Mkurugenzi wa kituo cha haki za Binadamu Helen-Kijo Bisimba
Mahakama
Kuu ya Tanzania imeshindwa kusikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa
na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kipindi cha miaka saba
iliyopita,
shauri
ambalo kituo hicho kinaitaka mahakama iilazimishe serikali kutoa
ulinzi wa uhakika kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini maarufu kama
albino.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo hicho Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, amesema hayo leo
katika mahojiano na East Africa Radio na kufafanua kuwa kuchelewa
kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa namna moja inaweza kuwa imechangia
kuzorota kwa usalama dhidi ya jamii ya albino nchini.
Kwa
mujibu wa Dkt. Bisimba, matukio ya ukatili dhidi ya albino nchini
yanayoendelea hivi sasa yanahitaji mbinu na njia nyingi katika
kukabiliana nayo, mojawapo ikiwa ni ulinzi wa uhakika kwa jamii hiyo
ya Watanzania.
0 comments:
Post a Comment