Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi
Askari watano wamejeruhiwa kufuatia
vurugu zilizotokea baina ya jeshi la polisi pamoja na wananchi
katika mji wa Ilula kijiji cha dinginayo wilaya ya kilolo mkoani
iringa pamoja na raia wawili kujeruhiwa.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi
PUDENSIANA PROTAS amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema
kuwa tayari jeshi la polis linawashikilia watuhumiwa kumi na nane kwa
mahojiano huku upelelezi ukiendelea.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 4
asubuhi na limesababisha kifo cha mwanamke mmoja aliyefahamika kwa
jina la mwanne mtandi na katika vurugu hizo kumesababisha uharibifu
wa mali za jeshi la polisi ambayo ni gari,pikipiki pamoja na gari
moja ambayo ilikuwa ni kielelezo katika kituo pamoja na kuharibu
jingo la polis kwa kuvunja vioo.
Aidha kamanda amesema kuwa fujo hizo
zilisababishwa na oparationi kuhusu uuzaji wa pombe za kienyeji na
makosa mbalimbali kwa wananchi huku akiwataka wananchi
kutokujichukulia sheria mkononi ili kuepusha majanga kama hayo.
0 comments:
Post a Comment