WAY

Wednesday, April 8, 2015

MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO WATISHIA KUGOMA IJUMAA KWA MADAI YA KUFANYIA UNYANYASAJI

   Mabasi ya Abiria yakiwa yamepaki stand kusubiri

Madereva wa vyombo mbali mbali vya moto nchini Tanzania, wanakusudia kushiriki mgomo wa nchi nzima siku ya Ijumaa wiki hii, kuishinikiza serikali kuondoa kero mbali mbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa ajira za uhakika pamoja na agizo la kutaka madereva hao waende kusoma kila wanapotaka kuhuisha leseni zao za udereva.

Wakizungumza kupitia Katibu wa Muungano wa vyama vya Madereva Bw. Rashid Saleh, madereva hao wamesema kuwa suala la kurudia kusoma ni aina nyingine ya unyanyasaji kwa maelfu ya madereva nchini, ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa hawana mfumo mzuri wa ajira licha ya kutupiwa lawama kibao kuwa wao ndio chanzo cha ongezeko la ajali nchini.

Katibu huyo wa Muungano wa Vyama vya Madereva ameitaja kero nyingine kuwa ni hatua ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT kutamka hadharani kuwa vyeti walivyonavyo madereva hao sio halali na kwamba Ijumaa wiki hii wanakusudia kukutana na Waziri wa Kazi na Ajira kwa ajili ya kuzungumzia kero hizo kwa lengo la kuepusha kutokea kwa mgomo huo.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...