WELCOME TO GMBONGO BLOG

To keep the body in good health is a duty... otherwise we shall not be able to keep our mind strong and clear.

TANGAZA NASI SASA

Tuwasiliane kwa Email: gmbongo.chuma@gmail.com

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Keep you Entertained always

WE ARE HERE TO SERVE YOU

Habari na Burudani

WELCOME TO GMBONGO WORLD

Kwa habari za Burudani na zenye uhakika.

WAY

Friday, February 27, 2015

KILIMANJARO INAONGOZA KWA UKATILI WA KIJINSIA

 Wajumbe wa SHIVYAWATA baada ya kutoka Ziarani Austaria
VYAMA vya Watu wenye ulemavu nchini, wanakusudia kuishitaki serikali kwenye vyombo vya kimataifa, endapo mauaji ya watu wenye ulemavu wangozi (Albino) yataendelea.



Akizungumza leo kwenye warsha ya ujumuishaji wa watu wenye ulemavu, katika nyanja za maendeleo iliyowezeshwa na EDAN ambayo ni programu ya Jumuiya ya Makanisa Duniani, Mshauri wa mradi wa watu wenye ulemavu, kuhusu haki na maendeleo yao,Dk. Elly Macha amesema Tanzania imesaini

mkataba wa kutetea haki za watu wenye ulemavu,lakini imeshindwa kuwalinda na matokeo yake wanauwawa ovyo.



Amesema kuwa hali ya mauaji ikiendelea kuwa kama ilivyo sasa, wataelewa wazi kuwa serikali imewaacha peke yao na watalazimika kwenda kwenye vyombo vya kimataifa kuishtaki serikali kw akushindwa kuheshimu mkataba huo.



Aidha amesema kuwa mbali na hilo katika warsha hiyo wamkubaliana na kutoa wito kwa serikali kusimamia,kuelekeza, kutekeleza na kufuatilia ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika nyanja za maendeleo hususani, kuhakikisha sera,sheria, mipango na upatikanaji wa rasilimali unawezesha ujumuishaji wa masuala hayo.



Dk.Elly amesema kupitia warsha hiyo wametoa tamko la kulaani mauaji ya kinyama ya Albino yanayoendelea kutekelezwa kw akasi, hasa kanda ya ziwa na kuitaka serikali kuchukua hatua madhubuti kukomesha tatizo hilo.



Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude, amesema kuna kesi nyingi zimeamuliwa na wengine wamehukumiwa kunyongwa, ila mpaka sasa hakuna aliyenyongwa wapo magerezani,hivyo wanaomba hukumu ikitolewa

izingatiwe, kwani isionee huruma wahusika hao wanaoua wenzao kama wanyama.

Thursday, February 26, 2015

JELA MIAKA MAISHA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MINNE

 Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yusufu Chatambala (45) mkazi wa Kijiji cha Makutupa Kata ya Lupeta Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa la kumbaka mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minne.

Mwendesha mashtaka wa polisi Godwill Ikema ameiambia mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Feb 20 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Makutupa kilichopo Wilayani Mpwapwa ambapo alimbaka mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka minne

Mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha sheria za nchi chini ya Kifungu namba 130 (1) 2 (a) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu kama kilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.

Amesema kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumkamata alipokuwa akicheza na watoto wenzake jirani na nyumbani kwao kisha kumpeleka kwenye shamba la mahindi kisha kumbaka mtoto huyo na kusababishia majeraha na maumivu makali.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa Paschal Mayumba alimtia hatiani mtuhumiwa huyo leo baada ya kukiri kutenda kosa hilo.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mayumba amesema Mahakama inamhukumu kwenda jela kifungo cha maisha kwa kosa la kubaka mtoto ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wanaotenda makosa kama hayo.

MAHAKAMA KUU YAKALIA SHAURI LINALOTAKA SERIKALI KUTOA ULINZI KWA JAMII YA ALBINO.

 Mkurugenzi wa kituo cha haki za Binadamu Helen-Kijo Bisimba
Mahakama Kuu ya Tanzania imeshindwa kusikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kipindi cha miaka saba iliyopita,

shauri ambalo kituo hicho kinaitaka mahakama iilazimishe serikali kutoa ulinzi wa uhakika kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini maarufu kama albino.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, amesema hayo leo katika mahojiano na East Africa Radio na kufafanua kuwa kuchelewa kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa namna moja inaweza kuwa imechangia kuzorota kwa usalama dhidi ya jamii ya albino nchini.

Kwa mujibu wa Dkt. Bisimba, matukio ya ukatili dhidi ya albino nchini yanayoendelea hivi sasa yanahitaji mbinu na njia nyingi katika kukabiliana nayo, mojawapo ikiwa ni ulinzi wa uhakika kwa jamii hiyo ya Watanzania.

CHANGAMTO ZAENDELEA KULIKUMBA ZOEZI LA UANDIKISHAJI BVR, WANANCHI WAGOMEA MASHINE MPYA, UMEME WAKATIKA VITUO VYAFUNGWA MAPEMA KWA MASHINE KUKOSA CHAJI


     Mashine ya kisasa ya kujiandikisha kitambulisho cha kura
Uandikishwaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura Mkoani Njombe nchini Tanzania leo asubuhi lilisimama kwa muda katika baadhi ya vituo kutokana na wananchi kuzigomea mashine mpya zilizoongezwa kwa ajili ya Uandikishaji.

Akizungumza na East Africa Radio msimamizi wa mashine za BVR, Astori Mgwame amesema kuwa wananchi hao waligomea mashine hizo kwa kuwa zilikua hazina muendeshaji wa kuziendesha kwa ufasaha na kusema kuwa hawatajiandikisha mpaka wahakikishiwe kuwa kuna mtaalamu wa kuzitumia.

Mgwame ameongeza kuwa hali hiyo inatokana na changamoto waliyokuwa nayo ya kuwa na upungufu wa wa wataalamu wa kuziendesha mashine hizo hivyo kufanya zoezi kuenda taratibu kushinda ilivyotarajiwa.

Aidha amesema changamoto nyingine iliyojitokeza jana jioni mpaka kupelekea kufungwa kwa vituo hivyo mapema kabla ya wakati ni kukatika kwa umeme na mashine kuishiwa chaji na kuzima hivyo kushindwa kuendelea na zoezi hilo.

Mgwame amesema kuwa licha ya changamoto hizo kujitokeza lakini uandikishwaji huo bado unaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi ili kuweza kupata haki yao hiyo ya kujiandikisha.

ASKARI WATANO WAJERUHIWA VURUGU ZA IRINGA KATI YA ASKARI NA WANANCHI



     Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi
Askari watano wamejeruhiwa kufuatia vurugu zilizotokea  baina ya jeshi la polisi pamoja na wananchi katika mji wa Ilula kijiji cha dinginayo wilaya ya kilolo mkoani iringa pamoja na raia wawili kujeruhiwa.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi PUDENSIANA PROTAS amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tayari jeshi la polis linawashikilia watuhumiwa kumi na nane kwa mahojiano huku upelelezi ukiendelea.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 4 asubuhi na limesababisha kifo cha mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la mwanne mtandi na katika vurugu hizo kumesababisha uharibifu wa mali za jeshi la polisi ambayo ni gari,pikipiki pamoja na gari moja ambayo ilikuwa ni kielelezo katika kituo pamoja na kuharibu jingo la polis kwa kuvunja vioo.

Aidha kamanda amesema kuwa fujo hizo zilisababishwa na oparationi kuhusu uuzaji wa pombe za kienyeji na makosa mbalimbali kwa wananchi huku akiwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi ili kuepusha majanga kama hayo.

WATU KADHAA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MWANZA KWA TUHUMA ZA UTEKAJI WA MTOTO MWENYE ULEMAVU PENDO EMANNUEL


                             Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw. Magesa Mulongo
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Bw. Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika kumuiba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel mwenye umri wa miaka 4 katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza, Disemba 27 wamekamatwa.

Akizungumza leo wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya wa mkoa huo, Bw. Mulongo amesema watu wote waliohusika wamekamatwa na hivi sasa bado hawafahamu kama mtoto huyo yupo hai ama mfu.

Amesema kuwa wezi baada ya kumuiba mtoto Pendo walimleta katika hoteli moja Jijini Mwanza, kisha kuwakabidhi watu walionekana wanunuzi, lakini wote hao wamekamatwa akiwamo mmiliki wa hoteli hiyo.

Hata hivyo, amesema watu hao waliofanya uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mwisho aliyetoweka na mtoto huyo toka hotelini hapo akiendelea kutafutwa
 
Hata hivyo, alisema watu hao waliofanya uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mwisho aliyetoweka na mtoto huyo toka hotelini hapo akiendelea kutafutwa.

Mulongo hata hivyo hakuweza kuitaja hotel wala mmiliki wake na wangine waliohusika na tukio hilo lilitokea Desemba 27 mwaka jana, lakini Shilinde akituhumiwa kuhusika zaidi na tukio hilo kutokana na kuamua kufanya hivyo kwa sababu alikuwa ana watoto wawili albino.

Mkuu wa mkoa huyo aliwataka wakuu wa wilaya wapya, kuhakikisha kushughulikia changamoto za wapiga ramli, kuangalia utoaji wa vibali kwa waganga wa jadi ili kudhibiti matyukio ya utekaji na mauaji ya albino.

Hata hivyo, alishangazwa na maneno yanayotolewa na watu kuhusiana na mauaji hayo kuwa yanatokana na masuala ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.

Katibu wa chama cha maalbino mkoa wa Mwanza, Mashaka Tuju, aliishutumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua stahili tangu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yalipoanza miaka tisa iliyopita.

Amesema kwa miaka tisa serikali inahangaika na kudai inachukua hatua lakini hakuna hatua yoyote inayoonekana mpaka sasa huku albino wengi wakiwa wanaishi vijijini katika nyumba zisizo na ulinzi thabiti, lakini utakuta viongozi wa serikali wanaenda huko pale linapotokea tatizo la mauaji ya watu hao.

Tuju amewashambulia mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Antony Diallo, naibu waziri wa nishati na madini, Charles Kitwanga na mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu, kwa kushindwa kufanya juhudi zozote za kuwalinda na kuwatetea albino.

Katika kipindi cha miezi miwili, watoto Pendo Emmanuel wa Kwimba na Yohana Bahati (mwaka mmoja) wa kijiji cha Ilelema Chato, walitekwa na watu wasiojulikana.

Wednesday, February 25, 2015

WANAWAKE WANASHINDWA KUTAMBA KATIKA MUZIKI KUTOKANA NA UKIRITIMBA ULIOPO KATIKA TASNIA


         Deborah Nyangi akiitumikia Kalunde Band.
Mwanadada anaetamba na Band ya Kalunde Band, Deborah Nyangi ambae anatikisa na wimbo wake wa FINGO amesema wanawake wanashindwa kutamba katika game la muziki wa kizazi kipya kutoka na ukiritimba uliopo katika tasnia.

Nyangi amesema anaamini kuna vipaji vingi sana vya kuimba kwa watoto wa kike ila tayari wameshajenga woga wa kujitokeza kutokana na kuamini kwamba ukitaka kufanya vizuri lazima uhonge kama sio pesa basi hata kutumia mwili wake.

Nyangi ambae kwa sasa anajipanga kuachia wimbo wake mpya amewataka watoto wa kike wajiamini kwa kile wanachokifanya na wasikubali kuyumbishwa na watu wachache ambao wanajihisi wameshikilia game ila kazi nzuri ndio itawafikisha wanapotaka.

Tuesday, February 24, 2015

HAJI RAMADHANI AIBUKA NA BABY LOVE ASEMA ANAAMINI ITALETA MAPINDUZI KATIKA TASNIA YA MUZIKI ATAMBA KUACHIA NYIMBO BAADA YA NYIMBO

                
                  Haji Ramadhani Makuke akiwajibika Jukwaani
Msaanii wa Kizazi kipya alitokea kwenye mashindano ya kuibua vipaji Bss na sasa anatamba na band ya Twanga Pepeta Haji Ramadhani Makuke amekuja na ujio mpya wa kazi nje ya band yake na kuachia Singo mpya alioipa jina mpya la BABY LOVE.

Haji amesema nyimbo hiyo ina vionjo vya kiasili amesema ameitoa ili kuwaonyesha watanzania kipaji kingine tofauti katika uimbaji na pia kuleta ladha mpya katika muziki wa kizazi Kipya.

Hajji amesema ameamua kufanya kazi kwenye band na nje ya band kama Solo ili kujiongezea mashabiki na pia kubadilisha ladha ya mziki ila pia kujitafutia kipato kutokana kuuza nyimbo kwa mtindo wa singo kwa kuwa album kwa sasa ni ngumu kuuzika.

Monday, February 23, 2015

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO KUFICHUA MAUAJI YA ALBINO

                          Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano

 Waandishi wa habari nchini, wametakiwa kutumia kalamu zao kufichua chanzo cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, ambao umeibuka kwa kasi kubwa siku za karibuni.

Akizungumza leo Mjini Moshi na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, (TAMWA),kwa lengo la kufichua ukatili wa kijinsia, Mshauri wa vyombo vya habari, Deo Peter, alisema kuna hajana ya kufichua chanzo cha mauaji hayo.

Amesema inasikitisha kuona watu hao wanaendelea kuuwawa kikatili, huku waandishi wakijikita kuandika tu jinsi wanavyouwawa, bila kufanya utafiti kujua chanzo cha mauaji hayo ni nini, jamo ambalo halisaidii kukomesha kiini cha mauaji hayo.
 
Aidha amesema sambamba na hilo pia hata kwenye seuala la ukeketaji nao waandishi wa habari wakijikita kufichua chanzo cha ukeketaji katika jamii husika ni zipi itasaidia kukomesha pia ukeketaji.

Amesema ukatili wowote ule unapofanyika unamyima mtu kukosa uhuru na kinaleta athari za kisaikolojia miongoni mwa wahusika wa ukatili huo.

Naye Mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),ambaye alikuwepo katika warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tamwa, Judica Losai, amesema kuwa wanahabari wanapaswa kuunganisha nguvu ili kufichua ukatili wa kijinsia ambao kwa sasa umeshika kasi
kubwa.

Amesema kinachopaswa kuzingatiwa katika uandishi wa habari za kufichu  ukatili wa kijinsia ni umakini, kuzingatia lugha ya kutumia na kuhakikisha waathirika wanapata msaada mwisho wa siku.

Amesema kuwa ukatili wa kijinsia nchini mkubwa ambao kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya za mwaka 2013 inaonyesha Mkoa wa Manyara unaongoza ukeketaji kwa asilimia 71, ikifuatiwa na Dodoma asimilia 64 na Arusha asilimia 59.

Thursday, February 12, 2015

SERIKALI IMEANZA KUSAMBZA NAKALA MILIONI MBILI ZA KATIBA INAYOPENDEKEZWA NCHINI NZIMA

                                    Waziri wa Katiba na Sheria Dkt, Asha Rose Migiro

Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.

Mikoa hiyo na nakala ziliozosambazwa katika mabano ni Katavi (15,640), Rukwa (27,040), Ruvuma (47,740), Mbeya (78,640), Simiyu (34,840), Mara (52,540), Tabora (58,540) na Kigoma (41,440). Mikoa mingine ni Kagera (54,340), Geita (36,940), Mwanza (57,040) na Pwani ambapo usambazaji umeanza kwa wilaya ya Mafia ambayo imepata nakala 2,400.

Idadi ya nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa, ndiyo maana baadhi ya mikoa unaona imepata nakala nyingi,” amesema Dkt. Migiro ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya waandishi wa Habari waliotaka ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa katika kazi ya uchapishaji na uasambazaji wa nakala za Katiba Inayopendekezwa.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, kuna zaidi kata 3,800 nchini kote na lengo la Serikali ni kusambaza nakala 300 katika kila kata ambazo zitasambazwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.

Kuhusu taasisi za elimu na dini, Waziri Migiro amesema Serikali imepanga kusambaza nakala 658,400 kwa taasisi za elimu, dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia na kuwa usambazaji huo utaanza hivi karibuni.

Pamoja na usambazaji huo, Waziri Migiro amewakumbusha wananchi ambao bado hawajapata nakala za Katiba Inayopendekezwa, kuisoma kupitia tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria (www.sheria.go.tz) na tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (www.agctz.go.tz).

Tuesday, February 10, 2015

TANZANIA YASHUTUMIWA KUWAFADHILI WAASI WA FDLR KUPANGA MASHAMBULIZI CONGO

                      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaJakaya Kikwete
 Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa mikutano nchini humo.

Taarifa hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa wakikutana nchini Tanzania.

Hata Hivyo katika kujibu madai hayo serikali ya Tanzania ilikanusha kabisa kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi yake na wapiganaji wa FDLR.

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUENDELEA NA BIASHARA WAKATI MWENYEKITI WAO AKIFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

  Mwenyekiti wa wafanyabiashara Tanzania Johnson Minja
Wafanya biashara nchini wametakiwa kuendelea kufanya biashara zao wakati mwenyekiti wa jumuiya ya Wafanyabiashara Johnson Minja akipandishwa kizimbani leo mjini Dodoma nchini Tanzania.
Wito huo umetolewa jana na Minja wakati akifungua kikao cha 

Halamshauri Kuu ya Taifa ya Jumuiya hiyo kilichofanyika mjini hapa ambapo alisema tayari viongozi wa ngazi za juu wa Jumuiya hiyo wameshawasili kuhudhuria kesi hiyo.

“Ni siku moja tu kabla ya siku ya kesi ambayo imefunguliwa Dodoma, jumuiya ya wafanyabiashara wanahudhuria kesi kwa pamoja kama taifa,” alisema Minja na kuongeza kuwa,

“Lakini pia, kumekuwa na muunganiko wa watu wengi ambao wanataka kujua maendeleo ya kesi na kitu gani kinaendelea, naomba wafanyabiashara wawe na amani na utulivu wakati kesi hiyo ikiwa inaendelea.”

Amesema tunaamini kwamba mahakama itatenda haki na mwisho wa siku yale ambayo tumejadiliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali kwa ujumla, yanaweza kufanyiwa kazi kwa aajili ya manufaa na maslahi mapana zaidi ya Taifa , wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla.

Amesema, haitakuwa na maana kama viongozi wote watakuwa mahakamani na wafanyabiashara nao wakafunga maduka yao hali itakayosababisha wao na Serikali kukosa mapato na wananchi kukosa huduma.

“Haina maana sisi tuna kesi na wao waendelee kupoteza wanapofunga maduka yao, wao wanapoteza ,wananchi wanakosa huduma na Serikali inakosa mapato, kikubwa tunachoomba kwao ni sala, watuombee lakini wasisitishe huduma, ili watoe huduma kwa wananchi na Serikali ipate mapato,” alisema Minja

Vile vile amesema, kitendo cha wafanaybiashara kufunga maduka yao yao wakati kesi hiyo ikiendelea mahakamani,inaweza kusababisha Jumuiya hiyo kushindwa kufikia azma yao kwa Serikali ya mazungumzo katika kuwasaidia kufikia muafaka wa changamoto zinazowakabili , kwa njia ya majadiliano.

Leo Minja anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara ya pili, mara ya kwanza alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma mjini mnamo Januari 28 mwaka huu kwa tuhuma ya kuwachochea wafanyabiashara wasilipe kodi ya Serikali.

Pia Minja anatuhumiwa kwa kosa la kuwapa maelekezo wafanyabiashara ya kutotumia mashine za Kilektoniki (EFDs).

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...