2
WASANII nchini wametakiwa
kujiunga katika mfuko wa pesheni kwa watumishi wa
umma –PSPF-ili waweze kujiwekea akiba kwa maaisha
yao ya baadae.
Hayo yamesemwa leo
jijini Dar es Salaam na Meneja msaidizi mpango wa
uchangiaji wa hiari –PSPF-Matilda Nyallu wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na semina ya
wasanii hao inayotarajiwa kufanyika februari 21
mwaka huu.
Matilda amesema
kuwa katika semina hivyo ambayo wataitoa kwa
wasanii inalengo la kuwashawishi kujiwekea
akiba ambayo itamsaidia kwa baadae kwa sababu asilimia
kubwa ya wasanii hawana akiba ya baadae.
Amesema kuwa kabla
ya kuwashawishi kujiunga na mfuko huo watatoa
elimu ili waweze kuelewa kwa undani umuhimu
wa kujiwekea akiba.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa bongo movie Stivu Nyerere amesema kuwa
kinachotakiwa wasanii wajitambue pamoja na kuitaka serikali
iweke sheria kali kwa watu wanaoiba
kazi za wasanii kwa sababu wanachangia kurudisha
nyuma maendeleo ya wasanii.
Aidha amewataka wasanii
wa hapa nchini waungane kwa pamoja na kupinga
hatua ya kuuza hati miliki ya kazi zao kwa
sababu zinachangia kwa asilimia kubwa kukosa haki zao za
msingi za kazi wanazofanya
0 comments:
Post a Comment