi MAREHEM HUSSEIN MKIETI almaarufu kama SHARO MILIONEA ambaye walipanga kufunga ndoa siku moja ya tar 14.02.2013 lakini mungu nae anamipango yake aliamua kumchukua na hivyo na yeye akaona bora awahi kuoa kama walivyopanga na rafiki yake.
                                                   KITALE TEJA AKIWA KAZINI
kitale amesema pia wasanii wengi huwa wanalisahau hilo kwa kuendekeza starehe huku wakijua kuwa wananafasi kubwa ya kuwa mifano bora katika jamii kwa kufuata yale yaliyo bora zaidi huku akisema tabia za wasanii wengi huwazinakua haziwafurahishi wanajamii na ndio hata kilichotokea kwa mke wake huyo mtarajiwa kuwachukia sana wasanii lakini mwisho wa siku alimuona kitale yupo  tofauti nawasanii wengine ndio maana hata wakifikia hatua ya kutarajia kufunga ndoa hiyo siku ya jumapili.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...