WAY

Thursday, January 17, 2013

BAADA KIMYA KIREFU BWANA MISOSI AIBUKA KIVYINGINE SAFARI HII AIBUKIA KATIKA STYLE YA KIAFRICA ZAIDI LAKINI VILE VILE AJITOSA KWENYE FILAMU ASEMA ANATAKA KUWA WA KIMATAIFA ZAIDI

MSANII wa kizazi  kipya aliewahi kutamba na nyimbo kama NITOKE VIPI,HESHIMA,na nyingine kibao baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kumbe kimya kingi kina mshindo mkuu sasa aibuka na style nyingine kabisa na wimbo wake umeanza kutikisa katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni wimbo ukiwa unaitwa IWEJE ambao ameimba katika mahadhi ya zouk ya asili kabisa amesema kwa yeye ana vipaji kibao hapo ameonyesha tu na kusema pia watu wasimkariri kwa style moja kwa anaweza ufanya kila aina ya muziki ila anaamini muziki wa kiafrica ndio wa kimataifa zaidi.
                                                    BWANA MISOSI
MISOSI amesema kazi yake hiyo imekubalika na wengi hata prof jay amempongeza kwa kubadilika huko na kumwambia kaze buti.

lakini vile vile misosi amesema kwa sasa yupo chini ya usimamzi wa kampuni ya hm ambao wanamsimamia kazi zake kwa hiyo mwaka huu utakua wake kwa kuwa amejiandaa vya kutosha na tazidi kuwashangaza watanzania kwa kazi ambazo atazitoa hapo mbeleni.
                                        MISOSI AKIWA NA MPENZI WAKE AMANDA PIA BWANA MISOSI amesema pia maeingia kwenye tasnia ya filamu na hvi karibuni ataibuka na vile moja kali ingawa amesema ni mapema mno kusema amefanya na nani ila kwa mwaka amesema atatimiza ndoto yake kufanya filamu kwa kuwa anaamini ana kipaji hicho cha uigizaji

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...