WAY

Monday, March 12, 2012

JE WAJUA ALIPO STAR WA MUZIKI WA DANSI WAZIRI SONYO BAADA YA KUTOKA JELA SASA ANARUDI KIVINGINE NA BAND NYINGINE

Aliewahi kutamba na band ya T.O.T plus kipindi hicho ikiwa chini ya LE GENERAL BANZA STONE wakati huwa akiwa na TOTO TUNDU NA ABDUL MISAMBANO  Band ambayo ilitikisa ulimwengu wa dansi nchini kwa vibao kama MTAJI WA MASIKINI,ELIMU YA MJINGA lakini ukiacha yote hayo kibao kilichowahi kushika hatu ya muziki ni MASIMANGO ambacho kilitungwa na WAZIRI SONYO a,k.a KOMANDO sasa amerudi tena baada ya kutoka jela .WAZIRI SONYO alishwahi kutamba na band kama MVIKO SOUND,T.O.T PLUS,.AFRICAN REVOLUTION NA NYINGINE KIBAO KIBAO
      WAZIRI SONYO ENZI ZAKE AKITIA MASAUTI
Kwa sasa WAZIRI SONYO yupo mkoani Tanga ambapo yupo na band ya NYUMBANI CLASSIC BAND ambao itakua ni band ya hotel huku wakisubiri ukumbi wao mkubwa wa jijin Dar-es-salaam uishe ili wahamishie majeshi jijini na kuanza upinzani na band zinazotamba na kutikingisha jiji lakini kwa mujibu wa waziri sonyo amesema tayari wapo mbioni kuitoa album ya nyumbani clasic band ambayo itakua na nyimbo sita ikiwamo NAZIHESABU HATUA ZANGU ambao ni utunzi wake mwenyewe huku band hiyo ikiwa na mwanadada anaejulikana kwa jina la lady ambae ni mzoefu wa nyimbo za copy  inagawa vile vile akitegemea kutengeneza nyimbo ambayo itaingia katika album ya NYUMBANI CLASSIC BAND
    WAZIRI SONYO AKIWA NA LE GENERAL BANZA STONE WAKIKUMBUSHIA ENZI KIDOGO KABLA SONYO HAJAPATA BAND.
SONYOamesema pamoja na mashabiki wake kummis toka alivyoenda jela lakini kwa sasa anaamini kuwa mwanzo mzuri wa kung'ara tena ndio huu na mashabiki wake wavute subira mengi mazuri yaja kwa waziri sonyo na band yake ya NYUMBANI CLASSIC.
                          WAZIRI SONYO a.k.a komandoo!

0 comments:

Post a Comment

.

.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...