WAY

Tuesday, October 30, 2012

JACKLINE PENTEZEL a.k.a JACK MABANGO a.k.a JACK MABANGO :ASEMA KWA KIWANGO CHAKE SASA NA JINSI SANAA INAVYOKWENDA KWA SASA BILA MILIONI SITA SICHEZI FILAMU.



Kama ni mpenzi  wa kucheki filamu za Kibongo, haina shaka utakuwa unaifahamu orodha ndefu ya mastaa wa kike wanaofanya vizuri kwenye tasnia  hiyo.

Kwenye exclusive interview aliyofanya mwishoni mwa wiki iliyopita staa wa Jumba la Dhahabu, Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuzi’, amefunguka kuwa sasa anajihisi milionea kufutia mshiko hevi anaoingiza kwa mwaka kupitia  uigizaji.





Jack wa Chuzi ‘super star’ wa muvi asiyekaukiwa matukio ameiarifu media kuwa sasa anauhakika wa kuingiza kiasi cha shilingi za kibongo milioni 18 kwa mwezi  kupitia malipo ya shilingi milioni 6 kwa kila muvi anayoigiza.


“Kwa sasa mtu akija na kazi yake sichezi chini ya shilingi milioni 6, ni kiwango ambacho ninaamini kiko kwenye hadhi yangu, ninafuraha kwa sababu sasa najihisi milionea”  alisema Jack wa Chuz.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...