WAY

Wednesday, March 19, 2014

MSANII WA FILAMU KUTOKA KENYA ANAEFANYA SHUGHULI ZAKE NCHINI UJERUMANI AKANA KUWA DEMU WA WASANII NA AKANUSHA MADAI YA KUTAKA KUIVUNJA NDOA YA BOB JOUNIOUR ASEMA WASANII WA AAFRIKA MASHARIKI YEYE NDIO HUWA ANAWAPA SAPPORT WAFIKAPO UJERUMANI

Msanii naekuja juu katika tasnia ya filamu afrika mashariki ambae anafanya shughuli zake ujerumani ASHLEY TOTOO amefunguka kuhusiana na skendo yake inayomkabili kuwa ni demu wa wasanii wa kutoka afrika mashariki ambao huwa wanaenda kufanya show nchini ujerumani na kusema kuwa yeye kule huwa anakua kama mwenyeji wao wa kuweza kuwatembeza sehemu mbalimbali ni marafiki wakawaida na wala si kama watu wengine wanavyofikiria kuwa kila msanii anaenda nchini humo basi lazima atoke na ashley.



Mbali na hilo pia ashley amekana kama alihusika na na kutaka kuvunja ndoa ya bob junior kwa kuwa ye alikua karibu nae kipindi amekuja nchini kenya na kusema kuwa wasanii wengi wa afrika mashariki ni rafiki zake na sio bobo jounior tu ila kuna kina ALLY KIBBA na wengineo kwa maswala ya bob juniour na mkewe ilikua ni mambo yao ya ndani wenyewe wala yeye hakuhusikaka kama ilivyokua imesambaa katika vyombo vya habari.
Kwa sasa amesema ameconcetrate katika kuandaa movies yake mpya ambayo atafanya na wasanii wa tanzania ili kuweza kupanua zaidid soko la filamu la afrika mashariki huku akiamini kuwa tanzania imepiga hatua kubwa katika tasnia ya swahili filamu afrika mashariki.

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...