WAY

Wednesday, December 12, 2012

IRENE UWOYA: AFUNGUKA NA KUSEMA KUWA KWA MWAKA 2012 HAJAFANIKIWA KABISA KATIKA MIPANGO YAKE KATIKA FILAMU




STAA wa filamu ambaye popote atakapopita shabiki lazima amshangae, Irene Uwoya, anasema kuwa mwaka 2012 unamalizika lakini asilimia kubwa ya mambo yake hayakutimia.

Anasema ndoto zake kubwa katika tasnia ya filamu ambazo kwa asilimia fulani anaamini hajazikamilisha, atazikamilisha mapema mwakani.

Kwa sasa kuna changamoto nyingi sana katika tasnia ya filamu ambazo kama msanii unatakiwa kuzikabili katika kulinda maslahi," alisema.

"Imenilazimu kupunguza muda wa kazi ili kupumzika na kufikiria filamu mpya ambayo itakuwa bora."

Irene anasema moja ya njia ya kuongeza maslahi kwa msanii wa filamu ni pamoja na kumiliki kampuni itakayojishughulisha na kazi ya kurekodi filamu na kufanya kazi za kampuni yake kwa kiwango kikubwa.

Kwa sasa watayarishaji wengi wanajitahidi kumiliki kampuni za utengenezaji wa filamu katika kujiongezea maslahi zaidi.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...