Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaJakaya Kikwete
Umoja
wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na
hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Ripoti
mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu
Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa
mikutano nchini humo.
Taarifa
hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi
wa FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa
wakikutana nchini Tanzania.
Hata
Hivyo katika kujibu madai hayo serikali ya Tanzania ilikanusha kabisa
kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake na
kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi
yake na wapiganaji wa FDLR.
0 comments:
Post a Comment