WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Wednesday, April 8, 2015

MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO WATISHIA KUGOMA IJUMAA KWA MADAI YA KUFANYIA UNYANYASAJI

   Mabasi ya Abiria yakiwa yamepaki stand kusubiri

Madereva wa vyombo mbali mbali vya moto nchini Tanzania, wanakusudia kushiriki mgomo wa nchi nzima siku ya Ijumaa wiki hii, kuishinikiza serikali kuondoa kero mbali mbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika pamoja na agizo la kutaka madereva hao waende kusoma kila wanapotaka kuhuisha leseni zao za udereva.

Wakizungumza kupitia Katibu wa Muungano wa vyama vya Madereva Bw. Rashid Saleh, madereva hao wamesema kuwa suala la kurudia kusoma ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kibao kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali nchini.

Katibu huyo wa Muungano wa Vyama vya Madereva ameitaja kero nyingine kuwa ni hatua ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kutamka hadharani kuwa vyeti walivyonavyo madereva hao sio halali na kwamba Ijumaa wiki hii wanakusudia kukutana na Waziri wa Kazi na Ajira kwa ajili ya kuzungumzia kero hizo kwa lengo la kuepusha kutokea kwa mgomo huo.

Monday, March 30, 2015

MUGABE AWATAKA VIONGZI WA AFRIKA KUACHA KUWA VIBARAKA WA MATAIFA YA ULAYA NA MAGHARIBI NA WAJISHUGHULISHE KUINUA WANANCHI WAO



     Rais wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe
Rais wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe amewataka viongozi wa nchi za Africa kukataa kuwa vibaraka wa mataifa tajiri duniani na badala yake wajitoe katika kuwatumikia waafrika ili kufikia mafanikio ya kimaendeleo katika ustawi wa bara hili.

Rais Mugabe ametoa mwito huo wakati akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa viongozi Vijana kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika na China unaofanyika katika ukumbi wa mikotano wa Ngurdoto nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo Rais Mugabe ametumia muda mwingi kuwaasa na kutoa mwito kwa viongozi hao vijana akisistiza kuwa Bara la Afrika linategemea mchango wa Fikra zinazojali uwajibikaji na nidhamu ya hali ya juu katika utumishi.

Awali akizungumza katika Mkutano huo,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Kikwete ameonyesha imani aliyoanayo kupitia mkutano wa viongozi vijana kutoka Afrika na Uchina kwamba utatoa fursa ya kutoka na maazimio yatakayokuwa na tija kwa mustakabali wa watu wote

Tuesday, March 24, 2015

SERIKALI KUTUNGA CHOMBO CHA KUCHUNGUZA, KUPEKUA NA KUKAMATA WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA


            Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh. Jenista Mhagama
Serikali leo imewasilisha mswada wa sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za Kulevya ya mwaka 2014, kutokana na tatizo hilo kuongezeka zaidi kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kutishia uhai wa taifa kutokana na vijana wengi kujiingiza katika biashara na matumizi ya dawa hizo.

Akiwasilisha mswada huo Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge Mh. Jenista Mhagama amesema matumizi ya dawa za kulevya yameongezeka ambapo takwimu zinaonyesha kuwa watumiaji wa dawa hizo kati ya laki mbili na 20 hadi laki nne na 20 hapa nchini wengi wakiwa ni vijana kati ya miaka 15 hadi 38.

Mh. Mhagama amesema ili kurekebisha matatizo ya kimfumo katika udhibiti ya dawa hizo serikali imekusudia kuanzisha chombo kinachojitegemea chenye mamlaka ya kiutendaji ya kuchunguza, kupekua na kukamata watuhumiwa tofauti na ilivyo tume kwa sasa.

Friday, March 6, 2015

WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUWAUA WATU WATANO KWA KUWATUHUMU WACHAWI


     Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, Philip Kalangi akizungumza na wanahabari
Jeshi la polisi mkoa wa mara limewakamata watu saba wakiwemo viongozi wawili wa serikali ya kijij cha park nyigoti katika kata ya ikoma wilayani serengeti mkoani mara baada ya kutuhumiwa kuwakamata na kuwafunga vitambaa usoni watu wanane wanaowatuhumu kwa uchawi kisha kuwachapa viboko na kusababisha vifo vya watu watano.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mara,kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Acp Ernest Kimola,amesema katika tukio hilo ambalo limesababisha watu wengine watatu kujeruhiwa kwa kuchapwa viboko hivyo na kulazwa katika hospitali teule ya nyerere ddh mjini mugumu wilayani serengeti.

Mbali na mwenyekiti na mtendaji wa serikali ya kijiji hicho kukamatwa pia viongozi wawili wa jadi wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo

nao baadhi ya ndugu wa marehemu wameelezea jinsi unyama huo ulivyotekelezwa kwa kisingizio cha ushirikinai

hadi sasa askari wa jeshi la polisi kutoka makao makuu ya mkoa wa mara kwa kushirina na polisi mjini wilayani serengeti wanaendesha na operesheni kali katika kuwasaka watu wote walihusika kufanya mauaji hayo ya kinyama.

Tuesday, March 3, 2015

VIKONGWE WAUAWA MKOANI DODOMA KWA TUHUMA ZA USHIRIKINA ETI WANAZUIA MVUA ISINYESHE MAENEO YAO


     Kamanda wa Jeshi la Polisi Dodoma David Misime
Vikongwe watatu akiwemo mganga wa kienyeji Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma, wameuawa kwa tuhuma za kuzuia mvua isinyeshe Wilayani humo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kamanda wa polisi mkoa wa Dodma, David Misime inasema kuwa tukio la kwanza lilitokea Machi mosi mwaka huu majira ya saa saba usiku katika kitongoji cha Golani, kijiji cha Masinyeti, kata ya Iduo, tarafa ya Mlali.

Kamanda amesema katika tukio hilo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Saidia Chakutwanga (80) ambaye ni mganga wa kienyeji aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kutobolewa macho.

Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina wakimtuhumu marehemu kuwa anazuia mvua kunyesha katika eneo hilo.

Katika tukio lingine amesema tarehe hiyo hiyo majira ya saa nane usiku kwenye kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda Kata na Tarafa ya Mlali mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Peter Kaluli (85) akiwa na mkewe aitwaye Kaila Kaluli (80) wakazi wa kitongoji cha Majengo wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao ya tembe, waliuawa na watu wasiofahamika kwa kuangushiwa ukuta wa nyumba yao kisha kuchoma moto na kubomoa nyumba mbili za tembe.

“Watu hao walifanya uharibifu mwingine kwa kuwaua nguruwe mmoja na ng’ombe mmoja kumkata miguu ambao ni mali za marehemu hao,” alisema Misime.

Kwa mujibu wa Kmanda uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji na uharibifu huo ni imani za kishirikina wakiwatuhumu marehemu kuwa wanazuia mvua kunyesha.

Kutokana na tukio hilo watu wanne akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihanda na wazee wawili wa kimila wa kijiji wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo kwani taarifa zinaonyesha waliandaa vikao vya kutekeleza mauaji hayo.

Upelelezi wa matukio yote mawili unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika na matukio haya ili sheri aiweze kuchukua mkondo wake.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa amewataka viongozi wa dini mkoani hapa kuhubiri amani kwa waumini wao ili vitendo vya mauaji kwa vikongwe viweze kukomeshwa.

Monday, March 2, 2015

HATUA KALI ZINAFUATA JUU YA WAUAJI WA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI TAYARI ADHABU YA KIFO ISHATOLEWA KWA BAADHI YAO-KIKWETE


         Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikweteamesema kuwa Serikali haitafumbia macho suala la mauaji ya walemavu wa ngozi kama hali ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.

Akiongea katika Hotuba yake kwa wananchi kwa kila mwisho wa mwezi Rais Kikwete amesema kuwa matukio hayo ambayo yaliibuka mwaka 2006 Serikali iliweza kukabiliana nayo na mpaka kufikiwa mwaka 2011 kukawa hakuna tukio lolote la mauaji ya watu hao.

Aidha rais Kikwete ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwafichua watu wote wanajihusisha na biashara ya viungo vya watu wenye Albinsim ili kwa pamoja kukomesha mauaji ya watu hao.

Kikwete amesema ni ujinga uliokithiri kwa mtu kutegemea ushirikina hasa kuwa na viungo vya ulemavu wa ngozi ndio kuna kufanya mafanikio katika shughuli zao hivyo kutaka juhudi zifanyike kueleimisha juu ya kuacha watu kuamini imani potofu.

Aidha Rais Kikwete amesema atakuata na watu wenye Ulemavu wa ngozi wiki ijayo ili kusikiliza maoni yao juu ya nini kifanyike katika kusaidiana kukomesha mauaji dhidi yao.

Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete amesema kazi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchini kwa kutumia mfumo wa BVR katika Halmshauri ya Makambako mkoani Njombe imevuka lengo la tume hivyo kulazimu kuongeza muda ili wananchi wote waliojitokeza waweze kujiandikisha.

Tume ilitegemea kuandikisha wapiga kura 9541 katika halamashauri hiyo lakini kutokana na mwitikio wa wananchi wameandikishwa watu 13.042.

Aidha Rais Kikwete amewataka viongozi wa vyama vya siasa,Serikali,dini na asasi za kiraia kuungana na tume katika kuwahamasisha wananchi kujiandikisha badala ya kuwachanganya kwa kutoa taarifa zisizo za kweli.

ETI TANESCO WAMESEMA WATALETA MFUMO MWINGINE WA KUNUNUA LUKU BAADA YA TATIZO LA MITANDAO KUKOSA NETWORK YA KUNUNUA UMEME

Meneja Mawasiliano wa Tanesco Adrian Mvungi
Wakazi na wajasiriamali wa jiji la Dar es salaam wamelilalamikia Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanesco baada ya Mtandao wa kuuza umeme kwa njia ya Luku kugoma kufanya kazi toka juzi usiku,

Wakizungumzana kutoka makao makuu ya Tanesco Ubungo jijini Dar es salam huku wakiwa na jazba wamesema biashara zao zimehathirika sana na kuwa sababishia hasara kutokana na kushindwa kununua Umeme kwa njia ya Luku huku biashara zao zikitegemea umeme wakati wote,

Kwa Upande wake Meneja mwandamizi Teknolojia ya Habari na mawasiliano wa Tanesco Kusenha A. mazengo amesema wamelifanyia kazi tatizo hilo na kuhaidi hivi karibuni wataleta mfumo mpya wenye njia mbadala wa kununua Umeme,

Wakati huo huo Meneja Mawasiliano wa Tanesco Adrian Mvungi amewaomba radhi wateja wao kwa usumbufu walioupata na kuhaidi kutorudia tena.

Friday, February 27, 2015

KILIMANJARO INAONGOZA KWA UKATILI WA KIJINSIA

 Wajumbe wa SHIVYAWATA baada ya kutoka Ziarani Austaria
VYAMA vya Watu wenye ulemavu nchini, wanakusudia kuishitaki serikali kwenye vyombo vya kimataifa, endapo mauaji ya watu wenye ulemavu wangozi (Albino) yataendelea.



Akizungumza leo kwenye warsha ya ujumuishaji wa watu wenye ulemavu, katika nyanja za maendeleo iliyowezeshwa na EDAN ambayo ni programu ya Jumuiya ya Makanisa Duniani, Mshauri wa mradi wa watu wenye ulemavu, kuhusu haki na maendeleo yao,Dk. Elly Macha amesema Tanzania imesaini

mkataba wa kutetea haki za watu wenye ulemavu,lakini imeshindwa kuwalinda na matokeo yake wanauwawa ovyo.



Amesema kuwa hali ya mauaji ikiendelea kuwa kama ilivyo sasa, wataelewa wazi kuwa serikali imewaacha peke yao na watalazimika kwenda kwenye vyombo vya kimataifa kuishtaki serikali kw akushindwa kuheshimu mkataba huo.



Aidha amesema kuwa mbali na hilo katika warsha hiyo wamkubaliana na kutoa wito kwa serikali kusimamia,kuelekeza, kutekeleza na kufuatilia ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika nyanja za maendeleo hususani, kuhakikisha sera,sheria, mipango na upatikanaji wa rasilimali unawezesha ujumuishaji wa masuala hayo.



Dk.Elly amesema kupitia warsha hiyo wametoa tamko la kulaani mauaji ya kinyama ya Albino yanayoendelea kutekelezwa kw akasi, hasa kanda ya ziwa na kuitaka serikali kuchukua hatua madhubuti kukomesha tatizo hilo.



Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude, amesema kuna kesi nyingi zimeamuliwa na wengine wamehukumiwa kunyongwa, ila mpaka sasa hakuna aliyenyongwa wapo magerezani,hivyo wanaomba hukumu ikitolewa

izingatiwe, kwani isionee huruma wahusika hao wanaoua wenzao kama wanyama.

Thursday, February 26, 2015

JELA MIAKA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MINNE

 Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yusufu Chatambala (45) mkazi wa Kijiji cha Makutupa Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.

Mwendesha mashtaka wa polisi Godwill Ikema ameiambia mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Feb 20 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Makutupa kilichopo Wilayani Mpwapwa ambapo alimbaka mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka minne

Mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sheria za nchi chini ya Kifungu namba 130 (1) 2 (a) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu kama kilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.

Amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumkamata alipokuwa akicheza na watoto wenzake jirani na nyumbani kwao kisha kumpeleka kwenye shamba la mahindi kisha kumbaka mtoto huyo na kusababishia majeraha na maumivu makali.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Paschal Mayumba alimtia hatiani mtuhumiwa huyo leo baada ya kukiri kutenda kosa hilo.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mayumba amesema Mahakama inamhukumu kwenda jela kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka mtoto ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wanaotenda makosa kama hayo.

MAHAKAMA KUU YAKALIA SHAURI LINALOTAKA SERIKALI KUTOA ULINZI KWA JAMII YA ALBINO.

 Mkurugenzi wa kituo cha haki za Binadamu Helen-Kijo Bisimba
Mahakama Kuu ya Tanzania imeshindwa kusikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kipindi cha miaka saba iliyopita,

shauri ambalo kituo hicho kinaitaka mahakama iilazimishe serikali kutoa ulinzi wa uhakika kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini maarufu kama albino.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, amesema hayo leo katika mahojiano na East Africa Radio na kufafanua kuwa kuchelewa kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa namna moja inaweza kuwa imechangia kuzorota kwa usalama dhidi ya jamii ya albino nchini.

Kwa mujibu wa Dkt. Bisimba, matukio ya ukatili dhidi ya albino nchini yanayoendelea hivi sasa yanahitaji mbinu na njia nyingi katika kukabiliana nayo, mojawapo ikiwa ni ulinzi wa uhakika kwa jamii hiyo ya Watanzania.

CHANGAMTO ZAENDELEA KULIKUMBA ZOEZI LA UANDIKISHAJI BVR, WANANCHI WAGOMEA MASHINE MPYA, UMEME WAKATIKA VITUO VYAFUNGWA MAPEMA KWA MASHINE KUKOSA CHAJI


     Mashine ya kisasa ya kujiandikisha kitambulisho cha kura
Uandikishwaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura Mkoani Njombe nchini Tanzania leo asubuhi lilisimama kwa muda katika baadhi ya vituo kutokana na wananchi kuzigomea mashine mpya zilizoongezwa kwa ajili ya Uandikishaji.

Akizungumza na East Africa Radio msimamizi wa mashine za BVR, Astori Mgwame amesema kuwa wananchi hao waligomea mashine hizo kwa kuwa zilikua hazina muendeshaji wa kuziendesha kwa ufasaha na kusema kuwa hawatajiandikisha mpaka wahakikishiwe kuwa kuna mtaalamu wa kuzitumia.

Mgwame ameongeza kuwa hali hiyo inatokana na changamoto waliyokuwa nayo ya kuwa na upungufu wa wa wataalamu wa kuziendesha mashine hizo hivyo kufanya zoezi kuenda taratibu kushinda ilivyotarajiwa.

Aidha amesema changamoto nyingine iliyojitokeza jana jioni mpaka kupelekea kufungwa kwa vituo hivyo mapema kabla ya wakati ni kukatika kwa umeme na mashine kuishiwa chaji na kuzima hivyo kushindwa kuendelea na zoezi hilo.

Mgwame amesema kuwa licha ya changamoto hizo kujitokeza lakini uandikishwaji huo bado unaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi ili kuweza kupata haki yao hiyo ya kujiandikisha.

ASKARI WATANO WAJERUHIWA VURUGU ZA IRINGA KATI YA ASKARI NA WANANCHI



     Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi
Askari watano wamejeruhiwa kufuatia vurugu zilizotokea  baina ya jeshi la polisi pamoja na wananchi katika mji wa Ilula kijiji cha dinginayo wilaya ya kilolo mkoani iringa pamoja na raia wawili kujeruhiwa.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi PUDENSIANA PROTAS amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tayari jeshi la polis linawashikilia watuhumiwa kumi na nane kwa mahojiano huku upelelezi ukiendelea.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 4 asubuhi na limesababisha kifo cha mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la mwanne mtandi na katika vurugu hizo kumesababisha uharibifu wa mali za jeshi la polisi ambayo ni gari,pikipiki pamoja na gari moja ambayo ilikuwa ni kielelezo katika kituo pamoja na kuharibu jingo la polis kwa kuvunja vioo.

Aidha kamanda amesema kuwa fujo hizo zilisababishwa na oparationi kuhusu uuzaji wa pombe za kienyeji na makosa mbalimbali kwa wananchi huku akiwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi ili kuepusha majanga kama hayo.

WATU KADHAA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MWANZA KWA TUHUMA ZA UTEKAJI WA MTOTO MWENYE ULEMAVU PENDO EMANNUEL


                             Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw. Magesa Mulongo
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw. Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika kumuiba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel mwenye umri wa miaka 4 katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza, Disemba 27 wamekamatwa.

Akizungumza leo wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya wa mkoa huo, Bw. Mulongo amesema watu wote waliohusika wamekamatwa na hivi sasa bado hawafahamu kama mtoto huyo yupo hai ama mfu.

Amesema kuwa wezi baada ya kumuiba mtoto Pendo walimleta katika hoteli moja Jijini Mwanza, kisha kuwakabidhi watu walionekana wanunuzi, lakini wote hao wamekamatwa akiwamo mmiliki wa hoteli hiyo.

Hata hivyo, amesema watu hao waliofanya uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mwisho aliyetoweka na mtoto huyo toka hotelini hapo akiendelea kutafutwa
 
Hata hivyo, alisema watu hao waliofanya uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mwisho aliyetoweka na mtoto huyo toka hotelini hapo akiendelea kutafutwa.

Mulongo hata hivyo hakuweza kuitaja hotel wala mmiliki wake na wangine waliohusika na tukio hilo lilitokea Desemba 27 mwaka jana, lakini Shilinde akituhumiwa kuhusika zaidi na tukio hilo kutokana na kuamua kufanya hivyo kwa sababu alikuwa ana watoto wawili albino.

Mkuu wa mkoa huyo aliwataka wakuu wa wilaya wapya, kuhakikisha kushughulikia changamoto za wapiga ramli, kuangalia utoaji wa vibali kwa waganga wa jadi ili kudhibiti matyukio ya utekaji na mauaji ya albino.

Hata hivyo, alishangazwa na maneno yanayotolewa na watu kuhusiana na mauaji hayo kuwa yanatokana na masuala ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mwanza, Mashaka Tuju, aliishutumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua stahili tangu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yalipoanza miaka tisa iliyopita.

Amesema kwa miaka tisa serikali inahangaika na kudai inachukua hatua lakini hakuna hatua yoyote inayoonekana mpaka sasa huku albino wengi wakiwa wanaishi vijijini katika nyumba zisizo na ulinzi thabiti, lakini utakuta viongozi wa serikali wanaenda huko pale linapotokea tatizo la mauaji ya watu hao.

Tuju amewashambulia mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Antony Diallo, naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga na mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu, kwa kushindwa kufanya juhudi zozote za kuwalinda na kuwatetea albino.

Katika kipindi cha miezi miwili, watoto Pendo Emmanuel wa Kwimba na Yohana Bahati (mwaka mmoja) wa kijiji cha Ilelema Chato, walitekwa na watu wasiojulikana.

Wednesday, February 25, 2015

WANAWAKE WANASHINDWA KUTAMBA KATIKA MUZIKI KUTOKANA NA UKIRITIMBA ULIOPO KATIKA TASNIA


         Deborah Nyangi akiitumikia Kalunde Band.
Mwanadada anaetamba na Band ya Kalunde Band, Deborah Nyangi ambae anatikisa na wimbo wake wa FINGO amesema wanawake wanashindwa kutamba katika game la muziki wa kizazi kipya kutoka na ukiritimba uliopo katika tasnia.

Nyangi amesema anaamini kuna vipaji vingi sana vya kuimba kwa watoto wa kike ila tayari wameshajenga woga wa kujitokeza kutokana na kuamini kwamba ukitaka kufanya vizuri lazima uhonge kama sio pesa basi hata kutumia mwili wake.

Nyangi ambae kwa sasa anajipanga kuachia wimbo wake mpya amewataka watoto wa kike wajiamini kwa kile wanachokifanya na wasikubali kuyumbishwa na watu wachache ambao wanajihisi wameshikilia game ila kazi nzuri ndio itawafikisha wanapotaka.

Tuesday, February 24, 2015

HAJI RAMADHANI AIBUKA NA BABY LOVE ASEMA ANAAMINI ITALETA MAPINDUZI KATIKA TASNIA YA MUZIKI ATAMBA KUACHIA NYIMBO BAADA YA NYIMBO

                
                  Haji Ramadhani Makuke akiwajibika Jukwaani
Msaanii wa Kizazi kipya alitokea kwenye mashindano ya kuibua vipaji Bss na sasa anatamba na band ya Twanga Pepeta Haji Ramadhani Makuke amekuja na ujio mpya wa kazi nje ya band yake na kuachia Singo mpya alioipa jina mpya la BABY LOVE.

Haji amesema nyimbo hiyo ina vionjo vya kiasili amesema ameitoa ili kuwaonyesha watanzania kipaji kingine tofauti katika uimbaji na pia kuleta ladha mpya katika muziki wa kizazi Kipya.

Hajji amesema ameamua kufanya kazi kwenye band na nje ya band kama Solo ili kujiongezea mashabiki na pia kubadilisha ladha ya mziki ila pia kujitafutia kipato kutokana kuuza nyimbo kwa mtindo wa singo kwa kuwa album kwa sasa ni ngumu kuuzika.

Monday, February 23, 2015

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO KUFICHUA MAUAJI YA ALBINO

                          Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano

 Waandishi wa habari nchini, wametakiwa kutumia kalamu zao kufichua chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, ambao umeibuka kwa kasi kubwa siku za karibuni.

Akizungumza leo Mjini Moshi na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, (TAMWA),kwa lengo la kufichua ukatili wa kijinsia, Mshauri wa vyombo vya habari, Deo Peter, alisema kuna hajana ya kufichua chanzo cha mauaji hayo.

Amesema inasikitisha kuona watu hao wanaendelea kuuwawa kikatili, huku waandishi wakijikita kuandika tu jinsi wanavyouwawa, bila kufanya utafiti kujua chanzo cha mauaji hayo ni nini, jamo ambalo halisaidii kukomesha kiini cha mauaji hayo.
 
Aidha amesema sambamba na hilo pia hata kwenye seuala la ukeketaji nao waandishi wa habari wakijikita kufichua chanzo cha ukeketaji katika jamii husika ni zipi itasaidia kukomesha pia ukeketaji.

Amesema ukatili wowote ule unapofanyika unamyima mtu kukosa uhuru na kinaleta athari za kisaikolojia miongoni mwa wahusika wa ukatili huo.

Naye Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),ambaye alikuwepo katika warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tamwa, Judica Losai, amesema kuwa wanahabari wanapaswa kuunganisha nguvu ili kufichua ukatili wa kijinsia ambao kwa sasa umeshika kasi
kubwa.

Amesema kinachopaswa kuzingatiwa katika uandishi wa habari za kufichu  ukatili wa kijinsia ni umakini, kuzingatia lugha ya kutumia na kuhakikisha waathirika wanapata msaada mwisho wa siku.

Amesema kuwa ukatili wa kijinsia nchini mkubwa ambao kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya za mwaka 2013 inaonyesha Mkoa wa Manyara unaongoza ukeketaji kwa asilimia 71, ikifuatiwa na Dodoma asimilia 64 na Arusha asilimia 59.

Thursday, February 12, 2015

SERIKALI IMEANZA KUSAMBZA NAKALA MILIONI MBILI ZA KATIBA INAYOPENDEKEZWA NCHINI NZIMA

                                    Waziri wa Katiba na Sheria Dkt, Asha Rose Migiro

Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.

Mikoa hiyo na nakala ziliozosambazwa katika mabano ni Katavi (15,640), Rukwa (27,040), Ruvuma (47,740), Mbeya (78,640), Simiyu (34,840), Mara (52,540), Tabora (58,540) na Kigoma (41,440). Mikoa mingine ni Kagera (54,340), Geita (36,940), Mwanza (57,040) na Pwani ambapo usambazaji umeanza kwa wilaya ya Mafia ambayo imepata nakala 2,400.

Idadi ya nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa, ndiyo maana baadhi ya mikoa unaona imepata nakala nyingi,” amesema Dkt. Migiro ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya waandishi wa Habari waliotaka ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa katika kazi ya uchapishaji na uasambazaji wa nakala za Katiba Inayopendekezwa.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, kuna zaidi kata 3,800 nchini kote na lengo la Serikali ni kusambaza nakala 300 katika kila kata ambazo zitasambazwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.

Kuhusu taasisi za elimu na dini, Waziri Migiro amesema Serikali imepanga kusambaza nakala 658,400 kwa taasisi za elimu, dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia na kuwa usambazaji huo utaanza hivi karibuni.

Pamoja na usambazaji huo, Waziri Migiro amewakumbusha wananchi ambao bado hawajapata nakala za Katiba Inayopendekezwa, kuisoma kupitia tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria (www.sheria.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (www.agctz.go.tz).

Tuesday, February 10, 2015

TANZANIA YASHUTUMIWA KUWAFADHILI WAASI WA FDLR KUPANGA MASHAMBULIZI CONGO

                      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaJakaya Kikwete
 Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa mikutano nchini humo.

Taarifa hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa wakikutana nchini Tanzania.

Hata Hivyo katika kujibu madai hayo serikali ya Tanzania ilikanusha kabisa kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi yake na wapiganaji wa FDLR.

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUENDELEA NA BIASHARA WAKATI MWENYEKITI WAO AKIFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

  Mwenyekiti wa wafanyabiashara Tanzania Johnson Minja
Wafanya biashara nchini wametakiwa kuendelea kufanya biashara zao wakati mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara Johnson Minja akipandishwa kizimbani leo mjini Dodoma nchini Tanzania.
Wito huo umetolewa jana na Minja wakati akifungua kikao cha 

Halamshauri Kuu ya Taifa ya Jumuiya hiyo kilichofanyika mjini hapa ambapo alisema tayari viongozi wa ngazi za juu wa Jumuiya hiyo wameshawasili kuhudhuria kesi hiyo.

“Ni siku moja tu kabla ya siku ya kesi ambayo imefunguliwa Dodoma, jumuiya ya wafanyabiashara wanahudhuria kesi kwa pamoja kama taifa,” alisema Minja na kuongeza kuwa,

“Lakini pia, kumekuwa na muunganiko wa watu wengi ambao wanataka kujua maendeleo ya kesi na kitu gani kinaendelea, naomba wafanyabiashara wawe na amani na utulivu wakati kesi hiyo ikiwa inaendelea.”

Amesema tunaamini kwamba mahakama itatenda haki na mwisho wa siku yale ambayo tumejadiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali kwa ujumla, yanaweza kufanyiwa kazi kwa aajili ya manufaa na maslahi mapana zaidi ya Taifa , wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla.

Amesema, haitakuwa na maana kama viongozi wote watakuwa mahakamani na wafanyabiashara nao wakafunga maduka yao hali itakayosababisha wao na Serikali kukosa mapato na wananchi kukosa huduma.

“Haina maana sisi tuna kesi na wao waendelee kupoteza wanapofunga maduka yao, wao wanapoteza ,wananchi wanakosa huduma na Serikali inakosa mapato, kikubwa tunachoomba kwao ni sala, watuombee lakini wasisitishe huduma, ili watoe huduma kwa wananchi na Serikali ipate mapato,” alisema Minja

Vile vile amesema, kitendo cha wafanaybiashara kufunga maduka yao yao wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani,inaweza kusababisha Jumuiya hiyo kushindwa kufikia azma yao kwa Serikali ya mazungumzo katika kuwasaidia kufikia muafaka wa changamoto zinazowakabili , kwa njia ya majadiliano.

Leo Minja anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara ya pili, mara ya kwanza alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma mjini mnamo Januari 28 mwaka huu kwa tuhuma ya kuwachochea wafanyabiashara wasilipe kodi ya Serikali.

Pia Minja anatuhumiwa kwa kosa la kuwapa maelekezo wafanyabiashara ya kutotumia mashine za Kilektoniki (EFDs).

Sunday, January 25, 2015

MWIGIZAJI WA FILAMU ZA KISWAHILI ASHELY TOTO AZUA UTATA WA AMBER ROSE MITANDAONI PICHA ZAKE ZASAMBAA

jmmaa
Mwigizaji tena promoter wa muziki raia wa Kenya ambaye makao yake yako nchini Ujerumani, Ashley Toto, amewaacha midume vinywa wazi baada ya picha zake za kitandani kuvuja kwenye mitandao ya kijamii huku sehemu muhimu za mwili wake zikiwa wazi.
10893289_10205138225722838_1824582473_o
Ashley Toto anayetamba katika filamu ya Moyo wangu aliyo higiza pamoja na wasanii wa V.A.D Production nchini Danmark, alikuwa matembezini katika nchi ya Mweshimiwa Jakaya Kikwete kwa mipangilio ya mahandalizi ya kucheza filamu pamoja na waigizaji wa nchi hiyo ya Tanzania.

Thursday, January 22, 2015

JESHI LA POLISI LAZINDUA MPANGO WA KUKABILIA NA MAJAMBAZI GEITA,KAGERA NA KIGOMA

    Kamanda wa polisi mkoa we Kagera Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Henry Mwaibambe  
JESHI la Polisi mikoa ya Kigoma,Kagera na Geita limezindua mpango endelevu wa kuuangamiza mtandao wa uhalifu wa kutumia silaha kwa kuwatahadharisha wananchi kuepukana na tabia ya kuwakarimu wageni wanaowatilia mashaka na badala yake wawaripoti Polisi au kwa mamlaka zingine.

Tahadhari hiyo imetokana na baada ya wananchi wa Kitongoji cha Mhama, kijiji cha Ilyamchele Wilayani Bukombe Mkoani Geita Januari 19 mchana kujikuta wakiwakirimu majambazi wakiwemo kutoka nchi jirani kwa chakula na vinywaji wakidhania ni Askari wa hifadhi kutokana na nguo walizokuwa wamevaa kufanana na sare za Askari wa hifadhi kumbe ni majambazi kabla ya kuwageuka na kutoa silaha za kivita na kuwapora.

Sanjari na kuchukua tahadhari hiyo wananchi wameombwa kutoa ushirikiano kwa polisi kwa kutoa taarifa za siri zitakazoiwezesha polisi kuwanasa watu wote wanaoendesha vitendo vya uhalifu wakiwemo wanaowaficha na wanaoshirikiana na watu kutoka nchi jirani katika mikoa ya Kagera,Kigoma na Geita.
        Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Joseph Konyo
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Joseph Konyo amesema hayo leo baada ya kikao maalum kati ya Kamanda wa polisi mkoa we Kagera Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Henry Mwaibambe cha kuzindua mkakati kabambe wa kuusaka mtandao wa uhalifu kilichonfayika katika kijiji cha Nyakanazi Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera Juzi januari 20.
‘’Wananchi wabadilike ..kama siyo mjambazi hao kuingiwa na hofu baada ya kupata taarifa ya kuwepo porini kwa Kikosi cha kupambana na Uhalifu wa kutumia Silaha cha mkoani Geita majambazi hao wangeweza kufanya kufuru lakini kwa kuhofia hilo waliamua kufyatua risasi juu na kisha kuiba mchele kilo 60 na baiskeli tatu walizotumia kubebea mchele walioiba kabla ya kuzitupa kwa kuhofia kukutana na kikosi cha Antroberry’’alidai Konyo.

Aliongeza majambazi hao wanadaiwa walifika katika kijiji hicho wamevaa nguo zinazofanana na sare za Askari wa hifadhi na wanakijiji waliwakarimu kama watumishi wa serkali kwa kuwanunulia chakula na vinywaji lakini mwanakijiji mmoja aliwadokeza wenzake kuwa wale watu pamoja na kuvaa sare za Askari wa hifadahi kwa juu lakini ndani walikuwa wamevaa sare za jeshi kama la wananchi Jwtz lakini wenzake walimpuuza.

‘’Baada ya kukirimiwa pombe na chakula ghafla watu hao walitoa bunduki za kivita ikiwemo bunduki nzito inayodaiwa kuwa Light Mchine Gun[LMG]na kuwaamuru wananakijiji waliokuwepo kukaa chini ya ulinzi kwa muda kwa kufyatua risasi hewani na kisha kuondoka na kilo 60 za mchele na baiskeli tatu ambazo baadaye walizitupa wakihofia kunaswa’’alisema Konya
Wakati wakitoka eneo la tukio wakiondoka majambazi hao walichoma kibanda[Kijumba]kwa moto kwa lengo la kuwafanya wanakijiji wasiwafuate na badala yake washughulikie uzimaji moto kibanda kile na ndicho kilichofanyika na wakatumia fursa hiyo kutoweka huku wanakijiji wakiwarushia mishale bila ya mafanikio.
Kamanda Konyo alisema uchunguzi wa kiintelijensia umebaini watu hao walivuka na kuingia nchi jirani bila ya kuitaja kwa sababu za kiupelelezi…na ni sehemu ya mtandao ambao umekuwa unaedesha uhalifu katika mikoa ya Kagera,Kigoma na Geita huku pori la akiba la Kigosi lililopo wilayani Bukombe linalopakana na wilaya za Biharamulo mkoani Kagera na mkoa wa Kigoma likitumiwa kama maficho ya wahalifu hao.
Hata hivyo watu hao walitupa baiskeli hizo baada ya kuhofia kukutana na Askari wa kikosi maalum cha kupambana na Uhalifu wa kutumia silaha[Ant-robberry]na kufanikiwa kutokomea kabla ya Askari kufika eneo la tukio hata hivyo taarifa zilizokwishapatikana za kiintelijensia zimedaiwa zitasaidia kuunasa mtandao huo na kuwataka wahalifu wote kujisalimisha wao au silaha zao kwani siku zao zimehesabiwa kutoka sasa iwapo wananchi nao watasimama kidete kutoa ushirikiano kuwafichua wahalifu hao kwani wanawatambua na baadhi wanaishi nao.
Inasadikiwa mtandao huo ni sehemu ya mitandao ya uhalifu wa kutumia silaha iliyopo katika Miji ya Lunzewe,Namonge,Kasanda na Mabamba iliyopo katika mikoa ya Geita,Kagera na Kigoma na baada ya hapo huvuka na kuingia nchi jirani na hushirikiana na wenyeji ambao wao huratibu utekelezaji wa matukio hayo na wageni huja kutekeleza.
Kikosi nguvu kazi hicho kitakachowashirkisha makachero na wale wa Kikosi cha kupambana na unyang’anyi wakutumia silaha katika mikoa mitatu kitakuwa kiungo mhimu katika utekelezaji mkakati huo huku ukiwemo mfumo wa kubadilishana taarifa za uhalifu na zile za kikachero’’kiintelejensia’’katika mikoa hiyo mitatu kwa lengo la kuufyeka kabisa mtandao huo ambao umekuwa kero kubwa katika mikoa ya Geita,Kagera na Kigoma
Hata hivyo wadau waliohojiwa mkoani Geita kwa masharti ya kutotajwa majina yao juu ya hali ya uhalifu mkoani humo wamesema idadi ya matukio ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita kulikochangiwa na ushirikishwaji wa wananchi kwa kuhakikishiwa usalama wao katika kufichua uhalifu…baada ya kutoa taarifa za siri badala ya kusalitiwa na Askari wasio waadilifu kwa kuzigeuza kuwa dili.

Wamesema hatua hiyo inatokana na Timu madhubuti iliyopikwa na uongozi uliopo sasa wa polisi mkoani hapa kwa kurejesha imani kwa wananchikwa kuwalindawatoa taarifa za siri na kusikilizwa,pia kikosi cha Kuapambanana uhalifu wakutumia silaha kimekuwa imara wakati wote tofuati na awali.

Mwaka jana watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walivamia kituo kikuu cha polisi wilaya ya Bukombe Mkoani Geita na kuua Askari wawili na kupora silaha,lakini kutokana na ushirikiano kati ya polisi na wanachi watuhumiwa waliweza kukamatwa pamoja na silaha zote zilizokuwa zimeibiwa.

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...