WAY

Monday, March 30, 2015

MUGABE AWATAKA VIONGZI WA AFRIKA KUACHA KUWA VIBARAKA WA MATAIFA YA ULAYA NA MAGHARIBI NA WAJISHUGHULISHE KUINUA WANANCHI WAO



     Rais wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe
Rais wa Zimbawe na Mwenyekiti wa umoja wa Africa Robert Gabriel Mugabe amewataka viongozi wa nchi za Africa kukataa kuwa vibaraka wa mataifa tajiri duniani na badala yake wajitoe katika kuwatumikia waafrika ili kufikia mafanikio ya kimaendeleo katika ustawi wa bara hili.

Rais Mugabe ametoa mwito huo wakati akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa viongozi Vijana kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika na China unaofanyika katika ukumbi wa mikotano wa Ngurdoto nje kidogo ya Jiji la Arusha.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo Rais Mugabe ametumia muda mwingi kuwaasa na kutoa mwito kwa viongozi hao vijana akisistiza kuwa Bara la Afrika linategemea mchango wa Fikra zinazojali uwajibikaji na nidhamu ya hali ya juu katika utumishi.

Awali akizungumza katika Mkutano huo,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta Jakaya Kikwete ameonyesha imani aliyoanayo kupitia mkutano wa viongozi vijana kutoka Afrika na Uchina kwamba utatoa fursa ya kutoka na maazimio yatakayokuwa na tija kwa mustakabali wa watu wote

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...