WAY

Sunday, March 11, 2012

UJIO MPYA WA NDANDA KOSOVI NA WATOTO WA TEMBO AACHIA MBILI HEWANI NA AJIPANGA NA ALBUM

Nani anependa muziki wa dansi na hamjui ndanda kosovo kichaa mtaalamu wa muziki wa dansi aliewahi kutikisa nchini kwa rap na vibao tofauti tofauti toka akiwa fm academia international kipindi hicho kbla ya kutawanyika na mafahari wawili yaani ndanda na nyoshi kila mmoja kushika hamsini zake basi yeye ndio aliweza kukitunga kibao cha kwanza cha fm academia baada ya kutoka jela kipindi hicho akiwa na kina NYOSHI EL SADAAT,MALUU STONCH,MULE MULE FBI,KING BLAIZE,PATCHO MWAMBA na wengina kama KINA CARDINAL GENTO hapo walitamba na kibao cha WAJELAJELA  lakini baadae ndanda alitoka fm academia na ikaundwa fm academia wajelajela gwaa na ndanda akaanzisha STONO MUSICA yyeye akiita wajelejela Original ambapo aliweza kutamba na kina MALUU STONCH,CHAI JABA,PATCHO MWAMBA NA WENGINE ambapo vibao vilivyoweza kutamba kipindi hicho kikiwemo BINADAMU ambapo ni utunzi wake ndanda huku wakitamba na RAP ZA KIDEDEA,NA KAOKOTA BI G
          NDANDA KOSOVO KICHAA KIONGOZI WA WATOTO WA TEMBO
Ndanda hakuishia hapo aliweza kuachana na stono musica na kuelekea nchini marekanai ambapo kwa mujibu wa yeye mwenyewe aliweza kwenda kwa shughuli za kimuziki ambazo zilikua na mafaniko makubwa sana na baadae akarejea nchini tanzania ambapo akawa anaendela na shughuli za kawaida lakni ndipo hapo alipoweza kuanzisha kundi la watot wa tembo kwa mara ya kwanza ambapo aliweza kuchukua wanamuziki toka kcongo ambao mwisho wa siku waliweza kumkimbia kutokana na kutoelewana ambao wote wamekimbilia mashujaa musica ambao nao kwa sasa wapo kweye ramani ya muziki wa dansi na kutishia band nyingine kongwe!
      NDANDA KOSOVO AKIWA NA WATOTO WA TEMBO AKIPIGA SHOW
 Yote ya yote sasa ndanda kosovo kwa sasa maeachia nyimbo mbili ambazo zinasumbua katika vituo mbalimbali vya radio na televisheni moja ambayo itabeba jina la album akiipa jina la FOCUS kwa kiswahili kizuri alisema malengo na nyingine akiita KWANINI ambazo moja maepiga katika mtindo wa sebene tupu huku nyingine akipiga katika mtindo wa rhumba sebene huku akisema  mashabaiki ambao wanasema ndanda amekwisha basi wasikilize ujio mpya wa wa album yake ambapo atakua na watoto wa tembo!
    NDANDA  AKIWA NA WANAE KAZINI
JE NDANDA ANAWEZA KUWA AMERUDI AU NDIO SIKIO LA KUFA  AU KIMYA KINGI 

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...