Mwenyekiti wa wafanyabiashara Tanzania Johnson Minja
Wafanya biashara nchini wametakiwa
kuendelea kufanya biashara zao wakati mwenyekiti wa jumuiya ya
Wafanyabiashara Johnson Minja akipandishwa kizimbani leo mjini Dodoma
nchini Tanzania.
Wito huo umetolewa jana na Minja wakati
akifungua kikao cha
Halamshauri Kuu ya Taifa ya Jumuiya hiyo
kilichofanyika mjini hapa ambapo alisema tayari viongozi wa ngazi za
juu wa Jumuiya hiyo wameshawasili kuhudhuria kesi hiyo.
“Ni siku moja tu kabla ya siku ya
kesi ambayo imefunguliwa Dodoma, jumuiya ya wafanyabiashara
wanahudhuria kesi kwa pamoja kama taifa,” alisema Minja na kuongeza
kuwa,
“Lakini pia, kumekuwa na muunganiko
wa watu wengi ambao wanataka kujua maendeleo ya kesi na kitu gani
kinaendelea, naomba wafanyabiashara wawe na amani na utulivu wakati
kesi hiyo ikiwa inaendelea.”
Amesema tunaamini kwamba mahakama
itatenda haki na mwisho wa siku yale ambayo tumejadiliana na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) na Serikali kwa ujumla, yanaweza kufanyiwa
kazi kwa aajili ya manufaa na maslahi mapana zaidi ya Taifa ,
wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla.
Amesema, haitakuwa na maana kama
viongozi wote watakuwa mahakamani na wafanyabiashara nao wakafunga
maduka yao hali itakayosababisha wao na Serikali kukosa mapato na
wananchi kukosa huduma.
“Haina maana sisi tuna kesi na wao
waendelee kupoteza wanapofunga maduka yao, wao wanapoteza ,wananchi
wanakosa huduma na Serikali inakosa mapato, kikubwa tunachoomba kwao
ni sala, watuombee lakini wasisitishe huduma, ili watoe huduma kwa
wananchi na Serikali ipate mapato,” alisema Minja
Vile vile amesema, kitendo cha
wafanaybiashara kufunga maduka yao yao wakati kesi hiyo ikiendelea
mahakamani,inaweza kusababisha Jumuiya hiyo kushindwa kufikia azma
yao kwa Serikali ya mazungumzo katika kuwasaidia kufikia muafaka wa
changamoto zinazowakabili , kwa njia ya majadiliano.
Leo Minja anatarajiwa kufikishwa
mahakamani kwa mara ya pili, mara ya kwanza alifikishwa katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma mjini mnamo Januari 28 mwaka huu
kwa tuhuma ya kuwachochea wafanyabiashara wasilipe kodi ya Serikali.
Pia Minja anatuhumiwa kwa kosa la
kuwapa maelekezo wafanyabiashara ya kutotumia mashine za Kilektoniki
(EFDs).
0 comments:
Post a Comment