WAY

Friday, February 27, 2015

KILIMANJARO INAONGOZA KWA UKATILI WA KIJINSIA

 Wajumbe wa SHIVYAWATA baada ya kutoka Ziarani Austaria
VYAMA vya Watu wenye ulemavu nchini, wanakusudia kuishitaki serikali kwenye vyombo vya kimataifa, endapo mauaji ya watu wenye ulemavu wangozi (Albino) yataendelea.



Akizungumza leo kwenye warsha ya ujumuishaji wa watu wenye ulemavu, katika nyanja za maendeleo iliyowezeshwa na EDAN ambayo ni programu ya Jumuiya ya Makanisa Duniani, Mshauri wa mradi wa watu wenye ulemavu, kuhusu haki na maendeleo yao,Dk. Elly Macha amesema Tanzania imesaini

mkataba wa kutetea haki za watu wenye ulemavu,lakini imeshindwa kuwalinda na matokeo yake wanauwawa ovyo.



Amesema kuwa hali ya mauaji ikiendelea kuwa kama ilivyo sasa, wataelewa wazi kuwa serikali imewaacha peke yao na watalazimika kwenda kwenye vyombo vya kimataifa kuishtaki serikali kw akushindwa kuheshimu mkataba huo.



Aidha amesema kuwa mbali na hilo katika warsha hiyo wamkubaliana na kutoa wito kwa serikali kusimamia,kuelekeza, kutekeleza na kufuatilia ujumuishaji wa watu wenye ulemavu katika nyanja za maendeleo hususani, kuhakikisha sera,sheria, mipango na upatikanaji wa rasilimali unawezesha ujumuishaji wa masuala hayo.



Dk.Elly amesema kupitia warsha hiyo wametoa tamko la kulaani mauaji ya kinyama ya Albino yanayoendelea kutekelezwa kw akasi, hasa kanda ya ziwa na kuitaka serikali kuchukua hatua madhubuti kukomesha tatizo hilo.



Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude, amesema kuna kesi nyingi zimeamuliwa na wengine wamehukumiwa kunyongwa, ila mpaka sasa hakuna aliyenyongwa wapo magerezani,hivyo wanaomba hukumu ikitolewa

izingatiwe, kwani isionee huruma wahusika hao wanaoua wenzao kama wanyama.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...