Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano
Waandishi
wa habari nchini, wametakiwa kutumia kalamu zao kufichua chanzo
cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino, ambao umeibuka
kwa kasi kubwa siku za karibuni.
Akizungumza
leo Mjini Moshi na waandishi wa habari kwenye warsha ya siku
tatu iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania,
(TAMWA),kwa lengo la kufichua ukatili wa kijinsia, Mshauri wa
vyombo vya habari, Deo Peter, alisema kuna hajana ya kufichua chanzo
cha mauaji hayo.
Amesema
inasikitisha kuona watu hao wanaendelea kuuwawa kikatili, huku waandishi
wakijikita kuandika tu jinsi wanavyouwawa, bila kufanya utafiti
kujua chanzo cha mauaji hayo ni nini, jamo ambalo halisaidii kukomesha
kiini cha mauaji hayo.
Aidha amesema sambamba na hilo pia hata
kwenye seuala la ukeketaji nao waandishi wa habari wakijikita kufichua
chanzo cha ukeketaji katika jamii husika ni zipi itasaidia
kukomesha pia ukeketaji.
Amesema ukatili wowote ule unapofanyika
unamyima mtu kukosa uhuru na kinaleta athari za kisaikolojia
miongoni mwa wahusika wa ukatili huo.
Naye Mwakilishi wa Chama cha Waandishi
wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),ambaye alikuwepo katika warsha
hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tamwa, Judica Losai, amesema kuwa
wanahabari wanapaswa kuunganisha nguvu ili kufichua ukatili wa kijinsia
ambao kwa sasa umeshika kasi
kubwa.
Amesema kinachopaswa kuzingatiwa katika
uandishi wa habari za kufichu ukatili wa kijinsia ni umakini,
kuzingatia lugha ya kutumia na kuhakikisha waathirika wanapata msaada
mwisho wa siku.
Amesema kuwa ukatili wa kijinsia nchini
mkubwa ambao kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya za mwaka
2013 inaonyesha Mkoa wa Manyara unaongoza ukeketaji kwa asilimia 71,
ikifuatiwa na Dodoma asimilia 64 na Arusha asilimia 59.
0 comments:
Post a Comment