Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge
Mh. Jenista Mhagama
Serikali
leo imewasilisha mswada wa sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa
za Kulevya ya mwaka 2014, kutokana na tatizo hilo kuongezeka zaidi
kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1980 na kutishia uhai wa taifa kutokana
na vijana wengi kujiingiza katika biashara na matumizi ya dawa hizo.
Akiwasilisha
mswada huo Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na bunge
Mh. Jenista Mhagama amesema matumizi ya dawa za kulevya yameongezeka
ambapo takwimu zinaonyesha kuwa watumiaji wa dawa hizo kati ya
laki mbili na 20 hadi laki nne na 20 hapa nchini wengi wakiwa ni vijana
kati ya miaka 15 hadi 38.
Mh.
Mhagama amesema ili kurekebisha matatizo ya kimfumo katika udhibiti
ya dawa hizo serikali imekusudia kuanzisha chombo kinachojitegemea
chenye mamlaka ya kiutendaji ya kuchunguza, kupekua na kukamata
watuhumiwa tofauti na ilivyo tume kwa sasa.
0 comments:
Post a Comment