WAY

Tuesday, March 25, 2014

JE WAJUA MITIHANI ALIYOPITA DOGO RAMA KATIKA MUZIKI JE WAJUA ASHAWAHI KUWA ANAPANDA JUKWAANI AKIMBA SAUTI HAITOKI NA MARA NYINGINE HATA KUKOHOA DAMU HIYO WAKATI AMEINGIA TU TWANGA PEPETA JE WAJUA ALIKUWA MPIGA DEBE NA MCHOMA CHIPS JIJINI MWANZA KUPITA BLOG HII AMEFUNGUKA

Dogo rama mwanamuziki anaesimama vizuri kwa sasa ndani ya twanga pepeta katika safu ya uimbaji akishirikiana kwa ukaribu na kina kalala junior, luiza mbutu,badi bakule na wengineo anasema katika changamoto ambazo hawezi kuzisahau maishani mwake ni pamoja kuamini alikuwa anarogwa pindi tu alipifika twanga pepeta huku akiwashukuru kina Marehemu MCD,ABUU SEMHANDO lakini pia kina JOJOO JUMANNE NA LUIZA MBUTU kwamba avumilie na ndio mapka leo yupo twanga.
Kwa mujibu wa maelezo ya dogo rama mwenyewe anasema wakati anafika twanga pepeta mwanzoni kabisa ambapo kipindi hicho alikuta twanga imekamilika walikuwepo kina Chalz baba,kalala junior,khalid chokoraa,furguson,amigolas na wengine sasa walati huo akitafuta nafasi alijikuta wakati mwingine akikohoa damu baada ya kushuka jukwaani lakini pia kuna kipindi sauti ilikua inakauka bila kujielewa na kusema alipata wakati mgumu sana wakati huo lakini baadae akweza kueleweka na kutokatamaa na ndio mpka leo bado yupo twanga,


Lakini changamoto nyingine ambayo anasema anaikumbuka sana ni pamoja na kupiga debe jijini mwanza pia kuchoma chips na kushona viatu yote akitafuta pesa ili aweze kutoka na hatimae ndipo alipoweza kuanza uimbaimba katika mabdn tofauti tofauti jijini mwanza na hatimaye ndipo alipoweza kuja dar na kuendeleza kazi aliyokuwa akiwaaza na kuiota kila siku,

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...