Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, Bw. Magesa Mulongo
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza, Bw. Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika
kumuiba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel mwenye
umri wa miaka 4 katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza,
Disemba 27 wamekamatwa.
Akizungumza
leo wakati akiwaapisha wakuu wapya wa wilaya wa mkoa huo, Bw. Mulongo
amesema watu wote waliohusika wamekamatwa na hivi sasa bado
hawafahamu kama mtoto huyo yupo hai ama mfu.
Amesema
kuwa wezi baada ya kumuiba mtoto Pendo walimleta katika hoteli moja
Jijini Mwanza, kisha kuwakabidhi watu walionekana wanunuzi, lakini
wote hao wamekamatwa akiwamo mmiliki wa hoteli hiyo.
Hata
hivyo, amesema watu hao waliofanya uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto
huyo, Emmanuel Shilinde, wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mwisho
aliyetoweka na mtoto huyo toka hotelini hapo akiendelea kutafutwa
Hata hivyo, alisema watu hao waliofanya
uhalifu huo akiwamo baba wa mtoto huyo, Emmanuel Shilinde,
wanashikiliwa na polisi huku mtu wa mwisho aliyetoweka na mtoto huyo
toka hotelini hapo akiendelea kutafutwa.
Mulongo hata hivyo hakuweza kuitaja
hotel wala mmiliki wake na wangine waliohusika na tukio hilo
lilitokea Desemba 27 mwaka jana, lakini Shilinde akituhumiwa kuhusika
zaidi na tukio hilo kutokana na kuamua kufanya hivyo kwa sababu
alikuwa ana watoto wawili albino.
Mkuu wa mkoa huyo aliwataka wakuu wa
wilaya wapya, kuhakikisha kushughulikia changamoto za wapiga ramli,
kuangalia utoaji wa vibali kwa waganga wa jadi ili kudhibiti matyukio
ya utekaji na mauaji ya albino.
Hata hivyo, alishangazwa na maneno
yanayotolewa na watu kuhusiana na mauaji hayo kuwa yanatokana na
masuala ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu.
Katibu wa chama cha maalbino mkoa wa
Mwanza, Mashaka Tuju, aliishutumu serikali kwa kushindwa kuchukua
hatua stahili tangu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino)
yalipoanza miaka tisa iliyopita.
Amesema kwa miaka tisa serikali
inahangaika na kudai inachukua hatua lakini hakuna hatua yoyote
inayoonekana mpaka sasa huku albino wengi wakiwa wanaishi vijijini
katika nyumba zisizo na ulinzi thabiti, lakini utakuta viongozi wa
serikali wanaenda huko pale linapotokea tatizo la mauaji ya watu hao.
Tuju amewashambulia mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Mwanza, Antony Diallo, naibu waziri wa nishati na madini,
Charles Kitwanga na mbunge wa Magu, Dk. Festus Limbu, kwa kushindwa
kufanya juhudi zozote za kuwalinda na kuwatetea albino.
Katika kipindi cha miezi miwili, watoto
Pendo Emmanuel wa Kwimba na Yohana Bahati (mwaka mmoja) wa kijiji cha
Ilelema Chato, walitekwa na watu wasiojulikana.
0 comments:
Post a Comment